Garatwa: Tangu nijiunge na CHADEMA sijawahi kuona Upendo mkubwa wa TBC kama huu wanaomwonesha Mwenyekiti wetu Mbowe sasa, Je huyu Mbowe ni huyu huyu?

Patriot missile

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2024
Posts
286
Reaction score
424
MAMBO MATANO YA KUTAFAKARI BAADA YA MBOWE KUNG'ANG'ANIA UENYEKITI WA CHADEMA.

Na; Garatwa Francis

Awali ya yote niwapongeze sana wapenda mabadiliko wote mliopo ndani na hata nje ya nchi yetu hususani ninyi wenzetu wa Diaspora kwa kazi kubwa mnayoifanya usiku na mchana kuhakikisha Mbowe anapisha kwenye uongozi wa chama hiki na anasogezwa mbele jemedari wa vita Tundu Lissu ambaye ni mtu pekee ambaye CCM ya Samia inamhofia sana endapo akishinda uchaguzi huu na kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

Aidha, niwape pole kwa mfadhaiko wa nafsi mlioupata jana kutokana na yale maelezo ya kejeli, dharau na majivuno aliyokuwa akiyatoa Mbowe jana pale nyumbani kwake chini ya usimamizi wa kada mtiifu wa CCM Deo Balile aliyekuwa anaongoza taratibu za mkutano wake. Ikumbukwe Deo Balile ni sehemu ya mifumo yenu; ambaye amejifunika koti la uhariri kuutimiza wajibu wake wa nyuma ya pazia.

1. SUALA LA MARIDHIANO

Hatutaki kusikia mambo mengi yenye technicalities za kutuzubaisha kisiasa kwenye suala hili. Sisi tunasema, licha ya kwamba jambo hilo la maridhiano lilitoa mwanga na mafanikio ya kiwango fulani kwenye chama kama nilivyoeleza juzi wakati najibu ule upotoshaji wa Yericko Nyerere; ni dhahiri kama chama tulipata hasara kubwa zaidi ikiwemo kupoteza vipaumbele vyetu vyote vya msingi ambavyo ni Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, Mabadiliko ya Sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi hususani kwenye masuala ya chaguzi za kiserikali n.k

Baada ya kupima kwa kina zaidi, tumegundua wazi kwamba, suala hili la maridhiano linatumiwa na Mbowe kama kivuli ama kinga ya kufanikisha mambo yake binafsi badala ya taasisi iliyobariki suala hili kufanyika. Ni kwa bahati mbaya sana, wakati Chama kupitia mifumo yake ya uongozi kinakubaliana na jambo hili, haikuwa rahisi kujua dhamira ya Mbowe iliyokuwa nyuma ya pazia. Dhamira halisi ya Mbowe imekuja kujulikana ilivyo yenye nia ovu baada ya mienendo ya Mbowe isiyo na uhusiano wenye malengo ya CHAMA kuwa na dhamira ya dhati ya kuing'oa CCM madarakani kama ilivyokuwa huko nyuma kabla Mbowe hajaanza kukutana na Mama yenu humo Ikulu ndani wakiwa peke yao.

Hivyo basi, kwa sababu Mbowe amefikia mahali ambako tayari mifumo ya dola kupitia kwa Mama yenu imeshamfunga mdomo na hata ule uwezo wake wa mwanzo wa spirit ya mapambano; tumeamua tumpate Tundu Lissu ambaye CCM na hata dola ya CCM wanahofia uwezo wake wa mapambano ya kuipigania haki na spirit ya juu sana ya kudai mabadiliko. Lissu hana hulka za kujipendekeza. Lissu ni mtu amenyooka straight kwenye mambo yasiyo na tija huwezi kumkuta huko hata kama utamtisha kumuondoa uhai wake.

Hii CHADEMA inayoporwa uchaguzi wote wa Serikali za Mitaa nchi nzima na M/Kiti wa Chama analegea kama mlenda inahitaji mabadiliko makubwa sana ya mifumo ya uongozi kuanzia kwenye nafasi ya M/Kiti wa Chama ngazi ya Taifa ambaye atakuwa mbadala wa Mbowe ili hizo hekima ama busara za Mbowe zisikilizwe kama CCM wanavyosikiliza hekima na busara za akina Mzee Butiku na Jaji Waryoba.

