GAZETI LA UHURU: 'Tumechoka' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GAZETI LA UHURU: 'Tumechoka'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Friday, 29 July 2011

  NA KULWA MAGWA, DODOMA

  KWA mara ya pili katika kipindi cha siku mbili, wabunge wa CHADEMA wameendelea kulikosea heshima Bunge, ambapo watatu walitimuliwa ndani ya ukumbi jana.

  Juzi mbunge wa chama hicho katika jimbo la Nyamagana, Ezekia Wenje, alifukuzwa na Mwenyekiti wa Bunge kutokana na kutokutii amri ya kiti cha spika iliyomtaka kukaa chini, ambapo aliendelea kuzungumza. Tukio la aina hiyo lilijirudia jana, ambapo wabunge Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) walifukuzwa ukumbini.

  Uamuzi wa jana ulifikiwa na Naibu Spika, Job Ndugai, aliyeamuru askari wa Bunge wawatoe nje na kuwasimamia hadi watakapoondoka kwenye viwanja vya Bunge. Ndugai alimuru wabunge hao waondolewe baada ya kushindwa kutii amri yake, walipokuwa wakidai muongozo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, akizungumza. Bila ruhusa ya naibu spika, wabunge hao waliwasha vipaza sauti na kuomba muongozo, huku Ndugai akizungumza.

  Wakati Lukuvi akiendelea kuzungumza, wabunge hao waliwasha vipaza sauti na kuomba muongozo, wengine wakilalamika, huku wenzao wa upinzani wakishangilia, jambo lililosababisha utulivu uliokuwepo kutoweka. Kitendo hicho kilimuudhi Ndugai, ambaye asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu, alitoa darasa kwa wabunge, akiwataka kuzingatia Kanuni za Bunge.

  "Kwa kuwa nimeeleza hapa asubuhi, nawatoa watu watatu ambao nimewaona wana vurugu. Mheshimiwa Lissu, Lema na Mchungaji Msigwa naomba mtoke ndani, naomba askari wawasindikize hadi nje kabisa ya geti," alisema Ndugai.

  Akiahirisha kikao Bunge kwa ajili ya mapumziko ya mchana, Ndugai alisema alilazimika kuwatoa ndani wabunge hao kwa kuwa walishindwa kutii kanuni, ambazo muda mfupi uliopita alikuwa ameeleza zifuatwe. Ndugai alisema mbunge hapaswi kuzungumza bila idhini ya spika, naibu spika au mwenyekiti wa Bunge. Alisema sera za matumizi ya nguvu ili kufikia malengo ya kisiasa zinakatazwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo kila mwananchi anapaswa kuifuata.


  Naibu spika alimshangaa Mchungaji Msigwa kutokana na kuwa 'mshangiliaji' mkubwa wa tukio hilo, wakati alipaswa kuwa mtulivu ili kulinda hadhi ya uchungaji wake.

  "Mchungaji Msigwa alikuwa anapiga sana kofi, naomba mchungaji awe kidogo na staha," alisema.

  CHANZO:
  Tukio hilo lilianza baada ya Waziri Lukuvi kuomba kutoa taarifa na muongozo wa spika kuhusu hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, iliyosomwa na Lema.

  Katika hotuba hiyo, Lema alitoa shutuma na kashfa dhidi ya serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi ya idara zilizo chini ya wizara hiyo.

  Kutokana na hotuba hiyo, Lukuvi ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, aliomba kiti cha spika kitoe muongozo kuhusu maneno yaliyokuwa ndani ya hotuba ya Lema.

  Lukuvi akitumia kanuni ya 64 (1) a, b, f na g na ile ya 68 (7), alieleza jinsi serikali ilivyovumilia kusomwa kwa hotuba hiyo na taswira ya Bunge inavyogeuzwa kuwa mbaya kwa wananchi na baadhi ya wabunge.

