Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Wananchi zaidi ya 8,000 Katika Kijiji cha Ndogomi , Kata ya Magenge ,Wilayani Gairo Mkoani Morogoro wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya Maji safi na salama mara baada ya Serikali kutoa fedha Shilingi Milioni 894 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Maji.
Akizindua mradi wa Tank la Maji lenye Lita 150,000 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndg, Ismail Ali Ussi pamoja na wakazi wa eneo hilo wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Gairo Mh,Ahmedy Shabiby kwa kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali katika kuhakikisha wanapata maendeleleo.
Awali akizungumza Mbunge wa Jimbo la Gairo Mh ,Ahmedy Shabiby aweipongeza Wizara ya Maji pamoja na Wakala wa Maji safi na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Morogoro kwa kushirikiana kwa pamoja hadi wameweza kufanikisha upatikanaji wa Maji umekuwa wa uhakikika kwa wananchi.
Sanjari na hayo Mbunge huyo amewataka Wananchi wawe mabalozi wa kulinda na kutunza mindombinu yote ambayo Serikali imekuwa ikitoa fedha ili miradi hiyo iweze kunufaisha kizazi kilichopo na Vizazi vijavyo.