Chama chetu (CHADEMA) kimefika hatua ambayo wapiganaji wengi walishashtukia mchezo na wakaamua kukata tamaa ya kujitoa kwa sababu wengi hawaoni ahueni huko mbele tuendako zaidi ya upigaji wa fedha za dola ya CCM unaowapa manufaa watu wachache wenye maguvu ndani ya Chama. Tazama huyo Wenje ambaye anaungwa mkono na Mbowe anachokieleza hadharani mbele ya vyombo vya habari kuhusu mambo ya akina Abdul mtoto wa M/Kiti wa CCM Taifa. It's very shame enough!

Halafu huyu Wenje naye ni M/Kiti wa Kanda na Mgombea wa nafasi ya Makamu M/Kiti CHADEMA Taifa kwenye huu Uchaguzi na anaungwa mkono na Mbowe tangu kwenye Uchaguzi wa Kanda uliogubikwa na matumizi makubwa ya fedha chafu alizokuwa anaeleza Tundu Lissu kila kuitwapo leo. Wenje hakuwa na uwezo wa kumshinda John Pambalu pale Mwanza; najua Pambalu ana mengi kifuani kwake huenda siku moja atatema nyongo ili awe huru kwenye nafsi yake.

2. MAELEZO YA AFISA WA IDARA YA IT CHADEMA MAKAO MAKUU

Kuna kitu watu walio wengi mnakisahau na badala yake mnazubaishwa na maneno ya janja janja za kisiasa ambayo yana uwezo wa kukuzubaisha usijue hata la kufanya wala usijue kutofautisha jema na baya. Pengine mnasahau kwa maksudi ama kwa kutotilia maamani anachokisema huyu Afisa wa Idara ya Information Technology - Makao Makuu ya Chama.

Huyu Afisa wa IT Makao Makuu Bw. Remigius Selestine mpaka sasa ameeleza mambo (5) matano kati ya (10) kumi ambayo wao kama watendaji wa Makao Makuu ambayo ndio Injini ya Chama wameyabaini kwamba ni vikwazo ambavyo wanaamini kwamba; pasipo kuubadili mfumo wa uongozi kuanzia nafasi ya M/Kiti wa Chama Taifa mpaka Sekretarieti ya Chama iliyopo sasa, hakuna chochote kipya chama kinaweza kufanikiwa kwa hali ilipofika sasa.

Huyu Afisa anaeleza jinsi wanavyogawana fedha za ruzuku ya chama kwa baraka za wakubwa wa chama huko maofisini, lakini ni wangapi tunaelewa hayo? Afisa anaeleza namna chama kilivyopoteza uwezo wa kubuni miradi mipya inayoweza kuwa vyanzo vya mapato ya chama na badala yake chama kinajiendesha kwa kutegemea ufadhiri wa Mbowe uliopelekea amejaa kiburi na majivuno ya kuita wengine wabangaizaji yeye mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa. Very shame!

3. RUZUKU YA CHAMA KILA MWEZI

Hili suala la Ruzuku ya chama linafichwa sana kwenye koti la (CAG) Mkaguzi wa Hesabu za Serikali. Yes! Licha ya kwamba mimi sio mtaalam wa masuala ya mambo ya mahesabu ya fedha, lakini nimesoma kidogo Course inayohusu mambo ya Accounts hapa University ili kunipa mwanga kama Mwanasheria huko mbeleni nijue jinsi ya kuwahudumia wateja wangu nikifanikiwa kuwa Wakili.

Lakini pia, nimekuwa M/Kiti wa Serikali ya Kijiji na baadae tena nikawa M/Kiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo Kupitia fursa hizi, ninao mwanga wa masuala ya mahesabu ya fedha na mbele yangu huwezi kutumia koti ama kwapa la CAG kutaka kuficha matumizi yasiyo na baraka za wanufaika wote ndani ya taasisi halafu ukaja kutwambia kwamba CAG ametoa hati safi sijui miaka 20 mfululizo. Kwangu mimi patachimbika kama sio kutoana meno bila ganzi.

Enzi za Dr. Wilbroad Slaa ukiachilia mbali madhaifu yake mengine kama ya kwetu sisi Binadamu wengine, ni dhahiri kile kiwango kidogo sana tulichokuwa tunapata kama chama wakati ule, matumizi yake yalikuwa yana uwazi (transparency) usiotiliwa shaka na mtu yeyote yule.

Chini ya CHADEMA hii ya Mbowe na Mnyika, specific kwenye suala la matumizi ya Ruzuku, sisi hatukuhoji habari za CAG kutoa hati safi ama chafu. Sisi tunahoji ni kwa nini matumizi ya fedha za Ruzuku ya chama yanakuwa ni yale tu yenye baraka za wakubwa kujilipa posho na per diem za vikao na semina lakini hata Elfu 10 tu ya kununulia karatasi za Katibu wa Chama wa Wilaya ama Mkoa hatuoni?

