dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewasimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita (OCD),Mkuu wa Kituo cha Polisi Geita(OCS) na Mkuu wa Upelelezi Wilaya hiyo (OC CID),kwa kosa la Mahabusu kutoroka Mahakamani. Na pia ameelekeza Askari 8 wa kituo hicho wawekwe Selo.
Hivi karibuni Mahabusu 17 waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali walitoroka.
Mahabusu hao walikuwa wamewekwa katika ukumbi wa jengo jipya la mahakama wakisubiri kusomewa kesi zinazowakabili wametoroka Jumanne Mei 21, 2019.
Taarifa zinaeleza kuwa walitumia moja ya milango iliyokuwa katika jengo jipya la mahakama na kutoroka wakati askari wakiwa nje ya lango kuu la kuingia katika ukumbi huo.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Magereza (ACP), Robert Rumanyika akizungumzia tukio hilo alisema jeshi hilo halijaanza utaratibu wa kuwapeleka mahabusu mahakamani kama ilivyo kwa mikoa mingine na kwamba kwa sasa mahabusu wanaopelekwa mahakamani wanakuwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi.
Alipoulizwa kuhusu jambo hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema ni kweli wametoroka ila hakuweza kuzungumzia tukio hilo kwa undani kwa maelezo kuwa yupo katika ziara ya ufunguzi wa masoko ya dhahabu wilayani Geita.
zaidi, soma;

Geita: Mahabusu 17 watoroka Mahakamani
Jumla ya watuhumiwa 17 wa makosa mbalimbali waliokuwa wamehifadhiwa kwenye ukumbi wa jengo jipya la Mahakama ya Mkoa wa Geita kusubiri mashauri yao kutajwa mahakamani, wametoroka katika mazingira ya kutatanisha. Awali Mahabusu hao walikuwa wamehifadhiwa katika Ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi...
www.jamiiforums.com