officialBossmtoto
JF-Expert Member
- Jul 1, 2019
- 370
- 1,227
Habari wana jamvi wenzangu. Poleni sana lakini pia hongereni sana kwa majukumu ya kutimiza ndoto zenu. Kwanza niseme kabla ya kuendelea kwamba uzi huu sio rafiki sana kwa mtu mvivu wa kusoma, pia uzi huu unahitaji kidogo kutuliza akili ili unielewe. Tuweke mihemko pembeni.
Turudi kwenye Mada. Kumekuwa na fursa nyingi sana hapa nchini na Duniani zikiahidi vijana kuwabadilishia maisha, zingine zinafika mbali na kutumia watu ambao husema kwamba wameacha ajira za maana au biashara zao za maana na kujikita kwenye fursa hizo. Wengine pia huonyesha Magari ya kifahari na majumba makubwa kusema kwamba wameyamiliki mara tuu baada ya kuchangamkia fursa.
Hali hii huleta mgawanyiko wa makundi mawili.
Kundi la kwanza ni wale wanaoingia na kundi la pili ni wale wanaopiga vita kwa kusema ni utapeli na ni upigaji. Naomba kusema kwamba wote wako sahihi kabisa. Huu ni mtazamo wangu.
Mara nyingi fursa kama hizi zinapotokea wengi huwa wanakuwa na hizia za kutapeliwa mwanzoni na wanakuwa wazito sana kuweka au kufanya maamuzi. Kuna ambao hufanya tafiti mbalimbali kujua uhalali na uhalisia wa kitu huku wengine wakikataa kabisa hata kusikiliza. Wapo ambao wakiskia fursa kama hizo haraka haraka wanaingia bila kupeleleza na kuweka hela kwa tamaa huku wengine wakiweka hela kidogo kidogo huku wakisoma mchezo.
USHAURI WANGU
Mara nyingi hizi fursa huwa na mwisho wake. Hata wakijitahidi vipi, naona lazima itafika tu siku watasepa na mkwanja. Fuata yafuatayo ili uweze kunufaika na fursa hizi au kupunguza machungu ya kupigwa:
1:- Sikiliza kwa makini sana anaekupa fursa hii. Msikilize kwa kumzingatia na kuangalia kwanza uelewa wake juu ya jambo hili. Zingatia uweze kujua kwamba anajua anachokuambia ama amemezeshwa? M-challenge kwa maswali ya hapa na pale yenye kudodosa na kuchimba zaidi.
2:- Usikurupuke kuweka hela. Kwanza tambua historia, kisha tambua utendaji kazi. Uliza hela inatoka wapi? Sio unaambiwa tu unamuunga huyu na huyu unapata pesa, fahamu kwanza inatoka wapi? Je hela yako unayoweka ina usalama gani?
3:- Je inatambulika kiserikali? Japo hii usiipe nguvu sana. Wanaweza kua wanatambulika na wakawapiga tuu vile vile. Ila ni njia moja wapo ya kupata kaangalau fulani.
4:-Usitumie zaidi ya mwezi kufanya maamuzi. Mara nyingi tumeona fursa hizi wanaofaidi sana ni wale wa mwanzo. Mfano kama Scatec waliofunga ofisi na kusepa zao, sio kwamba watu hawakupata faida, watu walipata Faida sana. Wapo walionona mashavu kupitia scatec. Unapowahi unakua miongoni mwa wale watakaopata pata wa mwanzo kuliko kuendelea kujivuta ukose au ujiunge kwa kuchelewa ndo wale hicho ulichokiweka
5:- Usiweke hela ya Ngama. Nikisema hivi namaanisha kwamba usiweke hela unayoitegemea, usitoe kwenhe mtaji, usiuze mali yako ili weke huku, usiweke ada wala kodi.
Huku kwenye hii michezo weka hela ambayo hata ikipotea au ikiliwa unaweza jikuta unacheka tuu. Hii iwe kama kubet, muhindi anakula kila siku na watu wanaelewa kwamba hii ni bahati na sib.
Weka hela uliopewa zawadi, weka hela uliopata kwenye udalali, weka hela uliopata baada ya kuuza au kufanya biashara kwa faida kubwa zaidi. Ukishaweka hii hela unakua na machale kama mwewe.
6:- Hii ni ya muhimu sana EPUKA TAMAA. Michezo kama kalyinda, unavozidi kupata ndo hela inazidi kuongezeka. Mtu anaweza kufika mpaka laki tano, ila anawaza akitoa laki tatu na kubaki na laki mbili atarudi nyuma sana hivo anaona bora aendelee na hio laki tano. Badae inafika milioni anaona yale yale, mwisho wa siku anko mzungu anasepa nazo. Kumbe ni heri angetoa ile laki tatu acheze tena apate ingine atoe, yeye anataka izidi tuu basi.
7:- Hii ni kama onyo, Zingatia anaekuunga. Maana wapo wanaoungwa na marafiki zao, huku marafiki hao wakiwazunguka na kuchukua password wanaingia kwenye account zao wanabeba pesa.
Binafsi nimeskia Kalyinda na Scatec na kama una zingine tusaidie. ila pia hata za zamani kama deci ukifuatilia utajua ndugu zetu wa zamani walipata kweli wale wa mwanzo mwanzo. Waliozembea na kuja kujiunga mwisho, Hawa ndo walilia kweli kweli deci wanasepa wao hawajala chochote.
USHAURI huu wa bure vijana tuzingatie tuu. Hii ni namba ninayotumia mimi kupima fursa na naona kuliko nibet kwa Mbet bora nibet style hii. Nacheza kistaarabu bila tamaa na nikiona dalili za kunimeza nawahi natoa pesa yangu mapema
HII NI KAMA BAHATI NA SIBU. WEWE WAHI, WEKA HELA ZA KUSKIZIA, KAA KWA MACHALE, SUBIRIA KUTOKA KIMAISHA AU KUWATOA MAKAMPUNI KIMAISHA