Ardhi ni sehemu nzuri ya kupatia mtaji mkuu. Funga mkanda miezi kadhaa tumia jembe la mkono utapata tu mtaji si unajuwa tena mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe?
Ni jambo zuri na ninapenda sana kulima na nimewahi kufanya hivo na matokeo yakawa mabaya kwa miaka miwili mfululizo.
Mwaka wa kwanza nililima mpunga sikufanimiwa kwasababu hapakuwapo na mvua ya kutosha..
Mwaka ulofuata niliamua nilime mahindi, yakaliwa na wadudu 'viwavi' bado ikawa tatizo.
Ulichaguwa mazao mabaya sana kwa maana ya gharama na hata uangalizi wake na hata faida yake ni ndogo. Safari hii kalime kati ya matikiti maji, alizeti, vitunguu saumu, vitunguu maji au tangawizi. Lima ekari moja tu. Usisubiri mvua, tafuta sehemu uwe unamwagilia kwa ndoo.
Maeneo ambayo niliyatumia ni milki ya wazazi wangu hivyo sikutozwa ila nikitaka kilimo hicho inabidi niangalie maeneo yalio na mto au bwawa kwa urahisi wa kumwagilia hivyo bado tatizo lita kuwa ni lile lile la mtaji kwa sababu mwenye ardhi atahitaji chochote kitu ndipo akuruhusu utumie chake....bado shida mkuu
Fanya kazi ya udalali au affiliate marketing kwa muda kisha ukipata mtaji utaenda kulima.
Uzoefu wa hiyo kitu nao ni shida, nko dar lakin najaribu kufanya mipango ili nipate inshu ambayo itanipatia kipato hivyo hata kama ww anachochote cha kunishirikisha ntakushukuru.
Nimejaribu kucheki lakini kama sijaelewa elewa hivi!
Hauko makini, unatakiwa ufate utaratibu wa kilimo bora na kabla ya kulima unatakiwa uwe na basic needs kama mbegu bora, madawa ya kuulia wadudu, na hakikisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya kumwagilia( nafahamu labour na land kwa TZ sio tatizo sana), sio unakurupuka tu na pia ningekushauri mjiunge kwenye vikundi ndo kwa pamoja mnaweza mkapata mkopo sio wewe kama wewe....anza na hilo kwanzaMwaka wa kwanza nililima mpunga sikufanimiwa kwasababu hapakuwapo na mvua ya kutosha..
Mwaka ulofuata niliamua nilime mahindi, yakaliwa na wadudu 'viwavi' bado ikawa tatizo.
Hauko makini, unatakiwa ufate utaratibu wa kilimo bora na kabla ya kulima unatakiwa uwe na basic needs kama mbegu bora, madawa ya kuulia wadudu, na hakikisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya kumwagilia( nafahamu labour na land kwa TZ sio tatizo sana), sio unakurupuka tu na pia ningekushauri mjiunge kwenye vikundi ndo kwa pamoja mnaweza mkapata mkopo sio wewe kama wewe....anza na hilo kwanza