  "Kwa maelezo ambayo nimetoa na kelele nyingi kutoka kwa Watanzania, leo tumeshuhudia kanuni nzima ya 64 imevunjwa, lakini (serikali) tumekuwa wavumilivu, tumetaka maneno yote yaliyotolewa (na Lema) yasikike," alisema Lukuvi na kuhoji:

  "Hivi ni kweli mbunge aliyechaguliwa na wananchi aseme Tanzania si nchi ya haki. Watawala wanatesa wananchi? Polisi leo wanahamasishwa wasikubali maagizo ya makamanda wao, hata wasilinde maandamano? lakini mwisho unaomba waongezewe mishahara."

  Lukuvu alisema Tanzania ni nchi ya amani tofauti na maelezo ya Lema.

  Aliwashangaa wabunge wanaogharamiwa kwa kodi za wananchi ili wawatetee bungeni kuzungumzia mambo ya uchochezi.

  Wakati waziri akiendelea kuzungumza, Lissu alisimama na kuwasha kipaza sauti na kuomba muongozo wa spika bila ya kuruhusiwa kufanya hivyo.

  Licha ya Ndugai kumkatalia na kumtaka akae, alisimama na kusisitiza apewe nafasi, huku akizungumza kupitia kipaza sauti.

  Kwa upande wake, Lema naye alisimama kutaka naibu spika amnyamazishe Waziri Lukuvi, kwa madai anachotoa si muongozo, bali anahutubia Bunge.

  Hatua ya wabunge hao iliibua zogo, hivyo kuondoa umakini kwa wabunge wengine waliokuwa wakifuatilia maelezo ya serikali yaliyokuwa yakitolewa na Waziri Lukuvi.

  Mchungaji Msigwa kwa upande wake aliomba muongozo na bila kuruhusiwa aliwasha kipaza sauti akidai naibu spika ana upendeleo.

  Wakati naibu spika akitoa ufafanuzi, aliwataka wabunge kupunguza hotuba au maneno yanayohamasisha chuki kwenye jamii.

  Alisema ilipaswa hotuba zote zinazotolewa bungeni zingekuwa zinawasilishwa mapema ofisini kwake ili ikiwezekana zipitiwe kabla ya kusomwa kwa kuwa zinafuatiliwa na wananchi.

  Ndugai aliwahakikisha kiti cha spika kitaendelea kutenda haki kwa kila mbunge, bila kujali chama chake cha siasa.

  Akichangia makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Anna Abdallah (Viti Maalumu -CCM), alisema kitendo cha kuomba haki bila wajibu ni fujo na kwamba, kila mtu anapaswa kutekeleza wajibu wake.

  "Hata uongozi unatoka kwa Mungu, hivi unatukana polisi na magereza na mwisho unatoa wito waongezwe mishahara nini maana yake. Nasema haki bila utaratibu ni batili," alisema mbunge huyo mkongwe.

  Anna alisema wananchi wanakerwa na baadhi ya mambo yanayofanywa na wabunge, na kutoa mfano kuwa, jana alisikiliza redio moja ambapo wananchi walionyesha kuwadharau kutokana na matendo yao.

  Wabunge walaani hotuba ya Lema

  BAADHI ya wabunge wamelaani hotuba ya kambi ya upinzani iliyosomwa jana na Lema, kwa madai kuwa ni ya uchochezi.

  Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba (CCM), alisema inashangaza kuona viongozi wa CHADEMA kuwa ndiyo chanzo cha vurugu bungeni.

  Komba alisema viongozi hawatakiwi kuwa watu wenye jazba, kwani kwa kufanya hivyo watashindwa kueleweka kwa wanachama wao.

  Alisema vurugu ndani ya Bunge haikuwepo katika awamu iliyopita, ambapo kambi ya upinzani iliongozwa na CUF, kwani busara ilitumika pale palipotokea kuhitilafiana.


  "Hawa wenzetu inashangaza, viongozi wenyewe ndio wanaoongoza vurugu, sasa sijui itakuaje," alisema.

