GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Ni Kwamba Muda Si Mfupi Mtangazaji Wa Zamani Wa Clouds FM Gadner G. Habash Ambaye Baadae Hadi Hivi Sasa Alikuwa Akitangaza Kituo Cha Redio Cha E FM Ametoka Kumalizana Na Uongozi Wa Clouds Media Group Na Kwamba Sasa Ni RASMI Kuwa Kuanzia Jumatatu Ijayo Atakuwa Akitangaza Katika Kipindi Cha JAHAZI.
Pongezi Kwake Gadner G. Habash Na Uongozi Mzima Wa Clouds Media Group Kwani Hakika Sasa Tutaanza Kuiona Ile Clouds Ya KITEGA UCHUMI Yenye Mafundi Watupu Akina Fina Na Kipanya Katika Power Breakfast Na Gadner Katika Jahazi.
Naomba Kuwasilisha Na Nirudie Tena Kusisitiza Kuwa TAARIFA HII HAINA CHEMBE YOYOTE YA DHANA NZIMA YA SIKU YA WAJINGA Kwani UKWELI Ndio Huo.
=======================
RASMI
Gadner akisaini mkataba wa kujiunga tena na Clouds FM akiwa na Meneja wa Vipindi wa kituo hicho, Shafii Dauda.
Hatimaye zile taarifa nyeti za dodoso kuhusu kurejea kwa Gadner Clouds FM zimethibitika pasi na chembe ya shaka.
Gadner amerejea tena Clouds Fm akitokea EFM alikokuwa akifanya kipindi cha jioni kiitwacho Ubaoni. Kabla ya kuajirwa na radio EFM, 'G' alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha Times FM. Kwa sasa, mtangazaji huyo anatarajiwa kurejea kwenye kipindi chake cha jioni cha Jahazi ambacho kilijizolea umaarufu mkubwa chini ya uendeshaji wake wa enzi hizo.
Gadner almaarufu kwa jina la utani ‘Captain’, anaingia kwenye kikosi cha Clouds FM ambacho hivi karibuni kiliweweseka kufuatia watangazaji wake wawili, Gerald Hando na Paul James wa kipindi cha PowerBreakfast kuacha kazi na kudaiwa kuingia mkataba mnono na E-FM radio.