Gas ni ya watanzania si mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gas ni ya watanzania si mtwara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kupe, Jan 4, 2013.

 1. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2013
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,024
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo wana mtwara msituletee ukabila na ukanda . je na dar nao wakisema bandari ni ya dar itakuwaje. kama hujaridhika ruksa kuhamia mkoa wowote uupendao
   
 2. Kankwale

  Kankwale Senior Member

  #2
  Jan 4, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usidanganyike Mtwara na Lindi kwanza Tanzania baadaye.
   
 3. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2013
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Unaelewa ni kwa nini wanataka KWANZA hiyo gas ibaka Mtwara?? Sometimes ficha upumbavu wako...
   
 4. N

  Nyanijike Member

  #4
  Jan 4, 2013
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akili yako itakuwa imekeketwa na magamba ya CCM.
   
 5. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2013
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,095
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mkuu, mbona gari unadandia kwa mbele? Fatilia madai yao kwanza usiwe kama aliyepanda treni ya mwanza akitegemea ashushwe kamata.
   
 6. m

  matengele Member

  #6
  Jan 4, 2013
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani jamaa hajaelewa madai ya wana mtwara.ebana nakushauri ufatilie vizur madai ya hao wana mtwara ndipo utajua uje na thread gani ya maana ambayo kila mmoja atakuelewa!
   
 7. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2013
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,451
  Likes Received: 620
  Trophy Points: 280
  Orodhesha madai yao alafu ndio upinge hoja

  Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
   
 8. c

  chief72 JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2013
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 564
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hujui kinachoendelea, pliz kaombewe maana hata magazeti husomi pole
   
 9. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2013
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,863
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  kwa nini usiseme gesi ni ya mataifa yote?
   
 10. spartacus

  spartacus JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2013
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Unadandia treni kwa mbele....hata uelewi unaongelea nini....
   
 11. O

  OMARY2012 Senior Member

  #11
  Jan 4, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Unafiki kama huu ndio unatuweka pabaya watanzania. Lakini kumbuka historia ina tabia ya kujirudia. Katika ili la gesi viongozi msikurupuke kisiasa kuwajibu wananchi wa mtwara. Utawala bora ni ustawi wa wananchi wote bila kujali maeneo waliyopo. Msituletee ya nigeria hapa.
   
 12. Kamanda Kazi

  Kamanda Kazi JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2013
  Joined: Dec 15, 2012
  Messages: 2,616
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  nadhani hamjamuelewa mtoa topic! sio kwamba anapinga madai ya wana Mtwara na Lindi. yeye anakataa kusema gasi ni ya wana Mtwara na Lindi jambo ambalo hata mimi namuunga mkono. hebu fikirini kama kila mkoa ukiandamana kudai raslimali zilizoko katika mikoa husika ni mali ya Wana mikoa hiyo tutaishi katika mazingira gani?!! raslimali zote ragardless ziko mikoa ipi ni mali ya watanzania wote. jambo la maana ni kwamba tupiganie wananchi wa mikoa husika wanufaike na raslimali zilizoko katika mikoa yao kwa maana kwamba maendeleo yaonekane na sio blaa blaa!

  pili serikali haipasi kutumia kauli za ubabe. isikilize madai ya wananchi. tumekuwa na raslimali lukuki lakini bado tumebaki kuwa maskini. mali zetu zinabebwa na wazungu na hao hao wazungu wanatucheka na kututukana kwa majina mabaya. fikiria Buhemba dhahabu imebebwa tumeachiwa mahandaki. wenyeji wamebaki maskini. Geita na Nyamongo dhahabu inabebwa wananchi wanabaki kutamani mabaki ya mawe baada ya kutoa dhahabu (magwangala). wnavamia migodi wachukue mabaki then wanaambulia kupigwa risasi! mwanza minofu ya sangala inabebwa kwa midege kupelekea wazungu...wakazi wa kanda ya ziwa wanabaki wanawania mapanki. mzungu mmoja kwa kutukejeli akatengeneza sinema ya mapanki, serikali ikamjia juu but mesage sent and delivered! ni mambo ya kusikitisha sana[SIZE=4]. kesho nitatoa thread ya jinsi mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi ilivyo [SIZE=4]ya kinyonyaji[SIZE=4]!!!![/SIZE][/SIZE][/SIZE]
   
 13. h

  hope1985 JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2013
  Joined: Jan 2, 2013
  Messages: 778
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Nyie endeleeni tu,kumbe watu wa mtwara si watanzania? Au kumbe rasilimali yoyote nchi hii isipopelekwa dsm basi inakuwa si kwaajili ya watanzania? Hakika watu wamechoka kilichobaki mnaandaa mazngra ya uwepo wa waasi tz we ngoja tu we are so tired.
   
 14. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2013
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,574
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Mnapenda uasi ee! haya kaasi, ila angalia msitegemee gastu kwamba ni suluhisho la kuwatoa kwenye umasikini mkaacha shughuli nyingine. Maana nasikia mmeacha kujishughulisha mnasubilia gas hasa vijana.
   
 15. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2013
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,605
  Likes Received: 5,509
  Trophy Points: 280
  vyenu mumekula na wazungu vyetu tule wote!. Mumeshindwa kulinda mali zenu mkitegemea zetu?, mtegemea cha nduguye hufa heri maskini. mia
   
 16. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2013
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 3,710
  Likes Received: 1,267
  Trophy Points: 280
  Liwalo na liwe..ikiwaka mulika,ikizima papasa!
   
 17. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2013
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,471
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Naona mnaanza kufanikiwa kuwagawa watz.
   
 18. R

  Ryabagosi New Member

  #18
  Jan 5, 2013
  Joined: Jan 5, 2013
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa ndg yangu,rasrimali zote ni za watanzania wote na tunayo haki ya kuzitumia,ingekuwa hivyo kama wanavyohitaji wana Mtwara,basi kila mkoa hapa TZ ungelitumia rasrimali zinazopatikana mahali husika.Nina wasiwasi kama walioandamana kweli ni wana Mtwara,maana nchi yetu sasa hivi raia wake wamechanganyikana,yupo wa kutoka Musoma ,Kigoma,Kanyigo nk nk.Tafadhali tuwe makini na hizi tunazoiita siasa za ubaguzi.
   
 19. Anthonio

  Anthonio JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2013
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [Unaelewa ni kwa nini wanataka KWANZA hiyo gas ibaka Mtwara?? Sometimes ficha upumbavu wako...]
  NAUNGA HOJA MKONO!!!!!
   
 20. O

  OMARY2012 Senior Member

  #20
  Jan 5, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanamtwara wanatambua hilo na ndiyo maana walikubali yafuatayo:
  Kuichagua ccm miaka yote pamoja na kung'olewa reli huko, kuhamishwa baadhi ya miundombinu kupelekwa maeneo mengine ya tanzania.
  Mikoa ya kusini kuwahifadhi wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa afrika na kuzua wasiwasi kwa serikari ya wakati ule kuwekeza mikoa hiyo.
  Bandari yenye kina cha asili kudharauliwa.
  Wakati umefika rasimali za nchi zinufaishe wananchi wote na si waliopo dar. Tu, ndiyo maana jiji hilo kutokana uhamiaji wa wananchi kutoka mikoani kuendelea kwa kasi kubwa serikali imeshindwa kuwa na miundombinu kukabili hali hiyo. Wakati umefika viwanda vingi vijengwe mikoani waliko watanzania wengi. Haiwezekani watanzania wote tujekuishi dar.
   
Loading...