  Mbunge wa Viti Maalumu, Diana Chilolo (CCM), alisema hotuba hiyo imejaa uchochezi na uvunjifu wa amani.

  Wananchi: Tumewachoka
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Uhuru jana, baadhi ya wananchi walisema waliwachagua wabunge ili wawawakilishe, lakini kinachoendelea sasa ni kero na aibu kwa jamii.

  Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema tabia ya wabunge kukaidi amri na taratibu hadi kutolewa nje, inatia kichefuchefu.

  Alisema wabunge wanapaswa kufahamu Bunge ni chombo cha wananchi na mhimili wa dola, na si jukwaa la wanasiasa, hivyo halitakiwi kuchezewa.

  Dk. Bana ameishauri Kamati ya Uongozi ya Bunge, kukaa na kutafakari mambo ya fedheha yanayoendelea na ichukue uamuzi.

  Alisema iwapo kiongozi anakaidi kufuata taratibu na kanuni zinazomwogoza, hawezi kushawishi wananchi kufuata sheria za nchi, na kwamba aina hiyo ya viongozi ni aibu kwa jamii.

  "Bunge si uwanja wa siasa, bali ni chombo na mhimili muhimu wa dola, hivyo kanuni na taratibu ni lazima zifuatwe.

  "Katika mabunge yote duniani, wabunge wanabishana kwa hoja, lakini hili la kwetu linatia aibu. Utovu wa nidhamu umetawala kiasi cha kutia kichefuchefu,Ó alisema.

  Dk. Bana alisema kitendo cha mbunge kukaidi amri na kutolewa nje na askari ni kero kwa jamii, na inaonyesha udhaifu wa wabunge kutofuata matakwa ya Bunge.
  Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Madinah Social Services Trust, Sheikh Ally Al-Mubarak, alisema Bunge limekuwa kichekesho.

  Alisema wabunge wanapaswa kuwa mfano bora kwa jamii, lakini Bunge limekuwa kinyume chake kwa baadhi ya wabunge kuonyesha utovu wa nidhamu na kudharau mamlaka ya spika.

  "Wapo wanaodhani kuongea sana bungeni au kuwa mkaidi ni kujijenga kisiasa na kupata umaarufu mbele ya jamii, hilo si kweli hata kidogo. Jambo la msingi unaongea nini kwa manufaa ya wananchi," alisema.

  Alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakililetea Bunge sifa mbaya kwa kujali maslahi binafsi na uroho wa madaraka kwa kivuli cha kutetea wananchi, wakati hawana uchungu nao.

  "Wanaongea sana kuonyesha wana uchungu na wananchi wakati tangu wamechaguliwa hawajachangia hata dawati, tumechoka," alisema.

  Mkazi wa Dar es Salaam, Adam Mkwepu, alisema vitendo vinavyoendelea bungeni kwa sasa vinaonyesha ni jinsi gani baadhi ya wabunge wamekosa uelewa juu ya kilichowapeleka bungeni.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  OH KWELI NA NI WASHINDI...

  KAMPUNI ya Uhuru Publications Limited (UPL), wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, imeshinda tuzo katika shindano la ubora katika mapato na ukuaji, lililoandaliwa na Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na Kampuni ya Ushauri na Ukaguzi (KPMG), ambalo lilianza Desemba mwaka jana na kuzishirikisha kampuni 200 za hapa nchini, ambapo 100 kati ya hizo zilishinda, huku UPL ikishika nafasi ya 70. Pichani, Mhariri Mtendaji wa UPL, Josiah Mufungo, akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwakilishi wa KPMG, Dk. Boniface Abayo, katika hafla iliyofanyika juzi usiku, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Muhasibu Mkuu wa UPL, Alvera Kabwogi.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  uhuru wa mafisadi huu.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  My foot ..
   
