Gazeti la amani leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la amani leo

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  FRONTAMANI.jpg [​IMG]


  Hayo mambo kazi kweli.................
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  mastaa.jpg [​IMG]

  [​IMG]Na Gladness Mallya
  KUTOKANA na kuzidi kwa wimbi la mastaa wa Kibongo kuugua na kulazwa mwaka 2012 katika hospitali mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, daktari aliyeomba hifadhi ya jina lake ameeleza sababu na kusema wapo hatarini kuzeeka mapema, Amani lina ripoti kamili.
  Gazeti hili lilizungumza na daktari huyo anayefanya kazi katika hospitali moja kubwa hapa nchini ambapo alisema sababu zinazowafanya mastaa wengi kukumbwa na magonjwa mbalimbali ni uzee, vyakula wanavyokula, kutofanya mazoezi na kutokuwa na mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara.
  “Unajua mastaa hawa wakishapata umaarufu, basi wanabweteka. Hawafanyi mazoezi, wanapenda vyakula vyenye mafuta mengi wakidhani wanakula
  vizuri kumbe wanajiharibu,” alisema dokta huyo.
  Mastaa wengi waliolazwa kwa mwaka 2012 walikuwa wakisumbuliwa zaidi na magonjwa kama presha, tumbo, kifua, malaria na mengine mengi ambapo hapa tunakuletea listi ya mastaa hao na magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua.

  WEMA SEPETU
  Hivi karibuni Wema alilazwa katika Hospitali ya Heamed iliyopo Upanga, Dar akisumbuliwa na tatizo la kubanwa kifua ambapo hali yake ilikuwa mbaya kiasi cha kuwafanya Watanzania wamuombee.

  NASIBU ABDUL ‘DIAMOND’
  Diamond aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar ambapo alikimbizwa kwenye Hospitali ya Heamed na kulazwa akisumbuliwa na homa kali na uchovu uliosababishwa na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.

  SAID NGAMBA ‘MZEE SMALL’
  Mkongwe huyo wa maigizo na filamu anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza ambapo alilazwa Muhimbili, Dar na baadaye aliruhusiwa lakini hadi sasa bado ni mgonjwa.

  COLETHA RAYMOND ‘KOLETA’
  Hivi karibuni mwigizaji huyo alilazwa kwenye Hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni, Dar akisumbuliwa na ugonjwa wa kidole tumbo ‘appendix’ ambapo alifanyiwa upasuaji na kupoteza fahamu kwa takribani saa saba.

  TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
  Wiki mbili zilizopita Amanda alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan, Dodoma kutokana na kusumbuliwa na presha kushuka.

  RUTH SUKA ‘MAINDA’
  Mwigizaji Mainda alilazwa kutokana na kusumbuliwa na presha ya kushuka ambapo alidondoka ‘lokesheni’, tatizo hilo likaendelea kumsumbua mara kwa mara.

  JUMA KILOWOKO ‘SAJUKI’
  Mwigizaji Sajuki alilazwa nchini India akisumbuliwa na uvimbe tumboni ambapo baada ya matibabu alirejea Bongo na mpaka sasa bado hajawa fiti vya kutosha.

  WASTARA JUMA
  Mwigizaji Wastara ambaye ni mke wa ndoa wa Sajuki naye alilazwa nchini India wakati alipokwenda na mumewe kwa ajili ya kumhudumia.

  HUSNA IDD ‘SAJENTI’
  Wiki iliyopita mwigizaji huyo alilazwa huko kwao, Kondoa-Irangi, Dodoma akisumbuliwa na homa ya mapafu.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  amanifront.jpg [​IMG]

  Haya tena kazi kweli.....................
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  amani.jpg MBUZI2.jpg MBUZI31.jpg [​IMG]
  [​IMG]


