Fursa kwa Wafugaji: Naanzisha Poultry Slaughtering & Processing Plant

Fursa kwa Wafugaji: Naanzisha Poultry Slaughtering & Processing Plant

Jack HD

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
851
Reaction score
1,170
Habari wana jukwaa.

Kwa miaka kadhaa nimekuwa mfugaji wa kuku hususani kuku wa kienyeji, chotara na broilers ila kwa miaka ya karibuni nimejikita zaidi kwenye kufuga broilers.

Kwa mara kadhaa, nimekuwa nikivutiwa sana na kuanzisha machinjio ya kuku, kufanya packaging na kusupply hii ni kutokana na kutoeleweka kwa soko kipindi bei ya soko la kuku ikiporomoka. Nikaona ni bora kuanza kufanya processing mwenyewe.

Jana nimebahatika kupita sehemu ambazo wananunua kuku na nimekutana na baadhi ya wazabuni walioshika tender za kusupply kwenye hotel kadhaa na wakanipa requirement zao na mahitaji kiujumla.

Kiukweli uhitaji ni mkubwa, japo binafsi ni mfugaji pia lakini siwezi kusupply kwa wingi kama nikitumia kuku wangu pekee, hivyo basi ningependa kupata wafugaji wenye uwezo wa kufuga kuku broilers na tuingie makubaliano ya mimi kununua kuku wao.

Hvyo basi, kwa mwenye kuona itampendeza kujumuika katika fursa hii asisite kuwasiliana. Hakikisha wewe ni Mfugaji aliye Dar es Salaam, Uwe na uwezo wa kufuga kuanzia kuku 500. Kuhusiana na ubora wa kuku tunaonunua tafadhali tuwasiliane.

Nipm ama nicheki Whatsapp +255 717 810 141
 
Back
Top Bottom