GARI LA POLISI

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
532
Difenda si gari la polisi!

Tuache masihara difenda ni gari la FFU na Magereza.

Zamani tulikuwa na vigari vya polisi. Vitetresaiklin vile vilikuwa na rangi mbili. Siku hizi sijui viko wapi.

Kama Tanzania ina magari ya polisi mimi siyaoni. Jiji kama Dar lilitakiwa liwe angalau na magari thelathini ya polisi kwa kila wilaya.

Polisi wana nyodo ndani ya magari ya polisi. Mara misele, mara honi mara ving'ora.

Asikuongopee mtu kuwepo magari ya polisi mjini tu kunapunguza uhalifu asilimia hamsini.

Tukio likitokea Ilala ndani ya dakika sifuri polisi wa mji mzima wanajua na wanaelekeza nguvu haraka kwenye tukio. Jambazi atakimbilia wapi, panyarodi atathubutu? Kabla mwizi hajachomwa moto gari la polisi limefika na kumuweka mwizi kiti cha nyuma ambacho kina madirisha ya jela tayari.

Nashangaa hii nchi wabunge wamegombea kupewa migari ya nguvu wawafikie wananchi wao lakini nchi haina gari za polisi za kutosha. Ingekuwa mali wabunge wakapanda mabasi ili wayajue machungu ya wananchi wao.

Na huko bungeni hoja za shilawadu zinajadiliwa kila siku bila ya kupangwa kwenye ajenda lakini pembejeo za polisi hazijadiliwi.

Majukumu ya polisi hayaeleweki. Polisi anaweza kumlaza mtu central kwa kosa la parking. Wakati alitakiwa atumie kimashine tu kutoa tiketi ya adhabu ya malipo bila hata ya kuzungumza na mkosaji.

Yote tisa kumi ni pale unapopata tatizo halafu inabidi uende kituo cha polisi. Polisi anaitwa jamani na anakuja haraka mno. Ila kama anakuja kwa miguu hana gari hiyo ishu. Yaani ukivamiwa usiku mpaka ukienda kuchukua RB jambazi bado atakuwepo?

Ni ya kuyaangalia haya si ya kuyapuuzia kama kweli tunataka mabadiliko

.
56f79994e8e9cfd776e548f969e2244d.jpg
 
Kwa Tanzania unataka kuongeza vituo vya TRA. Angalia hawa tigo siyo wengi sana ila wanavyokula rushwa hadi raha. Sasa ongeza hayo magari 30 kila moja lina Polisi8 mbona tutakoma.
Mshkaji kasema mengi. Utendaji, majukumu n.k... Hasa majukumu, yakijulikana hayo sio kila sehemu itakuwa ya rushwa!
 
Back
Top Bottom