Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

Kubenea bado watanzania tutasimama na kuamini katika kile ulichokifunua kuhusu ushiriki wa staff wa TISS kwenye kuteka, kutesa na kumdhuru Dk Ulimboka.
Wakilifungulia tunakuomba Kubenea na waandishi wenzako wa Mwanahalisi kuendelea na moto huo huo wa kufichua umafia wa serikali hii ya watendaji wazembe wa serikali.
 
Kubenea anautafuta umaarufu wa nguvu kweli kweli kwa kutaja majina ya watu kuweka picha zao na kuzihusisha na matukio mabaya.,mungu amlaani mwezi huu mtukufu wa toba.
 
GAZETI lolote linatakiwa liripot facts, na sio kuwaaaminisha vitu ambavyo waandish wenyewe hawana uhakika navyo...kuweka, flani, namba ya kura ni ngapi, alizaliwa lini...sisi inatuhusu nn?? how do u directly connect him na tukio husika?? na kusema aliwasiliana na namba hii, na hii, na hii...so wat....we unawasiliana na watu wangapi kila siku?? gazeti limejaa upuuzi mtupu..mi nilivosoma toleo la mwisho, story ya kwanza, nikaona nisiendelee kwingine...yale yalikuwa maoni ya kubenea, na taarifa alizopata toka watumishi wa tigo, NEC na kwingineko, point ya msingi....unamuhusisha vp mtu na tukio tajwa??,,,bado watanzania wengi wasio na ufahamu wa kisheria, wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama walio wengi humu JF, mnasema, eti ameiweka serikali uchi...bora walifungie tu...tena lisifunguliwe leo wala kesho....na liwe fundisho kweli..limezd kuandika vitu visivyo na msingi..........
 
kinachotokea tanzania leo, napata picha ya tunakoelekea. Naliona jeshi la ukombozi ambalo nyinyiem mtaliita waasi likiongezeka, madaktaqi sina shaka wamejaa na walimu wanakuja..naomba ulimboka akija awe amiri jeshi mkuu, watu waingie msituni.
 
eti serikali inayojali demokrasia, inaua watu na kisha inajaribu kuficha ushahidi.
Kama ni kweli mwanahalisi wamekosea kwa nini wasiwashitaki mahakamani?
Sasa tumeingia vita mpya. Vita ya kufichua ukweli.
Tutaweka kwenye mitandao na ikibidi tutaweza vijarida vingi zaidi na watu watasoma.
Hivi mwanahalisi hawawezi kwenda mahakamani kupinga hili?


Nashauri Mwanahailisi na wapenda haki kwa ujumla wafungue kesi mahakamani kupinga uonevu huu wa serikali ya ccm kwa vyombo vya habari. Ninasubiri kwa hamu tamko la LHRC na Jukwaa la wahariri.

Hongera Kubenea kwa kutoogopa vitisho na kusimamia kweli.
 
kinachotokea tanzania leo, napata picha ya tunakoelekea. Naliona jeshi la ukombozi ambalo nyinyiem mtaliita waasi likiongezeka, madaktaqi sina shaka wamejaa na walimu wanakuja..naomba ulimboka akija awe amiri jeshi mkuu, watu waingie msituni.
 
aaaahhhhhh,hii serikali dhaifu sana,mbona hata sisimizi hajafa kisa gazeti la mwanahalisi.sijaiona hiyo amani iliyohatarishwa.
 
Waoga hao! Kwanza kulifungia ndio itazidisha uvumi kwamba serikali inahusika haswa. Pili kwani hata Ulimboka watanfunga mdomo akirudi?

Mkuu, Only in Tanzania!
Huyo Dr. Ulimboka naye kwa kuogopa kuwachonganisha wananchi na Serikali yao wanayoipenda sana anaweza kufungiwa asitembee na wala asizungumze na mtu yeyote hata wanawe.

Kama kifungu hicho hakipo katika katiba kitatungwa haraka sana bungeni, na wazee wa ndiyo watakipitisha kwa kura nyingi.
 
