galax s4 clone

structuralist

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,230
Reaction score
911
wadau nataka kununu galax s4 clone ila sina uelewa wa kutosha hasa kuhusu ubora na mapungufu yake. Najua kuliwahi kuwa na hyo mada wakati ule chief mkwawa aliposema anaziuza,ila nimejaribu kutafuta ile mada hakika sijaipata. Naombeni kujuzwa zaid tafadhal ukizingatia jamaa kasema price ni 350,
 

Hukuweka juhudi za kutosha kutafuta hiyo mada. Nimekusaidia kuitafuta. Iko HAPA. Enjoy S4 Clone
 
sina tena hizo simu na uwe makini sana siku hizi kuna clone fake nyingi
 
Hukuweka juhudi za kutosha kutafuta hiyo mada. Nimekusaidia kuitafuta. Iko HAPA. Enjoy S4 Clone

Hasante sana mkuu kwa msaada wako. Niliweka juhudi ila vitu viwili nahsi vilichangia kutofanikiwa. Moja kutokuwa mtaalam sana wa mambo ya kutafuta vitu humu jukwaani. Pili natumia simu na hainipi fursa nzuri ya kutafuta habar,ndio maana nilitafuta page baada ya page hadi kufika 16 nikachoka,ndipo hapo nikatafuta njia mbadala
 
sina tena hizo simu na uwe makini sana siku hizi kuna clone fake nyingi

chif imekuaje tena huleti mzigo,vp i hope kwenye yale maelezo yako no inayoonekana pale ni yakwako,nipo sawa? ningependa nikuchek unipe details za kutosha mkuu hasa kunisaidia kujua clone fake. Thx mkui
 

Ni PM mkuu nnayo clone in a good condition kwa bei cheap zaidi ya iyo..
 
nyengine ni clone sio fake mfano no1 s6 haijaandikwa hata sehemu neno samsung ila wameclone specs na umbo


cloning, imitation, faking yote ni yaleyale mkuu, watu wamepatent mpaka design, anayeiga hata muonekano tu hata kama amebadili jina yuko sawa na hao wengine tu! BTW, zile clone zako zilikuwa vizuri mkuu, vipi mbona sku hizi hauzileti? demand iko juu sana!
 
ivi guys unawezaje kutofautisha fake from real ones. maana jamaa wamekuwa hatari mno
 
sina tena hizo simu na uwe makini sana siku hizi kuna clone fake nyingi
hakuna cha ''clone fake''. hizo simu zote unazowauzia ni feki! sio original! hakuna feki yenye afadhali hapo na wala hakunaga cha grade kwenye simu feki! hizo ni market strategy, clone ni clone!! welcum to the world of clone-fake-counterfeit.....!!aka simu feki za kichina!
 

maybe najudge kilugha zaidi.

1. simu inayoitwa jina ambalo si lake hio ni fake. mfano clone inaitwa samsung

2. simu ambayo inadanganya specs ni fake. mfano inasema ina ram 2gb wakati uhalisia ni 512mb tu.

3. hawa jamaa hawadangany specs wala hawajiiti wao samsung bali wameclone umbo la simu kama ilivyo na kueka specs zao tu. na sababu ni manufacture wadogo wa kichina hawawez kushtakiwa.
 

kaka htc one alikamatwa kaiba mic za nokia bila ubishi je htc one ni fake?


hio gs4 yenyewe imekua inspired na makumi ya feature toka lumia 920 lakini hatuiti fake
 
Naomba kuchangia hoja hapa, kama mtu mnatumia mtandao nenda Amazon.de ukaone bei za simu na unaweza kununua pia...tuachane na bei hizi za kuumizana Dar
 




Kwa sura zinavutia sana... hii ni star s9500. bei £102 amazon
 
kaka htc one alikamatwa kaiba mic za nokia bila ubishi je htc one ni fake?


hio gs4 yenyewe imekua inspired na makumi ya feature toka lumia 920 lakini hatuiti fake

Hajaclone, hajafake, hajaimitate, wamenunua component tu, tena kutoka kwa manufacturer mwenyewe, hapo mwenye kosa ni kampuni iliyowauzia, ST Micro kama sikosei! cloning inainvolve kudanganya macho na akili ya mteja kuona kama ananunua kifaa A kumbe ni kinafanana tu na kifaa A na uhalisi wake ni kifaa Z, hapo utaona kwa nini HTC One haiwezi kuitwa fake kwa sababu ya hiyo chip tu! Yaani tunaposema S4 Clone, mtu anainunua kwa sababu ni mfano wa S4 na inaonekana kama S4, na mtengenezaji ameitengeneza hivo kwa sababu anajua soko la S4 lilivyo na anatake advantage....thats faking!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…