barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Fyekeo la Magufuli limewakuta Madaktali wa hospital za Rufaa....
Mishahara imepunguzwa kwa 30% kuanzia July hii, lengo ni kuwafanya walingane na Madaktari wa hospital za kawaida (District & Regional Hospital). Itakumbukwa kuwa kwa kiwango cha Elimu wengi wa Madaktari wa Wilaya na Mikoa wapo sawa na wale wa Hospital za Rufaa, lakini kwa kuzingatia kazi na mlundikano wa majukumu ya kuwahudumia wagonjwa, hawa wa Hospital za Rufaa sasa watapata sawa tu na wale wa zile za Wilaya na Mikoa.
Kauli hii imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati akiingea na Watumishi wa afya katika Hospital ya Rufaa ya Bugando
Hali hii inaweza kupunguza morali kwa madaktari wengi wa hospital za rufaa, japo tetesi zinasema hospital za Muhimbili, KCMC na Bungando zinaweza zisiathirike na punguzo hili. Kada nyingine pia zijiandae kupunguziwa mishahara ili kuendena na dhana ya "HAPA KAZI TU" katika kufika lengo la Serikali ya Viwanda na pato la kati kwa kila mwananchi ifikapo 2025
Hatua hii inaweza kuzorotesha huduma za afya katika baadhi ya hospitali za rufaa
HAPA KAZI TU....

Baadhi ya Hospitali binafsi zimeanza kupunguza mishahara ya watumishi wake wakiwemo madaktari ili kutekeleza agizo la Serikali la kuwa na uwiano wa mishahara baina ya watumishi wa kada ya afya katika sekta binafsi na sekta ya umma. Agizo hilo la serikali limelenga kupunguza utofauti mkubwa wa mishahara kwa madaktari na watumishi wengine wa afya kati ya sekta binafsi na sekta ya umma. Pia kuzuia madaktari wa hospitali za umma kukimbilia sekta binafsi kutokana na kuvutwa na mishahara mikubwa.
Hospitali ya rufaa Bugando imeanza kutekeleza agizo hilo kwaa kupunguza mishahara kwa madaktari wapya kwa 30% kutoka mishahara wanayolipwa kwa sasa. Nimefanikiwa kupata barua ya mmoja wa madaktari hospitalini hapo inayoonesha kupunguziwa mshahara wake kutoka 2,100,000/= hadi 1,470,000/= ikiwa ni punguzo la 30%. Kwa utaratibu huu mpya, ina maanisha daktari anayetibu KCMC au Bugando atakuwa na mshahara unaolingana na daktari wa Ndanda au Ukerewe ikiwa watakuwa na sifa na uzoefu unaofanana.
#MyTAKE
Kwa leo sitoi maoni yoyote kuhusu suala hili. Ningependa kusikia kutoka kwenu, then nitaunganisha maoni yenu na yangu katika makala yangu gazeti la Mwananchi jumamosi. Karibuni.!!
Malisa Godlisten