Geita, Mwanza: Mtoto afariki dunia baada ya kuliwa na fisi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
download.jpg

MTOTO mwenye umri wa miaka sita Joseph Simon[6]mkazi wa kijiji cha Buzanaki, Kata ya Nyamarimbe wilaya na mkoa wa Geita ameuawa na fisi na kisha kuliwa baadhi ya viungo vya mwili wake kabla ya familia kwa kushirikiana na wanakijiji kuokota mabaki ya mwili wake.

Wanakijiji wakishirikiana na familia husika walifanikiwa kuokota mabaki ya mwili wa mtoto huyo yakiwamo utumbo na kipande cha mfupa wa ambavyo vilizikwa kwa heshima kijijini Buzanaki na tayari fisi saba wameuawa katika nyakati tofauti katika oporesheni ya kuwasaka.

Ofisa wanyamapori wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Msese Kabulizina, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 2, mwaka huu zikiwa ni siku tatu tangu wakazi wengine wa Kijiji cha Idoselo Kata ya Luezela wilayani Geita nao kujeruhiwa na fisi kisha kulazwa katika Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Geita.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 2,wakati akitoka kuchuma embe zikiwa ni siku mbili tu baada ya wakazi wengine watatu wakazi wa kijiji tofauti cha Idosero Kata ya Luezera kujeruhiwa na fisi.

Walwa aliongeza kuwa tukio la kujeruhiwa watu watatu lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 29 usiku baada ya kundi la fisi wanaodaiwa kuwa zaidi ya wanne kuvamia nyumbani kwa mzee Magadula kisha kuishambulia familia hiyo kabla majirani kufika kutoa msaada na wao kujeruhiwa.

Aliongeza baada ya fisi hao kuvamia ndipo familia hiyo ilipopiga makelele kuomba msaada na majirani waliofika kwanza walikuwa ni Kulwa Jamoka na mwanaye Yohana Kulwa ambao katika kutoa msaada nao walijikuta wakijeruhiwa.

Hata hivyo, wakati makelele yakiendelea huku fisi nao wakishambulia wao na mbuzi nakumtafuna kabla ya umati wa wanakijiji kuongezeka na kuanza msako ambapo hadi Jumamosi walikuwa wameuawa fisi saba katika matukio tofauti kwa kusaidiana Idara ya Askari wanyamapori Halmashauri ya wilaya ya Geita.


Muungwana
 
jamani hivi geita ipo mjini au vijijini?
mi sijawah fika huko nnajua mjini cz kuna watu wananiambia wapo kikazi geita...kazi za maofisi makubwa.
 
jamani hivi geita ipo mjini au vijijini?
mi sijawah fika huko nnajua mjini cz kuna watu wananiambia wapo kikazi geita...kazi za maofisi makubwa.
Geita kubwa mamiiii, kuna mji(Geita mjin) pia kuna vijiji tena mapori haswaaa! hata me pia nipo kikaz huku, Chukua noti ya elfu 5 angalia utaona, huo mgodi ndo unatuweka mjin
 
Hii habari imenisikitisha sana. Mtoto amekufa kifo chenye mateso mengi. Pumzika kwa Amani Mtoto!
 
Back
Top Bottom