Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ametoa msaada wa vitendea kazi vya michezo kwa wanamichezo wa Jimbo la Buchosa. Hafla hiyo ilifanyika katika kata ya Bupandwa, ambapo Shigongo alikabidhi mipira kwa ajili ya wanamichezo wa kata hiyo.
Shigongo alikuwapo kupitia diwani wa kata ya Bupandwa, Masumbuko Bupamba, na alisisitiza umuhimu wa wanamichezo kuendeleza vipaji vyao. Aliahidi kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanamichezo hao wanapata fursa ya kufikia malengo yao.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka wanamichezo hao kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika kutumikia wananchi wa Tanzania.