Tatizo la Watanzania ni moja, mnapenda sana kutafuniwa, utakuta mtu hapa anataka kujua fulsa za Zambia, basi ataanza kuuliza mpaka Nauli ya Daladala ni bei gani kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ataanza kuuliza mpaka Vocha zinauzwa Bei gani!
Muwe mnauliza maswali Yale ambayo ni Main Question, vitu vingine utakutana navyo huko huko......na utakuta mtu analalamika hapa "Ohh watu wachoyo kutoa information ilhari yeye mwenyewe hajawahi kutoa kile anachojua kwa wengine.....Binafsi nimepeleka Biashara South Africa na Zambia....sasa kwa vile Uzi unazungumzia kuhusu biashara kwa Zambia, Mimi ntaorodhesha biashara chache ambazo ni deal Zambia.....
Zambia wana uhitaji mkubwa sana na Mboga....
1.Dagaa wa Tanganyika na Victoria...
Inabidi uwe na Mawasiliano na Madalali au Buyers wa Dagaa Sokoni, coz kama Dagaa wa MWANZA wakiwa Sokoni then Dagaa wa Tanganyika wakaingia Sokoni, Dagaa wa Mwanza hawatatembea kwa wakati.
Price kwa Gunia la 50 kg kwa Kitwe na Ndola ni around 400,000 t'sh....
Kama utafikisha mzigo Lusaka utauza zaidi.
Kama utafanikiwa kufikisha Dagaa hao hao huko Congo kuna mji mmoja wa kibiashara unaitwa (Mbunjimayi) utauza zaidi ya 700,000 na kuendelea kila Gunia...
Kwa Gunia la 100 kg weka ×2.
Mchele pia ni biashara nzuri Zambia, sio Michele tu, ila Mchele toka Mbeya, wenyewe wanaita Mchele wa Nakonde...
Kule wanauza kwa Gallon ambalo lina kama kilo 5 na price kwa Gallon hasa mijini ni around 100 Kwacha kama 20,000+ t'sh
Ukiwa na Mchele wa Mbeya mzigo haukai.....unaweza kuwa na stock ya kutosha ukauza mtaani tu ukamaliza, pia kama una Connection unaweza kukopesha Wafanyakazi kwa around 120 Kwacha kwa kipindi flani, na ikakulipa zaidi.
Simu, Nguo, Mabegi wa Wadada, Viatu n.k
Hivyo vyote ni deal Zambia, kumbuka wanategemea vitu vingi toka Dar es salaam, na huko bidhaa huuzwa aghari kuliko Dar so ukipeleka chochote utapata faida nzuri.....
Ukiacha Lusaka mji wa pili ambao nashauri upeleke Biashara yako ni Kitwe!
Kwa nini?
Kwa sababu ni kitovu cha Biashara toka nchi 3, kwa maana ya Zambia yenyewe, Congo na Angola, Wafanyabiashara toka Congo na Angola huenda Kitwe kununua Mizigo ya Biashara.....
Kuna fulsa pia za Madini Copper, Gold, Zinc, Uranium, Emalard n.k....
Gold ndo wameanza kuchimba miaka si mingi, wana kiwango kikubwa sana cha Dhahabu, kuna maeneo nafahamu kama huko Solwezi wana kiwango mpaka cha 200+ grams per 1 tonne......
Pia kuna fulsa za Mbao, kuna mbao ni deal Sokoni zinaitwa Rosewood, kuna zingine ndo moja kati ya mbao zinazouzwa aghari Duniani zinaitwa Mukura, japo Congo zipo nyingi zaidi kuliko Zambia.
All in all kufanya Biashara kwenda nchi nyingine unahitaji uwe na roho ngumu, uwe Risk taker, kama una roho nyepesi, baki hapa hapa Bongo!