  [​IMG]Julius Mawimbi Kisena ‘Mawimbi’ akiwa na mbuzi wake wa ajabu.
  George Kayala na Haruni Sanchawa
  UKISTAAJABU ya Musa utaona ya Firauni. Mbuzi wa ajabu ajulikanaye kwa jina la ‘Mawimbi’ anafanya vitu ambavyo kwa akili za kibinadamu unaweza usiamini, Amani linamwanika mwanzo mwisho.
  Mbuzi huyo anayemilikiwa na Julius Mawimbi Kisena ‘Mawimbi’ mkazi wa Mazizini Ukonga, Dar karibu na Kituo cha Polisi Mazizini ameonekana kuwa kivutio kwa watu wa eneo hilo kutokana na kufanya vitendo vya kibinadamu.
  Mapaparazi wetu walimtembelea (Mawimbi) katikati ya wiki hii, nyumbani kwake hapo na kufanikiwa kuongea na ‘bosi’ wake huyo ambaye alikiri mbuzi huyo kuwa na maajabu kibao.

  ANAPENDA KULA ‘BATA’
  Kwa kawaida mbuzi hujulikana kwa kula majani, lakini ‘Mawimbi’ yeye anapenda kula ‘bata’, vyakula kama nyama choma, nyama iliyopikwa, maandazi, chapati kwa mchuzi, ubwabwa kwa nyama, ugali, chipsi kavu na mihogo ya kukaanga ndiyo mwake.
  Ili kudhihirisha hilo, Mawimbi aliwaagiza waandishi waliopiga hodi nyumbani kwake kwenda gengeni kununua chapati ili waamini kile anachokisema juu ya mbuzi huyo mwenye uzito wa kilo 128.
  “Ili muamini kweli mbuzi wangu anakula vyakula vya binadamu, nendeni mkanunue chapati mumletee, mtaona atakavyozifuta chapchapu,” aliagiza Mawimbi.
  Mapaparazi wetu walikwenda gengeni jirani na makazi ya mbuzi huyo na kununua chapati tano ambapo alipopelekewa, alizifuta kama binadamu anayefungua kinywa kwa chai.

  BIA KWA SANA
  Mawimbi aliongeza kuwa mnyama huyo anakata kilevi kama hana akili nzuri. Alisema amekuwa akinywa aina zote za bia na ana uwezo wa kunywa za baridi zaidi ya 18 kutokana na uhitaji wake kwa siku bila kupepesuka wala kuwa bwii.
  Je, Mawimbi anajuaje kama mbuzi wake ana kiu ya bia?
  “Mara nyingi akipata hamu ya bia huenda kwenye baa na kuzungukazunguka hapo mpaka atakapohudumiwa.
  “Kama akiwakuta watu wanakunywa huwasogelea na kuwaangalia kwa macho yenye uhitaji. Wanaomfahamu humnunulia na kumwekea kwenye chombo na kumpa. Wasipotekeleza hilo hufanya fujo kwa kupiga kichwa meza za wateja mpaka kuangusha vinywaji vyao,” alisema Mawimbi.

  LAKINI MBAKAJI!
  Kila kizuri kina kasoro, wakati mbuzi huyo analeta mshangao kutokana na tabia yake hiyo lakini kumbe ana tabia za kubaka wanawake, hasa wale walio kwenye siku zao.
  “Tatizo la mbuzi huyu ana tabia ya kubaka wanawake, hasa wale walioko kwenye siku zao,” alisema Mawimbi.
  Akaendelea: “Amini usiamini hadi sasa ana kesi 18 za kubaka katika Kituo cha Polisi cha Mazizini. Waathirika wakubwa ni wanawake hao ambao hupita karibu yake.
  “Yeye akishasikia harufu ya mwanamke tu huanza kumkimbiza kwa lengo la kupata mambo ya kiutu uzima.”

  AKIIBWA ANAKUWA MZITO KULIKO TEMBO!
  Hili nalo, Mawimbi analisimulia kama maajabu mengine ya mbuzi wake, kwamba alishawahi kuibwa mara 3 bila mafanikio kwani wezi hao walimrudisha wenyewe baada ya kuelemewa na uzito wake kama wa tembo. Anasema hata akiibwa kwa kuingizwa kwenye gari huwa mzito.
  “Wamejaribu kumuiba mara 3 bila mafanikio. Kuna watu kwa nyakati tofauti walifanikiwa kumuiba na kumuweka kwenye gari lakini walishindwa kuondoka naye kutokana na kuelemewa na uzito.
  Kutokana na hali hiyo, walimrejesha wenyewe na kuondoka zao. Kuna mwingine siku moja alikata bati kwenye banda na kutaka kuondoka naye lakini mbuzi alimpiga kwa pembe yule mwizi, asubuhi tukamkuta amepoteza fahamu, nikampa shilingi 2000 kwa ajili ya kwenda kujitibu maana aliumia vibaya,” alisema Mawimbi.