 5. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Ni gazeti ambalo hata kufungia maandazi sitaki.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wanasema limeshida sababu lina ongoza kwa kuwa na wasomaji wengi na kila mwaka wanaongezeka...
  Hapa inaonyesha eti Wanalisoma sababu ya Itikadi ya CCM

  Kwahiyo Wananchi Wamechoshwa na Wabunge Waliofukuzwa...!!!???
   
 7. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  To hell!!!!nikiliona nasikia kichefuchefu na kuumwa tumbo
   
 8. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimevumilia sana kumaliza kusoma hii habari tena kwa heshima ya kuwekwa humu jf...hili gazeti lakibaguzi mno, tena lakichochezi mno..tena sio gazeti huru kama ambavyo wanajiita bali ni gazeti lilofungwa kwa minyororo ya mafisadi..hivi waandishi wa hizi habari wanapata 10% ya kutetea upuuzi huu? Change must com now...
   
 9. n

  nchasi JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Gazeti gani la magamba. Umechagua watu wanatoa maoni kwanza umechakachua. Haiwezekani hata kidogo ukaleta upendeleo wa wazi kabisa bungeni. Naibu spika analinda sana maslahi ya chama chake waziwazi sasa kanogewa na kujisahau ndo maana watu tunahasira nae vibaya mno. Hilo ni bunge la Watz wote sio la jimbo lake.
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  ni gazeti la ccm,ulitegemea waisifie CDM,acha kulalamika,cdm wanatakiwa kuwa na gazeti lao..mpinzani wako hawezi kukusifia...
   
 11. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  HILO GAZETI LA UHURU Halinunuliki na linawakilisha chama chama cha magamba hicho sio chanzo kizuri cha habari
   
 12. j

  join9527 Member

  #12
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni gazeti ambalo hata kufungia maandazi sitaki.


  [​IMG][​IMG]
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
   
 13. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,878
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  hata kama kukosoa wanatakiwa wawe objective, nikimaanisha they should b based on the reality.
   
 14. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #14
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa tumechoka kasema nan hv hao waandish wazima haibu yao milele mp"s chadema msiwape nafasi mafisad bungen tupo pamoja gazet lkenyewe linaitwa uhuru wa nchi gan tz hachen unafki nyie waandishi
   
 15. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi huwa nalitumia kuchambia nikimaliza haja kubwa.
   
 16. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hivi kumbe bado mnalisomaga tu hilo gazeti!
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Kuna watu bado wananunua hili gazeti?
   
 18. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Halikuachii alama ya wino mata.t.ak.oni kweli? maana ni jeusi kama limepakwa mkaa
   
 19. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani gazeti la Uhuru bado lipo? Duh!
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Unajua watu wengine me sijui lakini kwa mawazo yao ila
  My Take:
  Hotuba ya Lema (Mbg) kama wao CCM wana sema ilikuwa na Uchochezi ningependa kuwauliza hao wabunge wa CCM matukio yote ya kupigwa rai risasi huko Tarime,Arusha,Pemba/Unguja wao wanona ni sawa tu serikali kufanya hivyo mbona wao wasiliongelee hilo kwanini wasiwe wakweli daima mbele za mungu??

  Hotuba ya Mb-Lema imekuwa hivyo kwani ni dhaili kuwa serikali imeshindwa kujipanga na kurekebisha makosa yake, serikali makini inge hakikisha haimpi mtu yeyote kulalama kuwa askari kaua na kwanini nasema hivyo kuwa serikali haipaswi kua na kama wangekuwa wanafuata sheria za haki za Binadamu hayoyote yasingelikuwepo leo sasa mtu akiyasema wabunge wa CCM wanasema uchochezi hawajakaa na kujiuliza huyo mb-Lema hotuba yake imetokana na nini kivipi ilikuwaje je hayo aliyo yasema alitakiwa awe kimya kama viongozi wengine wa CCM au kwenye ukweli acheni ukweli uwepo makosa ya serikali lazima yakemewe kwa nguvu zote ukitaka wananchi wako wakuelewe tenda HAKI na AMANI itakuja kiraini bila tatizo
   
Loading...