Gari BMW X3 tatizo lishalekebishwa lakini Taa inaendelea kuwaka

Wakuu na wajuzi wa mambo ya magari naombeni msaada, jana wakati naendesha Gari (BMW X3) ghafla Alarm ikalia mara moja tu kucheki Dashboard nikaona Tire Pressure Light imewaka, nikajua tatizo ni upepo, kweli nikapita Mahali kwa pressure kucheki Tyre moja ya nyuma ilikuwa na misumari miwili

Basi nikazibiwa pancha, jamaa akanijazia upepo akacheki na tyres zingine kwa mara ya pili zote zilikuwa sawa lakini nilivyowasha gari Ile Taa pale kwa dashboard haijaondoka, yule jamaa aliyenizibia pancha akanambia Hadi nitembee kidogo ndio ikaondoka

Nimeendesha gari umbali wa zaidi ya kilometers 50 lakini Taa Bado inawaka!

Wenye Experience na hizi BMW hii Taa kuwaka ni kwamba itazima yenyewe? au inaondolewaje maana tatizo kwenye mataili hakuna tenaView attachment 2440310
Unatakiwa kuifanyia resetting.

Unapokumbana na changamoto uwe unaingia YouTube changamoto nyingi utazitatua mwenyewe bila kumtegemea fundi na hata zingine unakwenda kwa fundi unamuelekeza nini cha kufanya iwapo kama fundi siyo mzuri ila jitahidi kwenda kwa mafundi wazuri

Eg.
 
Wakuu BM imeniletea kipengele kingine, hiyo taa inaashiria Nini, nazungumzia Taa iliyopo pembeni ya alama ya milango
IMG_20221220_154740_341.jpg
 
Hiyo taa huwaka kwa sababu kuu mbili tu.

1. Incorrect tyre pressure. Whether imezidi au imepungua.

2. TPMS sensor mbovu, wabongo wengi wakiziba pancha hizi hawazirudishii na hapo ndio majanga yanaanza.

Hizi sensor jamani hazinaga wires hivyo mawasiliano baina ya hiyo TPMS sensor na gari huwa ni wireless.
Hiyo sensor inakaa sehem gani ya tyre naomba kujua mkuu
 
Unamiliki BMW x3 kwanini tyre iwe tatizo? Tena zinapaswa kubadilishwa kwa km sio kuangalia kashata.
Hii ni kweli kabisa tatizo tunamiliki bm alaf mfuko mkavu. Kuna mwamba petrol station nilikua naweka mafuta kwenye ka tvs kangu full tank kipindi kile ilikua 25100 bas mwamba kaja na washkaj zake yuko na jeep cherokee muundo wa zaman kidogo kaweka wese la 5k mpka nikacheka jamaa wa petrol station anasema ndo kawaida yake anazunguka mchana anaweka tena na jioni anaweka tena muda mwingine anakopa kaacha hadi earpods pale kisa wese
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
asilimia kubwa ya gari humu barabarani zina warning kwenye dashboard.. kama za ulaya ndio usisemee , ila tunaishi nazo tuuu

Bongo ni kawaida saaana sana

Unless ni oil au temperature…hapo lazima upark

Nakumbuka nlishawahi kuwakiwa na taa ya temperature kene mataa morroco ..asee nlitamani kupaa nkapaki gari pembeni..taa nazo haziruhusu alafu nipo mbele nyuma daladala kama zote .nkiwaza kuzima gari nawaza zile horn ntapigiwa+maaskari wa pale mataa

Asee baadae nlivumilia km dkk 7hivi nkachomoka kwenda kupaki pale TOTAL kuchek engine imechemk inatoa mvuke rejeta inavuja coolant imemwagika.
 
ilikuwa hatari sana hiyoo.. cheza na vyote hivyo ila Temperature sio ya kucheza nayo, hasa ile unaona inapandaa tuu.. kijasho lazi a kikutoke maana unaweza kaanga mambo live .. na alarm ya oil nayo ya kukaa nayo mvali, ila zingine zinavumilaka tuuu hata mwaka mzima 😆😆😆
 
H
Wakuu na wajuzi wa mambo ya magari naombeni msaada, jana wakati naendesha Gari (BMW X3) ghafla Alarm ikalia mara moja tu kucheki Dashboard nikaona Tire Pressure Light imewaka, nikajua tatizo ni upepo, kweli nikapita Mahali kwa pressure kucheki Tyre moja ya nyuma ilikuwa na misumari miwili

Basi nikazibiwa pancha, jamaa akanijazia upepo akacheki na tyres zingine kwa mara ya pili zote zilikuwa sawa lakini nilivyowasha gari Ile Taa pale kwa dashboard haijaondoka, yule jamaa aliyenizibia pancha akanambia Hadi nitembee kidogo ndio ikaondoka

Nimeendesha gari umbali wa zaidi ya kilometers 50 lakini Taa Bado inawaka!

Wenye Experience na hizi BMW hii Taa kuwaka ni kwamba itazima yenyewe? au inaondolewaje maana tatizo kwenye mataili hakuna tenaView attachment 2440310
Iyo inatakiwa ifanyiwe reset na diagnosis machine
 
Auffenberg Dealer Group

How to Reset Tire Pressure Light​

Hand Filling Tire with Air

TPMS Light On? What it Means and What You Need to Do​

When you see that low tire pressure light come on while driving around Shiloh, your first thought is probably “What does that even mean?” The purpose of the tire pressure light is to alert you to a problem with your tires. The service tire pressure monitoring system (TPMS) is an important safety feature of your car, truck, or SUV, so you should always make sure that it is activated and operating properly. The first thing you need to do if your TPMS light is on is to check the tire pressure and inflate them to the manufacturer’s recommended tire pressure.
Auffenberg Dealer Group is here to help you troubleshoot and get that light turned back off (and help you with service if there’s a more serious problem).
FIND A SERVICE CENTER NEAR YOU CONTACT US

Don’t Ignore Your Tire Pressure Light​

As far as dashboard warning lights go, the TPMS is one of the least severe — but it should never be ignored when you see the tire sensors indicating an issue. If one or more of your tires are underinflated, it can:
  • Reduce fuel economy
  • Lead to unpredictable vehicle handling
  • Decrease tire lifespan through uneven wear and tear
  • Impact your safety on the road (underinflated tires experience damage to the sidewall that can lead to blowouts)

Refill Your Tires to Reset Your TPMS Light​

The first thing you need to do when your TPMS light turns on is to check your tire pressure. Low air pressure is the most common reason for the TPMS light to come on. Next, you’ll want to refill your tires to the proper pressure to reset the TPMS light. Warning: do not overinflate your tires — always fill them to the manufacturer’s recommended tire pressure.
If your tire pressure light stays on even after you’ve added the correct amount of air to the tires, you’ll need to reset it. You can follow these steps to reset the TPMS light, or you can bring the vehicle into one of your local Auffenberg Dealer Group service centers, and one of our expert auto techs look at the service tire monitor system and take care of the problem for you.
If your TPMS light remains on after inflating the tires to the proper pressure, try these steps:
  • Drive the car at 50 mph for about 10 minutes. This should reset the tire sensors, and the next time you start the car the TPMS light should be off.
  • When the vehicle is off, turn the key towards “on” but don’t start your car. Hold the TPMS reset button until the tire pressure light blinks three times, then release it.
  • Start the car and let it run for 20 minutes, which allows the sensors to reset. You’ll find the tire pressure monitor reset button located beneath the steering wheel. Check your vehicle’s user’s manual if you’re having trouble locating it.
 
Back
Top Bottom