  AGONGWA NA PIKIPIKI, AVUNJIKA MGUU
  Wiki mbili zilizopita mbuzi huyo ambaye amekuwa gumzo pande hizo aligongwa na pikipiki na kuvunjika mguu wa kushoto mbele.
  Mawimbi anasema alimfuata daktari wa mifupa wa Hospitali ya Amana ambaye alimfunga bandeji ngumu ‘P.O.P’.
  “Kwa sasa mbuzi wangu hana raha, ana maumivu makali kwani hivi karibuni aligongwa na pikipiki, nikamwita daktari wa mifupa pale Amana, akaja akamtibu kwa kumfunga P.O.P, naamini Mungu atamsaidia kupona,” alisema.

  ANAWEZA KUWA MBUZI WA UCHAWI?
  Mawimbi anakanusha madai kwamba maajabu ya mbuzi huyo hayatokani na mambo ya kishirikina, bali ni uwezo alionao kutoka kwa Mungu.
  “Si mbuzi wa uchawi, ila ni mambo ya Mwenyezi Mungu tu,” aliweka wazi Mawimbi huku akiagana na waandishi.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  amuua.jpg [​IMG]
  [​IMG]
  IGP Said Mwema.
  Na Mwandishi Wetu, Simiyu
  AMA kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Msemo huu unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mkazi mmoja wa Kijiji cha Nghoboko wilayani Meatu mkoani hapa, Stephano Mihilu mwenye miaka 60, kudaiwa kumfumania mkewe wa ndoa akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa.
  Taarifa za kipolisi zilizotua kwenye dawati la Amani zinadai kuwa tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa Julai 22, mwaka huu ambapo baada Stephano kulishuhudia tukio hilo, aliwaua mama na mwanaye kwa kuwacharanga mapanga bila huruma.
  “Jamaa aliporudi nyumbani, aliingia ndani na kukutana na tukio ambalo hakuwahi kulifikiria, alimkuta mkewe akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa, nadhani akili ilihama, akachukua panga na kuwacharanga wote mpaka walipokata roho,” alisema afande mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwani si msemaji wa jeshi la polisi.

  HUYU HAPA KAMANDA WA POLISI WA SIMIYU
  Akilizungumzia tukio hilo la kusikitisha na kushangaza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Afande Salum Msangi aliwataja waliouawa kuwa ni Kundi Sita mwenye umri wa miaka 40, ambaye alikuwa mkewe na Boyani Stephano mwenye miaka 27 ambaye ni mtoto wao wa kumzaa.
  Alidai kuwa, Mihilu alimkuta mkewe akifanya tendo la ndoa na mtoto wake wa kumzaa ndipo alipopandwa na hasira kisha kuwashambulia kwa kuwakata mapanga na baadaye kuwachinja.
  Kamanda Salum alisema, baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alikwenda mwenyewe kujisalimisha kwenye kituo cha polisi ambapo alikabidhi silaha alizotumia katika mauaji hayo ambazo ni panga na fimbo.
  “Mihilu alitembea kuanzia saa 7 usiku hadi asubuhi kwenda katika Kituo cha Polisi cha Mwahuzi wilayani Meatu kwa lengo la kujisalimisha akidai kuwa hakutaka kuwasumbua wanausalama hao kwani yeye ndiye mhusika wa mauaji hayo,” alisema kamanda huyo.