Safi sana gazeti la udaku na majungu na kufitinisha watu hata hivyo serikali imechelewa mno kulifungia.
i thnk ua not ok.. ni stress za maisha na roho mbaya na ufisadi si kosa lako njaa mbaya tetea magamba wenzako but siku si nyingi zinasabika.
 
Baada ya serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi leo kwa kile inachosema ni uchochezi na kwamba Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

SASA KATIKA KUIPITIA KATIBA KATIKA KIFUNGU HICHO KINASEMA:

The Freedom of Expression

18.- (1) Without prejudice to expression the laws of
of the land, every person has the right to freedom of expression, opinion and expression, and to seek, receive and impart or disseminate information and ideas through any media regardless of national frontiers, and also has the right of freedom from interference with his communications.

(2) Every citizen has the right to be informed at all times of various events in the country and m the world at large which are of importance to the lives and activities of the people and also of issues of importance to society:



MY OPINION:

Kubenea amejaribu kutumia haki yake hiyo, na kuhakikisha mwananchi mmojammoja anapata haki yake ya kupata habari inayohusu Taifa lake au matukio yanayojiri.


KATAZO KATIKA KATIBA:

Limitations

30.-(1) The human rights and freedoms, the principles of which are set out in this Constitution, shall not be exercised by a person in a manner that causes interference with or curtailment of the rights and freedoms of other persons or of the public interest
.

SWALI:

Hivi kujua kilichomtokea Dr. Ulimboka sio interest of the public? Vyombo vya serikali hapa hofu yao ni nini? kama sio kweli si habari au taarifa za kweli zitolewe kabla ya kulifungia gazeti? What is the public interest in this matter?

Naomba kuwasilisha.
 
Kulifungia mwanahalisi nijuhudi za kuficha uozo wa serikali hii. Lakini hii ni sawa na mbuni kuficha kichwa akiamini kaficha mwili. Hivi tuseme akili za watendaji wakuu serikalini ziko likizo au ndio upeo wao wa kufikiri? Hawajui wanaendesha gari kuelekea korongoni na hawataki kuonyeshwa hilo wanafunga watu midomo. Mwisho ni mbaya kwa taifa hili. Lazima Watanzania tukemee tabia hii chafu. Imefikia muda wa kuanza kutafuta namna ya kuwa na Taharir square yetu.
 
Kabla ya kuandika na kuitoa hiyo story gazetini alitakiwa awapigie hao wenye simu kwanza then apeleke ushahidi wake polisi ,alichofanya ni kwamba alikurupuka

hakukurupuka ka unavyohisi wewe. Kwanza, yampasa kupewa na pongezi kwa ujasiri wake wakutoa taarifa kwa umma, kuliko hivyo vyombo vya dola. Mifano tunayo mingi. Dr. Mwakyembe alishawapeleka ushahidi wake mara ngapi kuhusu kutishiwa maisha wakashindwa kuufanyia kazi nakuja na majibu ya "viini macho". Inasikitisha sana umepewa masikio huna uwezo wa kusikia, umepewa macho hunauwzo hata wa kuona. Jitahidi sana uhepukana na hili kundi la hawa watu wenye "uvivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau."
 
dah kweli serikali kwishne, yaani kumbe kweli wanahusika mimi nilijua labda pengine hao maaskari walifanya huo unyama kivyao kumbe nikutoka serikalini.

Bado kidogo na sisi wananchi tutawafungia, subiria kidogo tu.
 
Baada ya Mwanahalisi, JAMII FORUMS itafuata... CCM haitaki kabisa kuambiwa ukweli. Mkakaati wa kufungia Jamii Forums umeshaiva. Naomba kuwasilisha.
 
Serikali imefanya vizuri kufanya hivi. Waandishi na wahariri inabidi wajue mipaka ya kazi yao.
 
Janja yao ipo ukingoni,wanachokitumia sasa ni ubabe tu.WAMESAHAU DAUD ALIVYO MUANGUSHA GOLIATI.
 
Back
Top Bottom