Game yetu....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Game yetu....!

Discussion in 'Entertainment' started by jouneGwalu, Aug 18, 2011.

 1. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni muda sasa, toka music yetu ianze kuchukuliwa kwa umakini na hata kuundiwa harakati..
  Ni vizuri, napongeza!
  Ningependa kuchukua fursa hii kukumbushia kidogo harkati za hii game ya music (hasa hiphop)...
  Miaka ya 90's hasa 94, mvumo ulisikika.....
  TMK, kulikuwa kuna washikadau GWM.... hawa watu haijalishi kwa sasa wanapwaya kiasi gani bado wana nafasi kubwa katika kumbukumbu...
  Bado kwa kutokea TMK kuna jmbe limepotea midomoni mwa watu..... Chief Ramson aka Zavara...
  Wakijitandaza vilivyo kwenye game na wana wa KWANZA UNIT.... Heshima za kwanza marazote ni muhimu kwenda kwa Bonny Love!
  Japo alifanya sampling kwenye beat zake ila halikuonekana la muhimu sababu vocal na message katika pini ndio kilikuwa kikubwa......
  Sugu ataendelea kuwa Sugu kwani aliweka alama ya kwanza katika game kwa kuwa EMCEE (sipendi kutumia jina msanii) wa kufanya "press conference" hapo mwaka 1995...
  Mengi yalitokea, na wengi walirap japo kwa wakati ule lakini, KWANZA UNIT walibaki kuwa ndio vinara katika uwasilishaji wa kile wengi tunachokiita "real hiphop".
  Mwaka 1997 ikiwa bado imedhihirika kwamba unaposema hiphop ya hapa home unazungumzia KWANZ UNIT... kuna kitu kilibadili historia...
  Hata hapo pamoja na uwepo wa washikaji toka Diplomat,
  Talent show zilikuwa zikiendelea kama kawa maenea mbali mbali japo hichi ktu kimekosa uendelebu kwa sasa, lakini Talent show babkubwa ilikuwa ile ya "Gogo hotel" (kipindi hicho).....
  Kilichotokea siku hiyo ni tukio la KWANZA UNIT kukubali kushindwa na kumpisha kiti "HASHIMU DOGO".
  Ndio, hapo ndio kuonekana kwa mtu ambaye tuliyemtambua kama "Bongo Psychology" aka Hashimu Dogo...
  Hii ilikuwa ni halali hata Stevie B (wa clouds fm) kipindi hicho yupo na wenzake wa "Undergound souls" walikubali.....
  Na huu ndio ulikuwa mwanzo wa historia "Kikosi cha Mizinga" (tutacheki next time)
  Track rasmi ambazo amepata kufanya Hashimu ni pamoja na "Tunasonga" na "Behind the shadow"...
  Pata wasaa wa kusikiliza pini hizo mbili japo najua ni ngumu sana kupatikana rediono kwa sasa (nao ni mjadala mwingine)
  Ni ukweli usiopingika kuwa bado mpaka sasa hapajatokea EMCEE wa kushika na kuziba nafasi ya Hashimu Dogo hata kuondoka kwake KIKOSINI hapo mwaka 2006 dio miongoni mwa sababu za msingi za kudorora kwa kikosi cha mizinga!
  Mlolongo wa matukio katika GAME yetu ni mrefu lakini japo kwa wasaa huu tu.....
  Tutaendelea..!
  Hii ni strictly kwa wapenzi wa hiphop kwa ujumla........ USIZINGUE.....
   
 2. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  GWALU''kuna mwana wa kikosi anajiita gwalu...ok nimekusoma japo mi nimeanza kisikiliza hihop ya kibongo 96 hivi, watu kama dogo hashimu, diplomats mamcees wa kwanza unit, mpaka kumjua sugu there after niga jay na watu wake,walume ndago na hiphop katuni up to know..ila real hihop niliisikia kwa kwanza unit, kikosi na nyimbo yao tunasonga, sugu na nyimbo zake kama vile polisi..wengine walikuwa wanafanya hiphop katuni/rap katuni haina ujumbe hiyo, kwakweli watu wa hiphop hasa kwa sasa wachache sana wengi mamluki na wapo kimaslahi,,na ndio maana mtu kama pina, sugu hawababaiki kama wanauza au hawauzi kwasababu wanajua maana ya hiphop, na angalia sana mamluki wengi wanawapinga watu wa kikosi, sugu kwa sababu wametekwa na wenye soko...lkn wachache tuliobaki tutazidi kuwakilisha hata kama kwa battle.
   
