Gari la ACT Wazalendo, laua mtoto mdogo Tabora

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,338
Katika hali ya kushangaza na kushitua gari la ACT wazalendo lilikuwa kasi na kugonga mama, na kusababisa kifo cha mtoto Tabora.

RIP Mtoto wetu.

GARI LA ACT LAUA, KUJERUHI

FRIDAY, APRIL 17 2015, 0 : 0

GARI la matangazo mali ya Chama cha ACT Wazalendo lenye namba T 811 BPQ aina ya Toyota Land Cruiser, limemgonga na kumuua mtoto mwenye umri wa miezi 10, kumjeruhi mama yake ambaye anaendelea na matibabu Hospitali ya mkoa Kitete.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Suzan Kaganda, alimtaja mtoto aliyekufa kuwa ni Ramadhan Juma, mkazi wa kijiji cha Magiri, Wilaya ya Uyui, mkoani humo.

Alisema ajali hiyo ilitokea jana saa tatu asubuhi wakati mama wa mtoto huyo akitokea hospitali ambapo baada ya kuteremka kwenye Kituo cha Mabasi Magiri ndipo akagongwa na gari hiyo kupinduka wakati akijaribu kumkwepa mama huyo.

Kamanda Kaganda alisema, dereva wa gari hilo, Mabona Kabwe, anashikiliwa na jeshi hilo na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Wakizungumza na Majira, mashuhuda walisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari hilo ambapo mama
wa marehemu, Shukuru Ibrahim (17), amelazwa katika wodi namba sita ikielezwa hajitambui kwani hawezi kuzungumza na amepata majeraha kichwani na mguu wa kushoto.

Katika hatua nyingine, Kiongozi wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe,amesema amechoka kunyanyaswa, kubaguliwa, kuzushiwa mambo mbalimbali ndio maana aliamua kuondoka katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Tarafani (Nyerere), Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora jana, Bw. Kabwe alisema lengo la kuanzishwa chama hicho ni kufyeka msitu, kuijenga nchi na uchumi imara kwa Watanzania wote ambao wengi wao ni maskini

"Nimechoka kunyanyapaliwa, kunyanyaswa kubaguliwa na kuzushiwa mambo mbalimbali ndio maana niliamua kuondoka
CHADEMA na kuhamia ACT ili niwe huru," alisema.

Akiwazungumzia wakulima wa tumbaku wa wilayani humo, alisema sh. bilioni 28 zimeliwa na viongozi wa Chama cha Ushirika Mkoa ambao hawajafikishwa mahakamani.

"Viongozi wa vyama vya ushirika wa wakulima wa tumbaku hapa Tabora wametafuna sh. bilioni 28, walipaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani lakini hadi leo wameachwa tu, tunamtaka Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu wachukue hatua," alisema.

Alisema Rais Kikwete alifuatilia suala hilo na kutoa tamko lakini hadi leo hakuna kilichofanyika zaidi ya viongozi hao
kuonekana mtaani bila wasiwasi wowote.

"Naomba wananchi mtuunge mkono kwani chama chetu hakitakubali kuona wakulima wa tumbaku wanaibiwa fedha zao na wahusika wakiachwa bila kuchukuliwa hatua.

Kabla ya mkutano huo, mamia ya wakazi wa Mji huo walijipanga barabarani ili kumpokea Bw. Kabwe ambapo mapokezi hayo yalifanyika saa sita mchana ambapo shughuli nyingi zilisimama kwa muda.

Katika ziara anayoifanya mkoani humo, Bw. Kabwe ameongozana na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Taifa, Bi. Anna Mghwira na mwanamuziki mkongwe nchini Seleman Msindi (Afande Sele), wakitokea
mkoani Singida.

Mkoa wa Tabora ni wa sita kutembelewa na viongozi wa ACT tangu chama hicho kianze ziara zake Aprili 9, mwaka huu ambapo leo watakuwa mkoani Shinyanga.


Source Gazeti la Majira

GARI LA ACT LAUA, KUJERUHI
 
Gari la matangazo la chama cha Zitto la gonga na kuua mtoto wa miezi kumi huku likimuacha mama yake akiwa na majeraha.

Source: Magazeti leo
 
Washirikina hao .....Hiki chama imeasisiwa kuzimu,toka ianzishwe vifo visivyoeleweka vimekuwa vingi sana
 
Hiki chama kina mkono wa shetani... toka ianzishwe vifo visivyoeleweka vimekuwa vingi sanaa
 
Yeah...! Kama gari la chama fulani likipata ajali hata watu hawajajua chanzo wanaingiza siasa na ushirikina?

chanzo ni mwendo kasi, sehem ya makazi....haya wapuuzi wao au wewe??!!
 
Kuna member humu alisema tangu ACT kizinduliwe mzimu wa ajali umeliandama taifa akauliza kwa nini kila wanakofanya mkutano kunatokea ajali? akaenda mbali na kuihusisha ACT na kafara ya damu sikumwelewa sasa naanza kumwelewa.

Walipokuwa Iringa mtoto aligongwa na gari akafa walipofika Morogoro zaidi ya watu 10 waliungua moto ndani ya basi, juzi wakati wakiwa Singida basi la Jordan lilipata ajali na kuua, jana ACT wenyewe wamemwaga damu ya kichanga. Masikini leo wanaelekea Shinyanga sijui watakufa wangapi tena.

Hiki chama kinamizimu ya usaliti badala ya kuwa ACT- Wazalendo mwisho kitaitwa ACT- Damu.

RIP kichanga.
 
Back
Top Bottom