Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 6,088
- 15,725
Hizi ni fursa za biashara ambazo mtu anaweza akafanya maeneo ya ufukweni mwa bahari ambapo watu wengi huenda kwa ajili ya matembezi au mapumziko.
1. Kukodisha Life Jacket kwa ajili ya kuogelea
Sehemu nyingi kwenye fukwe watu hutumia tube za gari zilizojazwa upepo kama boya la kuogelea.
Kama ukinunua life jacket au life vest ambazo ni maalum na zina usalama mtu akiwa katika maji utavutia watu wengi.
Mfano life jacket 1 ukinunua kwa elfu 70. Na ukawa unakodisha kwa robo saa kwa shilingi 500 -1000. Kwa siku unawastani wa kupata elfu 5 kiwango cha chini kwa kila life jacket 1.
Life jacket au vest inabidi uweke za watoto na wakubwa.
2.Kukodisha nguo au vifaa vya kuogelea kama miwani ya kwenye maji (Swimming Gears)
Ukiwa na nguo za kuogelea za wanaume na wanawake unaweza ukawa unakodisha au kuwauzia moja kwa moja kwa zile ambazo hazijatumika.
Pia unaweza ukaweka vifaa kama miwani ya kuogelea.
3. Kuweka pikipiki za michezo ya majini (Jet Skies and Water Bicycle)
Hii inaitaji mtaji kidogo kununua Jet skies au kiswahili tunaweza kuita pikipiki maji.
Jet skies mpya makadirio ya bei ni kama Usd 4500 ikiwa mpya yenye engine ya kawaida.Hapa utakuwa na machaguo kati ya umeme na ya mafuta kulingana na uhitaji wako.
Na ukiwa unafanya biashara hii mtu akikodi huwa hulipa kwa muda. Mfano kwenye mahoteli makubwa kukodi kwa dakika 15 huanzia Usd 50. Sasa kwa wazawa utapanga uweke bei ipi.
Marine bicycle hizi ni baiskeli za majini hazitumii nishati yoyote zaidi ya nguvu ya mwendeshaji.
Biashara nyingine kama picha za hapo kwa hapo,pop corn,juisi na take away food wengine mtaongezea.