Fursa ya biashara ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fursa ya biashara ni nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mgombezi, Jun 8, 2012.

 1. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  FURSA YA BIASHARA NI NINI?

  Watu wengi wamekuwa wakijiuliza biashara za kuanza kufanya, wakati mwingine kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwa na kianzio cha biashara (mtaji), lakini hawafahamu ni biashara gani wataweza kufanya.

  Fursa ya Biashara (Business Oppurtunity) hutokana na mahitaji ya watu katika eneo husika; kwahiyo katika kutengeneza wazo la biashara (Business idea) huanza kwanza kwa kuchunuguza fursa zilizopo katika eneo husika. Baada ya hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan).

  Kwa hiyo unapofikiria ni biashara gani ya kufanya ni vyema kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo husika (inaweza kuwa mtaani kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli nchi yetu bado kuna mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya biashara; hebu jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana nazo, naomba kuorodhesha baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji:

  1. Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa urahisi?
  2. Je unapotaka kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa urahisi?
  3. Je unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri kutoka eneo lako uko vipi?
  4. Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna vitendea kazi vya kutosha?
  5. Vitu gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi au shughuli za kila siku?
  6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira gani?
  7. .............................
  8. .............................

  Wengine wanaweza kuendeleza, mambo ambayo tunaweza kuchunguza kutokana na mazingira husika.

  Jambo lolote ambalo utaliona ni hitaji kwa watu basi hiyo ndio fursa ya biashara, kwa hiyo unapaswa kutengeza wazo la biashara. Tuache kuyachukulia mazingira yanayotuzunguka na mambo yanayoendelea katika jamii kuwa ni kawaida, kwa mfano unaweza kuwa unakwenda kupanda daladala kila siku kwa kugombania na ukachukulia hiyo ndio hali ya kawaida, lakini tunaweza kutumia hiyo hali kama fursa ya biashara na kutengeneza wazo la biashara.

  Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi; itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka. Hebu tuige mfano wa Mjasiriamali Bakhresa na kampuni yake ya AZAM, kwamba amekuwa akichunguza mahitaji ya jamii na kuleta bidhaa ambayo itakutana na hitaji hilo, mfano; CHAPATI, MIKATE, TUI LA NAZI na nyinginezo.

  Vile vile tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa fursa za biashara ndani ya Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana katika nchi zilizoendelea wamekuwa na biashara za mitandao na biashara nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi kuona baadhi ya link zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao n.k. Nafikiri bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa kuyatatua.

  Nawatakia kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la kutegemea bidhaa kutoka nje; yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha meno, miti ya kuchoma mishikaki n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu wamekuwa wakitoka mbali na wakifika hapa wanabaini fursa za biashara na kurudi kwao kutendea kazi.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ni kweli unavyo sema but Tatizo ni kwa sisi watanzania tunapenda sana Biashara zisizo kuwa na feature yoyote ile kisa tu zinaingiza pesa ya chapu chapu, na ukiona umeanzisha biashara leo na kesho kutwa unaanza kutengeneza faida ujue hiyo ni ya muda sana,

  Na tumekuwa waoga kwa project ngumu ambazo ndo zenye utajiri, kisa tunataka pesa ya haraka haraka, leo hii watanzania wengi hawataki kuwekeza kwenye project kama zaKilimo na ufugaji kwa sababu tu zinachukua muda mrefu sana kutengezea profiti, mtu anaona bora akanunue Toyo zake za kubeba watu,

  Na mwisho kabisa watu tunafanya Biashara bila malengo, jaribu kufanya kautafiti pita mitaani kwa wafanya biashara wa aina mbali mabli na waulize wana malengo gani na biashara zao,

  - Mtu anaweza kuwa siriasi na biashara lakini kumbe lengo lake ni anunue gari la kutembelea, akisha nunua gari basi kiu yake imeisha, sasa kwa mtindo huu hatuwezi piga hatua na ndo maana unaona watu wanashindwa kugraduate

  - Kuna watu wako katika biashara mbali mbali lakini leo ukamwambia kuna ajira mahali fulani basi atafunga biashara yake fasta na kwenda kuajiriwa,

  SO AIDEA HAZIWEZI FANYA KAZI ENDAPO HATUTAKUWA NA MALENGO NA BIASHARA ZETU, CHUKULIA MFANO MTU ANAFUGA KUKU HUU NI MWAKA WA KUMI NA IDADI YA KUKU NI WALE WALE,

  MTU ANA MGAHAWA WAKE HUU NI MWAKA WA 15 ILA HAKUNA CHANGES ZOZOTE ZILE, NI LAZIMA BIASHARA NDOGO IGRADUATE KWENDA YA KATI NA BAADAE IGRADUATE KUTOKA BIASHARA YA KATI KWENDA BIASHARA KUBWA,
   
 3. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  asante kwa ushauli wako mzuri.mungu akujalie na akupe mafanikio
   
 4. L

  Luushu JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 593
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  Fursa sawa katika biashara yako uwe umeajiriwa,uwe huna ajira njoo ubungo plaza kesho saa saba kamili namna ya kufika tuma PM kwangu weka namba ya simu takupigia utaingia bure ili usikilize kuhusu fursa ya biashara mungu anatupenda wote
   
 5. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Fursa za biashara ni mapengo ya mahitaji yanayotakiwa kuzibwa kwa jamii kupatiwa bidhaa au huduma zinazokosekana. Lugha ingine fursa ni matatizo yanaotakiwa kutatuliwa.

  Umeelezea vizuri lakini mada hujaiweka vizuri kwa namna ya watu kuchangia au kupata mtiririko mzuri utakaowasaidia katika kuanzisha na kuendesha biashara zao.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu bila shaka unazungumzia Forever Living,na kama sio hiyo basi ni GNLD
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
   
 9. Kuku wa Kabanga

  Kuku wa Kabanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 804
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  ambayo kwa mazingira yetu ni ngumu sana kufanya,hawa jamaa bidhaa zao zina bei sana na pia kujiunga ni gharama,ndo maana wanaofaidika ni wale waliojiunga mapema.
   
Loading...