  WANANCHI WANALIZUNGUMZIAJE TUKIO HILO?
  Wakizungumza na mwandishi wetu baada ya tukio hilo, baadhi ya wananchi wameonesha kushangazwa nalo huku wakieleza kuwa, kama ni kweli basi dunia inaelekea mwisho.
  “Hivi inawezekanaje mama kufanya tendo la ndoa na mwanaye wa kumzaa? Au kuna mazingira ya ushirikina?” alihoji Juma Sagala wa Meatu.
  Naye Mama Josephine, mkazi wa kijiji ambacho tukio hilo lilitokea alisema: “Hili tukio lina utata lakini kwa kuwa limeshafika kwenye vyombo vya dola, ukweli utajulikana na sheria itachukua mkondo wake ila limetushangaza sana.”
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  ifahari aina ya Toyota Land Cruiser Prado alilonunua kwa shilingi milioni sabini na tano.
  [​IMG]Gari la zamani la Diamond aina ya Toyota Opa.
  3.jpg DIAMOND3.jpg View attachment 63168 IMG_1790.JPG IMG_1796.JPG
  Na Shakoor Jongo

  STAA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amezidi kudhihirisha jeuri ya fedha baada ya hivi karibuni kununua gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser Prado kwa shilingi Milioni sabini na tano (75,000,000) Amani lina ushahidi.
  Staa huyo alinaswa hivi karibuni na mapaparazi wetu akiliegesha gari hilo nje ya mgahawa maarufu katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  GARI LAANZA KUZUA GUMZO
  Akiwa ndani ya mgahawa huo, baadhi ya mashabiki wake walizua mjadala kama gari hilo ni lake huku wengine wakisema gari analomiliki msanii huyo ni Toyota Opa lenye thamani ya shilingi milioni saba (7,000,000) kwa kuagizia nje ya nchi.
  Hata hivyo, wadau hao walishindwa kumuuuliza msanii huyo kama yeye ndiye mmiliki halali wa gari hilo lenye namba za ‘chesisi’ RZJ 1200017972.

  DIAMOND ANASWA LAIVU
  Juni 19, mwaka huu staa huyo alinaswa na paparazi wetu maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaam akishuka kutoka kwenye ‘ndinga’ hiyo na ndipo alipobanwa kufunguka kuhusu gari hilo jipya.
  Diamond: “Kwa kweli ngoma (gari) ni yangu. Nilinunua hili nikiamini linaweza kunisaidia kwenye ruti zangu.”
  Amani: Umelinunua shilingi ngapi?”
  Diamond: “Shilingi milioni sabini na tano pamoja na mambo yote ya ushuru.”

  ANATAKA NAMBA ZA KISASA
  Aidha, msanii huyo ambaye kwa sasa amepaa kwa kupata mafanikio kupitia shoo zake, alisema amechelewa kuweka namba za usajili kwa sababu anataka kubandika namba binafsi ambazo zitakuwa na jina la DIAMOND.
  Alisema namba hizo ambazo serikali iliruhusu hivi karibuni, zitamgharimu shilingi za Kitanzania milioni tano (5,000,000).

  UTAJIRI TAYARI
  Mbali na kununua gari hilo, pia Diamond anamiliki gari aina ya Opa, anajenga nyumba mbili za kisasa na kuna ushahidi kuwa anaingiza kuanzia shilingi milioni 16 kwa wiki kupitia shoo zake.
  Kwa mahesabu ya kawaida, kama staa huyo anaingiza kiasi hicho cha fedha kwa wiki, ni dhahiri anatumbukiza shilingi 2,285,714,28 kwa kila siku.
  Kwa maana hiyo, Diamond anaingiza shilingi 95,238.095 kila dakika sitini au kwa kila saa moja.
  Kipato hicho ni shoo tu, mbali na hizo msanii huyo ana tenda za makampuni mbalimbali ambapo hufanya matangazo na kuingiza kipato cha nguvu.
  Diamond anaweza kuwa msanii wa kwanza wa kiume katika Bongo Fleva Tanzania (kama kuna mwingine ajitokeze na vielelezo) kumiliki gari la kifahari.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  fuamnizi6.jpg fumanizi.jpg fumanizi2.jpg fumanizi4.jpg fumanizi1.jpg AMRIYA6.jpg
  [​IMG]

  Na Mwandishi Wetu


  KITIMTIMU cha aina yake kilitokea katika gesti maarufu iliyopo Mbuyuni Kunduchi-Mtongani jijini Dar es Salam kufuatia njemba mmoja kudakwa akiwa na mke wa mtu wakiigaragaza amri ya sita ya Mungu, Amani lina ishu mkononi.

  Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio, ishu hiyo ilijiri hivi karibuni mishale ya saa 3:30 usiku katika gesti hiyo.
  Shuhuda akasema mfumaniaji ambaye ni mwenye mke (jina tunalo) alifanikisha kuwanasa wawili hao baada ya kuwafuatilia kwa muda mrefu toka aliposikia penzi lake linasalitiwa.

  Ikadaiwa kuwa siku ya tukio, mume alianza kuingiwa na shaka saa 1:00 usiku baada ya mkewe kuonekana yuko kwenye harakati za kujiandaa kwa ajili ya mtoko ambao hakuwa na taarifa nao na alipomuuliza alisema anakwenda kumjulia hali mtoto wa rafiki yake aliyekuwa anaumwa.

  Ndipo mume huyo machale yakamcheza, akajipanga kwa kumpigia simu dereva wa ‘bodaboda’ na kumpa kazi ya kumfuatilia mkewe kila atakapotia mguu kisha amtaarifu kwa simu.

  Shuhuda akasema: “Baada ya mke kujikwatua vilivyo, akatoka nje bila kufahamu kinachoendelea, akakodi pikipiki ileile ambayo ilikuwa ikimsubiri atoke halafu imfuatilie na hivyo kurahisisha kazi ya dereva.

  “Alipoondoka tu, mumewe akachukua pikipiki nyingine na kumpitia mpigapicha ili apate ushahidi kwa kile ambacho atakishuhudia.
  “Bahati nzuri nyingine, mbele mwanaume alikutana na askari wa doria na kuwaeleza dukuduku lake, ndipo nao wakaamua kumsaidia kwa ajili ya usalama zaidi,” alisema shuhuda huyo.

  Kwa upande wake, mume naye alisema baada ya mkewe kuondoka, dereva wa pikipiki alimjulisha kuwa mkewe alimfikisha Mbuyuni, lakini alichukuliwa na jamaa mmoja kwenye gari wakaelekea maeneo ilipo gesti hiyo.

  Alisema: “Baadaye dereva huyo wa bodaboda aliniambia kuwa mke wangu na huyo jamaa wamezama ndani ya gesti hiyo ambayo haikuwa mbali sana na maeneo hayo ya Mbuyuni, tena wapo chumba namba sita. Da! Inauma sana.”

  Akasema ndipo yeye na ‘manjagu’ wakazama hapo kisha kugonga chumba hicho na kumkuta mkewe akiwa amejifunga shuka la gesti hiyo na jamaa akiwa anajiandaa kuvua nguo, tayari kwa ‘kubanjuka’.

  Hata hivyo, shauri hilo liliishia hapohapo baada ya jamaa kujitetea kuwa hakujua kama mwanamke huyo ni mke wa mtu kwani hata mwanamke naye hakumtaarifu kwamba ameolewa.

  Mpaka gazeti hili linakatiza mitamboni, haikujulikana ni hatua gani mume huyo alikwenda kuzichukua kwa mkewe baada ya kubaini kuwa alimficha ukweli.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  dar.jpg ​[​IMG]
  FUKWEZABAGAMOYO.jpg ​[​IMG]  MANGOGARDEN.jpg ​[​IMG]


  ...Hawa Mango Garden.
  [​IMG]...Hawa wakiwa Mlimani City.

  Na Erick Evarist
  JIJI la Dar es Salaam na viunga vyake hasa maeneo ya maegesho ya magari (parking), viwanja vya wazi na ufukweni, linatisha kwa vitendo vya ngono za rejareja vikiongozwa na watu maarufu, Amani limefanya uchunguzi wake na hii ndiyo ripoti kamili.
  Kwa nyakati tofauti, hivi karibuni, gazeti hili lilinasa matukio yenye kutia kinyaa yakifanywa waziwazi na wakati mwingine mchana kweupe.
  Katika maeneo tofauti, kamera yetu iliwanasa mabinti wadogo ‘wakidendeka’ hadharani bila kujali umati uliowazunguka.