 3. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  "The infamous"
  Pia umenikumbusha kuna wana wa mbele walikuwa wanajiita "infamous mob" jamaa walikuwa balaa, nadhani walikuwa wanawakilisha East, kuna mixed tape waliitoa "The mugs"..... Ilikuwa inaitwa "soul assasin I n' II" ah humo Infamous mob wana pini yao humo inaitwa "industrial shake down" (kama sijakosea)... Icheki.... Ila nadhani unaipata!
  Nafurahi tupo pamoja, lengo ni tuweke kumbukumbu sawa katika music yetu!
  Yah kweli kikosini amepata kuwepo "Gwalu" ila sina mahusiano nae kabisa!
  Umezungumzia 96 mzazi.....
  Dah kweli kwa kipindi hcho watu waliojuwa na walikuwa wanazungumza sense kwenye ngoma zao walikuwa wakina Chief Ra, Samia X, D-Rob na Mzazi K-Single kwa umoja wao walijipambanua kama kWANZA UNIT.
  Kabla hatujaenda mbali sana, wanakuja UNIQUE SISTERZ aka Watoto wa kipozi.... Ofcz hawa wadada walitoa mchango sana as ninavyokumbuka Hashimu kabla ya kutoa "tunasonga" alishirikishwa na hawa wadada.
  Kitu kikubwa ninachopenda Game yetu kipindi kile hakukuwa na kubebana, uwezo uliosukumwa na kipaji thabiti ndio pekee kilichokuwa kinasukuma music.
  98....chuzi limekubali mambo yee mambo waa.. Lol wazazi Hard Blasterz walileta changamoto kidogo... Wapi BiG Will, Fanani na Nigga J!
  Pia heshima nyingi sana kwa Master J kufungua kwake upande studio ya rap ilisaidia sana na kwa kiasi kikubwa ilifungua sana milango kwa vipaji mtaani. Pia kurejea kwa P. Funk na kufungua kwa Bongo Records!
  Hii iliendana na kuanza kwa tarent show za kutosha......
  Sina kumbukumbu za kivile kwamba ni nani aliyeandaa ile Talent show ambayo ilipelekea kuletwa pamoja kwa vichwa kama X-man ambaye baadae akaamua kujiita J-mo, Solo Thang, Mchizi Mox, Gado na Jaffarai wote waliitwa WATEULE. Nadhani miongoni mwa Talent show ambazo zimekuwa na mafanikio sana kwa maana ya kuleta wana-music wenye mchango endelevu kwenye Game ni hii iliyowatoa WATEULE.
  Kuingia kwa wateule kwenye Game miaka ya 99 mwishoni.... Ila bado utabaki ukweli kuwa WATEULE ile haitakuja kurudi na hili limeendelea kuwa tatizo kwenye game yetu hamna kitu ambacho Guru wa GANGSTAR alikiita "longvity" kwamba ma-EMCEE wengi hawana uendelevu katika ubora wao ndio maana hata nikipanga orodha ya hawa ambao leo wanaitwa wasanii na ukiringanisha walipokuwa ma-EMCEE ni utakubaliana na Guru na UKWELI...!
  Tunaendelea.
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mwaka 98 hivi jamaa wa clouds ndio wanafungua redio yao....
  Kitu kikubwa walichokuwa wamepatia kwa kipindi kile ni kwamba ilionekana kuwa ni redio ya music hasa...
  Kipindi cha Dr Beat chini ya K-Single na baadae kidogo Big Dog ML Chriss!
  Pamoja na mambo mengine jamaa walipatia sana kwenye kupiga kopo za hiphop na R n' B za ukweli ambazo redio zingine zilikuwa zikipigwa kwa nadra sana.
  Vilevile udau wa wakina K-Single katika Game ilifanya ailete music inayoendelea mtaani katika redio na kuongeza kuchochea....
  Hii ilitoa njia kwa wadau wengine wa music kujimwaga katika redio hii na kutupa utamu zaidi...
  Naamini nyuma ya akina K-Single kulikuwa na number one tz Deejay "Born Luv".....
  Hawa na vichwa vingine vilitengeneza chachu ya aina yake katika medani ya redio na utangazaji pamoja upangiliaji wa vipindi vya music hapa home.
  Mtaa ukaanza kupata mwanga kwamba sasa "media" imepatikana sababu wapo wenzetu!
  Sio kwamba "Radio One" haikuwapo..... Hapana! Ilikuwepo sana tu sema kujaza kwake watangazaji wa kutoka RTD ilipoteza mvuto., japo wakina Mike Mhagama walikuja kufanya vizuri sana hadi kuasisi jina la "BongoFleva" ie leo hii tunaambiwa eti ndio genre ya music yetu.... tuendelee!
  Kwa namna hii ilikuwa rahisi sana kwa mwaka 99 hiphop ya bongo kupata uwanda mahsusi kwa harakati zake.....
  Pilika pilika za Master J kutanua studio maalum ya Hiphop akitenganisha na ile ya Choir na Bendi....
  P Funk majani anajongea....
  Hiphop kwenye biashara
   
