Gawio tarajiwa kwa wanahisa wa NMB

Gawio tarajiwa kwa wanahisa wa NMB

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,196
Nichukue nafasi hii kuwapongeza Wakurugenzi wa Bodi ya NMB wakiongozwa na CEO wao Mama R. Zaipuna. Jana kwenye taarifa ya habari kupitia luninga ya ITV ilitangazwa kuwa gawio la mwaka huu 2024 kila HISA moja mwanahisa atapata Tshs.361.14.

Hongereni sana na hii haijapata kutokea katika historia ya NMB. Ninawaomba pia jirani zenu sitaki kuwataja pia waige mfano wenu kutokana na gawio lao kuwa kidogo kila mwaka ukilinganisha na faida wanayopata kwa mwaka.

Kumbe Mashirika yanayoongozwa na Wamama wanafanya kazi nzuri kuliko mashirika yanayoongozwa na Wababa. Hongera sana CEO wa NMB.
 
Back
Top Bottom