Fursa za kutangaza biashara zako China

Fursa za kutangaza biashara zako China

BarakaMaiseli

Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
9
Reaction score
5
Watanzania wenzetu, kampuni yetu ya TSHDF (www.tshdf.co.tz), kwa kushirikiana na kampuni ya nchini China inayoitwa Heilongjiang Jingxing Technology Co. LTD wameingia makubaliano ya kuanzisha mradi mkubwa wenye lengo la kuunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa china. Pia, mradi unakusudia kuwatengenezea mazingira wafanyabiashara wa Tanzania waweze kutangaza biashara na huduma zao China. Kwa sasa, mradi upo katika hatua za mwishoni kukamilika, na tunaiona kuwa hii ni fursa nzuri kwa wafanyabiashara wa ngazi zote kufahamika kwa urahisi na wafanya biashara (pamoja na watumiaji wa bidhaa) wa China, nchi ambayo ina wastani wa zaidi ya watu bilioni 1.3—ikilinganishwa na wastani wa takribani watu milioni 60 Tanzania, ambayo ni kama 4.6% tu ya idadi ya watu China.

Mafanikio ya mradi wetu, kwa asilimia kubwa, yanategemea ushiriki wako mtanzania. Kuweza kufanikisha kutangazwa, kuna baadhi ya taarifa tutazihitaji kutoka kwako ili ziingizwe kwenye tovuti:

(1) Biashara yako inahusu nini
(2) Maelezo zaidi kuhusu biashara yako
(3) Kama una “business name” au kampuni, tungependa kupata majina yake
(4) Picha mnato na video (zenye ubora, au zilizopigwa “professionally”) kuonesha bidhaa zako
(5) Mawasiliano
(6) Muda wa kazi, iwapo wateja watapendelea kukutembelea kazini

Wito huu haujaishi kwamba unafanya biashara ndogo au kubwa. Lakini pia tungependa kuwapa mwanga kwa baadhi ya vitu vinavyohitajika zaidi kwenye soko la china:

(1) Asali ya asili
(2) Ndizi
(3) Kahawa
(4) Mapambo yanayoonesha utamaduni wetu wa asili

Kwa kuongeza, watalii wengi nchini China wangependa kutembelea Tanzania, hasa kwenye maeneo yenye vivutio na kumbukumbu za kihistoria. Changamoto moja waliyonayo ni kuwa wanakosa taarifa za msingi zitakazowawezesha kututembelea. Mfano wa taarifa hizo ni kama hoteli za kufikia, maeneo ya kuvutia, hali ya usalama wa nchi, na huduma za usafiri. Mradi wetu pia unahusika na haya mambo yaliyotajwa, na iwapo ni mdau utatusaidia kufanikisha mradi huku wewe pia ukijitangaza.

Kufahamu zaidi kuhusu mradi na namna ya kukufikia, tunaomba uwasiliane na sisi kupitia mawasiliano hapa chini:

(a) Email: chiefsecretary@tshdf.co.tz

(b) Mobile & Whatsapp: +86-15545260875

Karibuni sana tuijenge nchi yetu. Unaweza kuona sehemu ya maendeleo ya mradi wetu kupitia tovuti Amaze UI Examples au picha iliyoambatana na ujumbe huu.
 

Attachments

  • tachmall.jpg
    tachmall.jpg
    63.3 KB · Views: 65
Back
Top Bottom