Fursa za biashara zilizopo mkoa wa Dar es Salaam

Mar 21, 2021
10
11
Za mida wapendwa.

Uzi wa leo ni wa kuangalia za biashara zilizopo mkoa wa DSM tu. Na kama uzi huu utazaa matunda basi bila shaka tutaelekea mkoa mwingine.

1. Kushona nguo- hapa ukipata fundi mzuri, unatoboa. Sio lazima ujue kushona.

2.Kuuza icecream za mia mia-hapa ukiwa mchapa kazi bila kuchoka unapiga hela vizuri tu.

3.Kulima na kusambaza mboga mboga- watu wanaolima mboga mboga watanielewa.

4.Kufuga kuku wa mayai pomoja na nyama.

5. Kufungua car wash sehemu iliyochangamka.

6. Kupika na kusambaza vyakula maofisini, kama kule posta mara nyingi vyakula vinakua sio vizuri, packaging mbaya na bei ni ya juu.

7. Kutengeneza na kuuza vifungishio vya zawadi.

8. Kupika vyakula vya hasili, kama mrenda, ugali mwekundu, ndizi za makabila tofauti tofauti n.k

9. Kuna watu mikoani wanatamani sana kuja DSM kuchukua mzigo KKO, ila ni gharama kwao, unaweza ukawatafuta hawa wajasiliamali wadogo, kwa uwaminifu mkubwa ukawachulia mzigo, na wewe ukawa unaweka kamisheni yako kidogo.

.............

Tuongezee mengine hapo chini bila kusahau kupatina connections, kwa wenye mitaji ama fursa kukutana.

Mfano unaweza usiwe na mtaji lakini una fursa ni vizuri ukashare na vice versa.
 
Biashara ya Mkaa ukiwa na mtaji wa kutosha na eneo zuri la biashara hiyo huwa inalipa sana wauzaji wote wa Mkaa nafikiri mmenielewa.
 
Biashara ya Mkaa ukiwa na mtaji wa kutosha na eneo zuri la biashara hiyo huwa inalipa sana wauzaji wote wa Mkaa nafikiri mmenielewa.
Biashara ya mkaa bwana nzuri kuuza mjini tu ila kule porini isikie tu aisee niliishia kuchoma mtaji na kurudi na nyuzi kadhaa za chain saw, ulaaniwe mkaa *****
 
Back
Top Bottom