  MAENEO HATARINI
  Maeneo yanayotajwa kukithiri kwa uchafu huo jijini Dar ni pamoja kwenye mikusanyiko ya wazi kama Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Makaburini, Buguruni, Ufukwe wa Coco na kwenye ‘parking’ mbalimbali za kumbi za starehe.

  NDANI YA LEADERS
  Mabinti waliotambuliwa kwa jina mojamoja, Husna na Vai walinaswa kwenye Viwanja vya Leaders Club wakifanya matendo machafu ya kisagaji.

  MLIMANI CITY
  Jumapili moja, Amani likiwa ‘rovingi’ liliwamulika ‘masistaduu’ ambao walitajwa kwa jina mojamoja, Jack na Teddy kwenye ‘parking’ za Mlimani City ambao wanadaiwa kuwa miongoni mwa kundi la wadada wanaoligeuza Jiji la Dar kuwa kama Sodoma na Gomora kwa kujihusisha na vitendo vichafu vya ngono.

  COCO BEACH
  Pia ‘patroo’ yetu ilimtia kibindoni mwigizaji wa muvi za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ‘akidendeka’ na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni ‘kuku mtamu’ kwenye Ufukwe wa Coco.

  MANGO GARDEN
  Kwenye Ukumbi wa Mango Garden, demu aliyetajwa kwa jina moja la Jack naye aliingia mtegoni baada ya kunaswa akiwalegezea zipu wanaume bila kujali macho ya kadamnasi.

  FUKWE ZA BAGAMOYO
  Mbali na maeneo hayo, pia fukwe nyingi zinazoanzia Dar hadi Bagamoyo nazo zilifumuliwa na ‘shushushu’ wetu aliyeshudia uchafu wa ajabu wa ngono rejareja zikihusisha dada zetu na watasha.

  WAZAZI
  Dawati la Amani linatumia fursa hii kuwataka wazazi kuwatupia macho watoto wao hasa mabinti kwani hali ni mbaya na watachuma majanga muda si mrefu.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  mzeesmall1.jpg
  [​IMG]  Said Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa hospitali.


  [​IMG]
  Mzee Small.

  Gladness Mallya na Erick Evarist


  NYOTA wa vichekesho kwa muda mrefu Bongo, Said Ngamba ‘Mzee Small’, Mei 21, mwaka huu alikata kauli ghafla muda mchache baada ya kuwasili nyumbani kwake Tabata Kimanga, Dar akitokea Mwanza kwenye ziara ya kikazi.
  Kwa mujibu wa mdogo wa gwiji huyo, Karim Said Ngamba, Mei 20, mwaka huu kaka yake huyo alimpigia simu kumtaarifu kuwa amerejea Dar lakini kiafya hakujisikia vizuri.


  MDOGO WAKE ASIMULIA
  “Kwa kuwa ilikuwa usiku nilishindwa kwenda lakini kesho yake nikawahi. Nilimkuta kama mtu aliyechanganyikiwa, midomo yake ikapinda, akawa hawezi kuongea.

  “Mkono wake mmoja ulikuwa ukishindwa kufanya kazi sawasawa kama mkono mwingine, hali hiyo ilitupa wasiwasi.


  ALIVYOSEMA DAKTARI
  Mdogo wake huyo akaendelea kusema: “Ikabidi tumkimbize Hospitali ya Amana ambapo daktari mmoja baada ya kusikia maelezo yetu na jinsi mgonjwa alivyo, alisema ana dalili zote za kiharusi ‘stroke’ hivyo akalazwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alisema Karim.


  MWANZA ALIFUATA NINI?
  Safari ya Mzee Small jijini Mwanza akiwa ameambatana na mkongwe mwenzake, Bi. Chau ilikuwa kwa ajili ya kufanya kampeni maalumu ya watu wenye ulemavu wa ngozi iliyofanyika katika Chuo cha Bungando jijini humo.


  NENO LA MHARIRI
  Ni kipindi kingine ambacho Watanzania kwa umoja wetu tunatakiwa kumwomba Mungu ili amrejeshee afya Mzee Small ambaye ana mchango mkubwa katika jamii
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Bongo inatishaaaaaaaaaaaaaaaaaa......pole mzee smollo
   
Loading...