fmpiganaji, hili gazeti haliwezi hata siku moja kuiandika vizuri CDM kwa sababu ndio waliomfanya bosi wao ajiuzuru ubunge wa Igunga. Lakini pia 'Profesa' J. aliimba "ili nifanikiwe ninahitaji marafiki, ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui. Maadui wa CDM wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana (japo bila kulitambua hilo). M4C inatesa watu wengi sana, kwa kuona haraka unaweza kuona kuwa haijafanya kitu, ila kiukweli kuna kitu kikubwa sana kimefanyika, Vijana ambao bado wamenyimwa haki yao ya kupiga kura ni wangapi katika hizo kata, uandikishaji ulifanyika 2010. Siumizwi na wakala wa NYINYIEM (RAI) ila ni kuongeza umakini ktk M4C inayofuata.......
huyu jamaa alikuwa na jenerali ulimwengu ,salva rweyemamu , padri privatus karugendo ,muhingo na wengine tu enzi za gazeti la rai.
Baada ya kuuzwa wananunuzi wakafikri na waandishi akili zao pia wamezinunua ,jamaa wakaachia gazeti wakaanzisha raia mwema vichwa vyote vikahama.
Isipokuwa prince bagenda aliyepewa jukumu la kuandika makombora enzi za mh.kikwete .baada ya ushindi .salva rweyemam akapewa mwandishi wa rais ,bagenda ama misimamo yake ama hulka yake akaachwa ,wenzie wote wakahamia gazeti la raia mwema.
Bagenda nampenda namheshimu ila ana udhaifu wake anatumiwa ana misimamo mikali akishika kalamu akakaa chini kama uko ofisini utatafuta pa kutokea ,kumbukeni enzi za gazeti la rai kipindi cha mkapa ,ila cha muhimu shujaa mmoja akipotea huzaliwa wengine MwanaHalisi ikazaliwa ........
Prince Bagenda ameliangamiza kabisa RAI.Tangu aajiriwe sijawahi kununua hilo gazeti nu afadhali nisome magazeti ya udaku.
Bagenda ni mtu wa njaa sana!
Nimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.
Ebu niambie kosa la gazeti la Rai ni nini?
Hata mimi si mnunuzi wa gazeti hili toka limemilikiwa na Rostam Aziz kutoka mikononi mwa Jenerali Ulimwengu & Co.
Lakini ni lazima twende mbele na turudi nyuma kidogo. Si kila kinachozungumzwa negative kuhusu CDM ni kibaya kweli. Negativity nyingine ni sehemu ya kujenga. Huwezi kuwa na taasisi Malaika isiyokosea au kuhitaji kukosolewa. Hii habari haiwezi kuwa shambulio.
Tunaweza tukabeza habari hii ya gazeti la RAI lakini principally unapoendesha project lazima uzingatie uwiano wa input na output. Kilichofanywa na gazeti la RAI ni kupima mambo hayo. Sasa kinachotakiwa kufanywa na CDM ni kukanusha kwa kuegemea mizania hiyohiyo ya INPUT na OUTPUT. Sasa suala linahojiwa na RAI ni Je Input ya CDM kwenye chaguzi hizo za udiwani inaona na output? Hapo ndipo pa kuanzia kujadili na kupatolea ufafanuzi.
Tukianza kushambulia gazeti bila kuona mantiki ya kilichoandikwa tutakuwa tunakosea sana na huko si kukisaidia chama.