 5. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  kuna watu historia ya muziki hiphop bongo inawasahau sana,ni kwamba hawakuwa na mchango unaoeshimika au?Saleh Jabir,Mc Ndolo,Afroreign nk
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nakupongeza kwa jitihada..

  Siku zote ni vizuri kufanya research/utafiti wa kutosha ili habari yako iwe na nguvu zaidi, kwa kukusaidia na utafiti hebu pita kwenye hii tovuti ya kitambo kidogo iliyotengenezwa na Royal Swedish Music Museum...

  Rap, ragga, reggae in East Africa: Dar es Salaam

  Halafu pia nunua/tafuta/azima kitabu hiki:

  " The Vinyl Ain't Final: Hip-Hop and the Globalisation of Black Popular Culture"

  Amazon.com: The Vinyl Ain't Final: Hip-Hop and the Globalisation of Black Popular Culture (9780745319407): Dipannita Basu, Sidney J. Lemelle, Robin D. G. Kelley: Books
   
 7. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hawezi kusahaulika mtu kama kila mtu atacheza nafasi yake katika kuweka kumbukumbu sawa!
  Nmejaribu kufungua kama mjadala endelevu juu ya music yetu,
  hivyo siwezi kumfunga mtu kwenye kuchangia sababu music ni mali ya jamii wala sio ya mtu au taasi flani.
  Binafsi sikuwahi kuvutiwa sana na hao uliowataja hvyo toka kipindi hcho sikuwa nawafuatilia sana.
  Nimejaribu kuangalia kuanzia enzi za ujio wa Sugu na Kwanza Unit sababu watu hawa wameendelea kuisindikiza na kusimamia harakati za hiphop mpaka sasa na ujio wao ulikuja na chachu ya namna ya pekee kwenye music.
  Ila nitafurahi kupata michango kutoka pande tofauti ili tuweke msawazo katika kumbukumbu,
  Binafsi siwezi kusema kila kitu ndo maana nkaleta hapa jukwaani ili tujengane Mkuu
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ahsante Bantu!
  Umeongezea vya kutosha kwenye lengo langu kuweka kumbukumbu sawa kwenye music yetu hasa hiphop, kweli hzo link ni za muhimu sana hata mi sikupata zipitia kabla!
  Ideally nltaka kujenga mwanzo wa kujadili ambavyo havijawahi kujadilika (kuchokoza mjadala), hvyo vingi ninavyovitoa ni vile ambavyo nimekuwa nikivishuhudia kwa macho na kushiriki kwa njia moja au nyingine.
  Nakubali kuna magap katika mtiririko wangu ndio maana nikaleta hapa ili kwa wingi wetu na upungufu wa kila atakayechangia hapa tukamilishe lengo katika kuishehenisha JF na kumbukumbu muhimu juu ya music yetu.
  Karibu sana kwa mchango zaidi Mkuu.
   
 9. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2013
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,316
  Likes Received: 8,419
  Trophy Points: 280
  dah! huu mjadala ungeendelea ingekuwa poa sana.
   
Loading...