Fursa Fursa Fursa Kwa Vijana 18+

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,972
3,511
Watu wengi sana wamekuwa wanachanganya maana ya neno fursa, mara utasikia ukiitwa kwenye fursa jua wewe ndiyo fursa yenyewe....Ndio ni kweli kwani aliyekuita na yeye ameona fursa.
Ngoja nianze taratibu unapoona fursa ya kufanya jambo fulani labda kutengeneza kiwanda, ukaweka mambo sawa ukatafuta wafanyakazi kuanzia wataalamu, madereva, vibarua mpaka walinzi. Wao kwao ni fursa ya kupata kazi pia kwako ni fursa ya kutengeneza faida kupitia ujuzi wao na kujituma kwao.

Watanzania wanataka fursa za kupata tu bila ya kuwekeza chochote hata betting lazima uwekeze jero ili ushinde billion 1 bonanza utaweka 200 kushinda 50k+. Hata kwenye imani lazima uwekeze maombi na utoe zaka na unasisitizwa ya kuwa njia ya uokovu ni nyembamba na ni safari isiyo nyepesi imejawa na majaribu ikiwemo ya kukata tamaa.

Kuna aina nyingi za fursa na biashara
Zipo biashara zenye risk kubwa na risk ndogo mfano pyramid scheme kama Qnet, D9, ....... Ni fursa zenye risk kubwa kwamba utoe 4+milion ununue saa alafu utafute wateja wengine wafanye kama wewe ndio upate ukikosa imekula kwako....hii ni aina ya high risk business na pengine huwezi kufanya ukiwa na akili timamu kabisa.

Mfano mwingine ni forex business mtu una mtaji wa dola 1000$ sawa na Tsh 2,300,000 anaweka lotsize ya moja akipata pips 6 ni dola 600 karbia Tsh 1,500,000 ndani ya masaa machache ama nusu saa hiyo ni very high risk business hivyo hivyo ndani ya nusu saa ama masaa machache unaweza kupoteza 2.3 million na kubaki na madeni.

NIELEZEE KUHUSU CRYTPTOCURRENCY KWA MANUFAA YA VIJANA NA TAIFA

Mimi kwa uelewa wangu huwa nashangaa sana naposikia mdau humu anapost tangazo kuwa unaweza kuchimba cryptocoin kwa kutumia simu yako ya Android hawa jamaa nawafananisha na wale wa kusalimia Good morning Usiku...lakini kiukweli wao wana akili sana kwani wanatambua ya kuwa wanachofanya ni utapeli na hamna namna unayoweza kumshtaki popote duniani na ukashinda.

Mwaka 2018 nilipata session jimbo la Pennsylavia na kujionea mechanism ya kuchimba coin za bitcoin..kwanza ule uwekezaji wa mitambo na makomputer ni zaidi ya billion 100+ za kitanzania.
Hawazalishi cryptocurrency coin kwa kutumia umeme wa kawaida kwa kuwa gharama ni kubwa hivyo utapata hasara wazalishaji wakubwa Duniani wanatumia nishati ya makaa ya mawe.

Kadiri unavyozidi kuzalisha coin nyingi ndivyo algorithms zinazidi kuwa ngumu, hivyo kuhitaji nishati zaidi na uwezo mkubwa zaidi wa computers kuweza kuwndelea kufanya uzalishaji.

Nani anamiliki Bitcoin? Kwa sasa kuna mtu ama kampuni ambayo anamiliki karibu 27% ya Bitcoin zote duniani hivyo kuna mtu mwenye uwezo wa kutikisa kwenda juu ama kushuka kwa thamani ya Bitcoin kwa kiwango ambacho yeye anadhani kinafaa.

Je watu hawaibiwi na Bitcoin? Mwaka 2021 nchini Marekani peke yake watumiaji wamepoteza takribani dola billion 40$ zaidi ya Trillion 100+ za Tanzania.
Nchini kenya mwaka huu vijana wamelizwa zaidi ya 20Billion ...hapa nimeongelea Pyramid scheme business na cryptocurrency ambayo nitaongelea Bitcoin kama mfano but zipo coin mamia kwa maelfu nataka upate uelewa mpana wa mambo yalivyo usizanie kuna pesa za bure pahali ukabebe tu...

