Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa leo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kuna ombi la Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo anataka kusema jambo.
Amesema kwa kutumia kanuni namba 70 ya kanuni za Kudumu za Bunge Tolea la Februari 2023 anampa nafasi ya kusema ambayo inasema kutokusema uongo Bungeni.
Soma, Pia: Gambo aibua tuhuma za ufisadi wa mabilioni Arusha, Spika Tulia amwagiza Mchengerwa kuandaa ripoti iwasilishwe Bungeni
Mapema leo Jumatano Aprili 23, 2025, Spika aliagiza Mbunge huyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mohamed Mchengerwa wakasikilizwe na Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya kuwa na mabisho kuhusu tuhuma ambazo zilikuwa zimeibuliwa kutoka Arusha.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Mheshimiwa Spika, utakumbuka ilitokea sintofahamu leo asubuhi. Baada ya kukaa na kutafakari nimeona niombe radhi," amesema Gambo.
Gambo amesema katika kipindi cha asubuhi ulitokea aliouita mtifuano ambao hakutaja nini maana yake.
Mbunge huyo amesema hawezi kuendelea zaidi kwani makofi ya wabunge yameonyesha kuwa wamemsamehe hivyo anaomba aishie hapo asije akaharibu.