Mnaposema CAG anatoa hati safi kila mwaka ni sahihi kwa sababu, CAG yeye anachotaka ni kuona kama taratibu za kutumia fedha zilifuatwa na matumizi ya fedha hizo.aone nyaraka zake husika. Shida ilipo ni kwamba, hizo fedha sio za kujilipa posho za vikao na semina; badala yake ni fedha za ujenzi wa chama, kwa nini kila mwaka CAG aambiwe kujenga Chama ni kulipa posho za vikao na safari za wakubwa kwenye chama.

Tumeamua kumtanguliza Tundu Lissu kwenye Uenyekiti wa Chama ili angalau mwaka ujao 2025 CAG akija kwenye ukaguzi pale Makao Makuu ya Chadema mwezi Julai 2025 aambiwe na Watendaji wa Chama kwamba, mwaka huu tumepeleka kila Wilaya ya nchi hii Shilingi (100,000/=) Laki moja kwa ajili ya kuchangia pango la ofisi za chama ama kulipia umeme na maji ama kwa ajili ya makatibu wetu wa chama kununulia karatasi ama kulipia huduma zingine za stationery.

4. WAPIGANAJI WAMEKATA TAMAA NA KURUDI NYUMA KWA SABABU YA MIENENDO YA MBOWE

Ni ukweli wazi kwamba, ile spirit ya mapambano iliyokuwepo kwa wapiganaji wengi wa CHADEMA huku chini imeshuka kwa kiwango kikubwa sana na imefikia hatua sasa, unaweza kuona ni kwa kiwango gani mbowe anapingwa na umma wa watanzania wakionyesha dhahiri ni mtu asiye na future tena ya kuipeleka popote CHADEMA hasa wanapopima na kutazama kwa kina zaidi kuhusu mahusiano yake ya siri sana na mkuu wa nchi ambaye pia ndiye M/Kiti wa Chama kinachoongoza dola CCM.

Watu tulio wengi hivi sasa tunamuona Mbowe kama mtu hatari kwa wapinzani wenzake kwa sababu ya mahusiano yake ya siri aliyonayo na watu wa mifumo ya dola kupitia kivuli cha maridhiano hasa mahusiano yake na mkuu wa nchi. Tulio wengi tunamuona Mbowe kama mpinzani aliyeamua ku-compromise mbele ya dola ya CCM huku bado akijiita kiongozi wa chama cha upinzani.

Mbowe tunamtazama sasa kama mpinzani aliye na uhakika wa usalama wake pengine kuliko sisi wengine wote maana yuko pamoja na mifumo ya dola na kwa hicho la tatu ukitazama vizuri unagundua Mbowe anapata ushirikiano wa mifumo kwa kiwango cha kutosha.

Tazama hata jana kwa mara ya kwanza tangu mimi Garatwa nizaliwe, naona TBC inaonyesha 'Live Coverage' tukio la Mkutano wa Kiongozi wa upinzani tena Kiongozi wa CHADEMA mwanzo mpaka mwisho. What!? Acheni tufe na Lissu wallah liwalo na liwe. Lissu alipo sisi tupo. Akishinda tutashinda wote; akikosa tutakosa wote maisha mengine yanaendelea.

5. MBOWE KUKATALIWA NA WENGI NI DALILI TOSHA YA UAMINIFU WAKE NDANI YA CHADEMA KUTILIWA SHAKA

Yes! Imeandikwa Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Katika huu umri wangu wa miongo mitatu sasa, sijawahi kuona Mbowe akipingwa na umma wote hadharani kwa kiwango hiki cha sasa. Hii ni dalili tosha kwamba, Mbowe hakubaliki na wengi, haaminiki mbele ya walio wengi na hana tena Legitimacy ya walio wengi bali hivi sasa anaweza kuishi ndani ya chama kwa mgongo wa dola kwa sababu ni dhahiri CCM na dola yao wanatamani kuona Mbowe akiendelea kuwepo kwenye uongozi wa CHADEMA ili agano lao la Mama kutopata shida kwenye uchaguzi ujao wa 2025 litimie.