Unaongeleaje bitcoin miaka 20 ijayo! Bitcoin ni Bubble coin 🪙. Kwamba unaweza kununua ikiwa chini kisha ikashuka zaidi na ukapata hasara au ukauza ikiwa juu na ikaendelea kupanda juu na juu zaidi na ukapata hasara. Bitcoin itaendelea kuwepo watu watapata pesa kwa wakati fulani kulingana na biashara zao, wazalishaji wataongezeka na pia kuna watu wengi tu watapoteza pesa nyingi kwenye bitcoin au cryptocurrency kwa ujumla.

Kampuni za Bitcoin duniani kote zinajulikana na wazalishaji wanaweza kuifanya icheze mdundo wautakawo wao, iwe kupanda kuwa stable ama kushuka. Pia wanaweza kuacha soko lifanye litakavyo kwa muda wa miaka kadhaa kisha wazalishaji wakubwa wanaingia kuchukuwa faida yao.

Je Kila Mtu Anaweza Kufanya Forex, cryptocurrency? Jibu rahisi ni hapana. Forex business is not for everyone only 5% are profitable traders 95% are loosers

Je Tanzania iwekeze kwenye cryptocurrency?
Hii ni biashara kama biashara zingine za technology zilivyo, nchi haiwezi kuwekeza kwa forex na crypto bali kuangalia sera zake zinavyoendana na teknolojia.
Ukitaka kufanya uwekezeji fanya utafiti ongea na wataalamu wa uchumi na biashara chambua soko na risk iliyopo kisha fanya uwekezaji huku ukijua kuna uwezekano wa faida na hasara.

Broker gani ni mzuri kwa forex?
Binafsi nimetumia brokers wengi wa forex ambaye niliona ni ecn ni Justforex broker huyu hana markets manipulation nyingi ukimpatia umempatia kweli.

Ni wapi ninaweza kuwekeza 1000$-3000$ na kupata faida ya asilimia 100+? Sehemu ya kueleweka mtandaoni na nje ya mtandao haipo dunia hii. Labda ufanye high risk business ambayo pia unaweza kuzipoteza.

Watu watapata utajiri na wengine wengi watakuwa masikini kutokana na Pyramid scheme business, forex na cryptocurrency.

NB: Graduates mliosoma IT, Software engineering, Computer Science, telecommunications, cyber security, ........ Changamkeni hamuwaoni wenzenu wanigeria, Ghanaian, USA, Canada, Ukraine, China, Korea wanafanya mambo makubwa kwa jamii na nchi yao tengenezeni vitu leteni pesa nyumbani.
Kwanza nimemkumbuka Hushpupp.. Lord of mess niishie hapa. Vita ya kiuchumi ni ngumu sana
 
Hatuna upendo huo hata ukijitahidi kuhadaa watu, ukiitwa kwenye fursa yoyote ujue wewe ndo fursa yenyewe….. unaweza kupindisha utakavyo ili uwanase maboya ila ukweli utabaki hivyo.
 
Umechelewa my Son, hapa JF palikuwa na Garacha zaidi yako, huyu alituaminisha hadi kwamba unaweza kudownload pesa na unaweza kudownload nyumba, si mwingine ni ONTARIO.

Hebu tuache kwanza tupumuwe.
 
Nikopeshe hela niingie huko madili yakitiki nitakutudishia..
Mkuu hapo nimetoa fursa ya mtu kupata uelewa na kujua kuwa high risk business kama hizo kupata na kukosa ni nusu kwa nusu 50/50 yaani mwezi mmoja unatosha kukufanya kuwa masikini wa kutupwa ama kuwa tajiri.

Ukitaka kuwekeza huko tafuta wataamamu wa uchumi na biashara mshauriane namna ya kufanya.
 
Umeanza kutrade lini? Coz lotsize ya 1 kwa pips 6 hupati $600 unapata $60
By 1lotsize 1pip equals $10 rudi darasani kwanza
 
Kwa manufaa ya wengine lot size ya 0.01 pips 10 ni sawa na dola 1.
Lot size ya 0.1 pips 10 ni sawa na dola 10$ na
Lot size ya 1 pips 10 ni sawa na dola 100$.
Lot size ya 0.05 pips 10 ni sawa na 5$
Lot size ya 0.5 pips 10 ni sawa na 50$
Nipo kwa forex industry tokea 2016.
 
Back
Top Bottom