Gari la manispaa lakamatwa na meno ya tembo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la manispaa lakamatwa na meno ya tembo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by COMPLICATOR2011, Jul 21, 2011.

 1. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  ASKARI wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wilayani Mpanda Mkoa wa Rukwa, wanalishikilia gari la Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya kulikamata likiwa na meno matatu ya tembo yenye uzito wa kilo tisa.

  Dereva wa gari hilo alilitelekeza na kutokomea kusikojulikana.

  Thamani ya nyara hizo za Serikali haikuweza kupatikana mara moja. Gari hilo aina ya Land Cruiser namba DFP 4383 mali ya Manispaa ya Ujiji mkoani Kigoma, lilikamatwa juzi saa 5:46 asubuhi katika Mtaa wa Kotazi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, askari wa Hifadhi walimkamata mtuhumiwa, Elias Chambati (25) mkazi wa Mkoa wa Kigoma akiwa ndani ya gari hiyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na tukio hilo akishirikiana na dereva wa gari hilo.

  Chanzo hicho kinadai kuwa Chambati alikamatwa kutokana na taarifa walizokuwa nazo askari wa Katavi na uchunguzi walioufanya wa kumfuatilia nyendo zake za kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.

  Kutokana na taarifa hiyo, walimfuatilia siku hiyo ya tukio kuanzia kwenye nyumba ya kulala wageni aliyokuwa amefikia, Family chumba namba sita iliyopo katika Mtaa wa Mjimwema mjini Mpanda ambako walimfuatilia hadi walipomkamata akiwa ndani ya gari hilo.

  Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Chambati alikamatwa akiwa ndani ya gari hiyo na askari hao wa Hifadhi ya Katavi ambapo dereva wa gari hilo alifanikiwa kukimbia na kutokomea kusikojulikana.

  Inadaiwa kuwa baada ya dereva kukimbia, askari wa hifadhi walifanya upekuzi katika gari ambapo walikuta meno matatu ya tembo yenye uzito wa kilo tisa ambayo thamani yake haijajulikana yakiwa yamefichwa chini ya viti vya gari hilo.

  Baada ya kumkamata, askari hao wa Hifadhi ya Katavi, walifanya mawasiliano na uongozi wa Manispaa ya Ujiji Kigoma ili kupata msaada wa kumtambua dereva ambaye Chambati alikataa kumtaja.

  Uongozi huo wa Manispaa ya Ujiji Kigoma ulimtaja dereva huyo kuwa ni Masoud Yassin ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

  Alisema gari hilo lililotelekezwa limechukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika Ofisi ya Hifadhi ya Katavi, na Polisi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi wanamsaka dereva aliyekimbia.
   
 2. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hehe uandishi mwingine
   
 3. T

  Triple DDD Senior Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maisha magumu maliasili lazima ziishe, ili kujazia mishahara na ukali wa maisha.

  Hapa kila mtu atatafsiri kula kwa aina yake, Kina Rostam hawatangazwi na mkapa na wengineo
  ila hawa ndg wanaojisaidia ili waishi watatangazwa ile mbaya kila kona.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kesi hii itaenda haraka mno lakinin ile ya KIA na twiga unaweza kusikia mashitaka hayajakaa vyema hivyo wameachiwa jamani Tanzania ni ya ajabusana .Tutege masikio .
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wakuu nataka kujua bei ya kila jino la tembo. Mpaka mwaka uishe wengi washakuwa vibogoyo.
   
 6. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Wanayapima kwa kg
   
 7. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Nadhani wamedhulumiana...
   
Loading...