Hiki kilichotokea jana sio bure nawaambieni. Jiulizeni huyu ndiye yule Mbowe ambaye kila uchaguzi amekuwa akisema alikuwa hataki kugombea ila watu wamemuomba!? Kutoka hatua ya watu kumuomba yaani kugombea shingo upande (sizitaki mbichi hizi) mpaka kung'ang'ania nafasi baada ya kupata mpinzani wa maana sana? Kumbe zile habari kwamba watu wameniomba ilikuwa ni bosheni tu yaani zingua bwege, sio?

Sisi ambao tupo kwenye vita hii tangu Julai mwaka jana 2023 tulijua dhamira ya Mbowe mapema sana ya kutotaka kukiachia chama na tukaanza kuwa attention kumuondoa kidemokrasia na sasa tupo tayari kumuondoa Mbowe kidemokrasia hapa Mlimani City Dar es Salaam na dunia itashaangaa nawaambieni. Mbowe mwenyewe anajua hali halisi ya nguvu ya Tundu Lissu kwenye uchaguzi huu isipokuwa hawezi kuwaambia ukweli walioko nyuma yake.

Kila mmoja wetu kwa nafasi yake ashiriki awezavyo kuwaonyesha wajumbe wa mkutano mkuu ukweli kuhusu upotoshaji mwingi unaofanywa na genge la watu kadhaa ambao wanakikamua chama hiki na kupiga pesa za CCM kupitia mgongo wa Chadema huku wengine tukiumia kwa kujitolea kwa gharama zetu za mifukoni huku tukiupoteza muda wetu mwingi sana tukiipigania Chadema.

Asanteni sana na Mwenyezi Mungu awabariki sana.

Garatwa Francis,
Dar es Salaam, Tanzania.
22 Desemba, 2024.
 
Lissu akirushwa live na TBC, kupatwa kwa upendo.
 
 
Wewe na upungufu wako wa akili unaamini kinachofanywa na TBC ni genuine..
Hiyo ruzuku unayoongelea ndio ya kulipia pango ofisi za wilaya? Maana ya chama na wajibu wa wanachama ni nini? Vitu gani vinakupa ujumbe kwamba chama mahali fulani kipo hai au kimekufa km makao makuu inalipia pango la ofisi, ofisi inaweza kuwa hata nyumbani kwa mtu kwa yeye kujitolea shughuli za chama zifanyike..Suzan Lyimo katoa nyumba yake iwe ofisi ya wilaya kinondoni, huko sehem zingine wanachama wanaishi mitini na lazima makao makuu wawalipie pango?
Unajua nyinyi akili zenu sijui hata zinaweza kufikiri kitu gani..mna-raise vitu vidogo vyenye majibu lkn sabab akili ina ulemavu mnataka kila kitu uandikiwe..watu wa aina hii ni mzigo hata kwa familia zenu wenyewe.
 
Kila mmoja wetu kwa nafasi yake ashiriki awezavyo kuwaonyesha wajumbe wa mkutano mkuu ukweli kuhusu upotoshaji mwingi unaofanywa na genge la watu kadhaa ambao wanakikamua chama hiki na kupiga pesa za CCM kupitia mgongo wa Chadema huku wengine tukiumia kwa kujitolea kwa gharama zetu za mifukoni huku tukiupoteza muda wetu mwingi sana tukiipigania Chadema
 
Ko hii picha ina uhusiano gani na mada?
 
Siku zote vyama vya upinzani vimekuwa vikililia vipewe haki sawa ya coverage katika vyombo vya habari vya umma ambavyo vinaendeshwa kwa ,kodi xetu sote, sasa kama TBC wameamua kuonyesha mkutano wa Mbowe ulitaka Mbowe akatae?

Pili CAG ndiye mwenye dhamana ta ukaguzi wa mahesabu ya fedha , ulivyo mbumbumbu unakosoa hata hilo hakafu unadai wewe ni mwanasheria! Mwanasheria ambaye haoni umuhimu wa kufuata sheria, miongozo na ,kanuni zilizowekwa ili kuendesha nasuala ya fedha za umma very shame.

Mkutano mkuu utaendeshwa kwa,mujibu wa agenda sio kwa mujibu wa matakwa yako
The best option kwa nyinyi nyumbu wa Lissu ni kuanzisha chama chenu au kuhamia vyama vingine ( ingawa itakuwa vigumu kupokelewa maana hamtaki kufuata taratibu, miongozo na sheria).

.Eti CCM inamuogopa Lissu!, imuogope mtu mwenye mashabiki mtandao ambao mwisho wao ni kwenye key board? Huyo Maria na nyinyi wengine Lissu akiitisha maandamano mnnaweza kuja katika maandamano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…