Furaha yao imepitiliza!

Nyie watoto, akili za kuambiwa changanyeni na zenu. Msiwe majuha.
 
wakishatoka hapo wanaenda zao madarasaniii'................
 

Attachments

  • TZ.jpg
    49.6 KB · Views: 43
  • TZZ.jpg
    34.8 KB · Views: 44
Imenikumbusha mbali! Hapo usikute wamechaguliwa wale 'wasafi' na ambao angalau wana 'yebo yebo'! Umasikini mbaya sana.

Mwalimu mkuu anakuja mstarini saa za kuondoka anasisitiza kila mmoja lazima avae viatu...na hivyo ndo viatu vilivyopo...utafanyaje ndugu yangu...
 
Reactions: SMU
shenzi kabisa me nilinua kuna cha maana humu.
 
Watoto wanaonesha wamepitiliza kwa hisia za furaha baada ya Mh.Raisi kuwatembelea.



Hii ndio Tanzania yetu....na hili ndio taifa la kesho......
Kazi ipo.....
 
Kama Mtanzania wa kawaida haguswi kwa nini yeye aguswe?

Mtanzania wa kawaida akiguswa atafanya nini??? yeye kama kichwa cha nchi ndiye msimamizi mkuu wa malengo yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maisha bora kwa kila mtz.
 
Mtanzania wa kawaida akiguswa atafanya nini??? yeye kama kichwa cha nchi ndiye msimamizi mkuu wa malengo yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maisha bora kwa kila mtz.

Kuna mengi ya kufanya sio lazima uwe Raisi ndio ufanye kitu, kama Mtanzania wa kawaida haguswi na kama kila mtu anasema hata nikiguswa nitafanya nini, basi hata Bw. Kikwete naye anasema hivyo hivyo, kama kila Mtanzania wa kawaida anavyosema anayaona matatizo lakini nitafanya nini!
Kumbuka Bw.Kikwete hajatokea Mbinguni, katokea humu humu Mtaani kwa Watanzania wa kawaida, ambao hata yeye pia alikuwa anayaona matatizo na pia alikuwa akisema ndio nayaona lkn nitafanya nini? Leo hii kawa Raisi lakini bado bado ni mtu yule yule tu Mtanzania wa kawaida kilichobadilika ni jina tu, na ndio maana hakuna jipya!

 
utoto raha kweli,liwake inyeshe ni raha tu.
mi nakumbuka tulipoenda kumpokea rais nyrere 1984 pale kdc,tulibeba majani na kumshangilia kumbe masikini nchi ilishamshinda hatukujua.
 

Hao watoto ndio watanzania wa kawaida. Uonavyo wewe wanaweza kufanya lolote kujikwamua ili wapate elimu bora??? wajijengee madarasa na kuajiri waalimu??? Rais sio mtanzania wa kawaida; ana uwezo wa kuhakikisha (kupitia baraza lake la mawaziri) Waziri wa Elimu anasimamia na kuhakikisha mambo yanaenda vizuri kwenye suala hilo la elimu, na hiyo ndiyo sababu ya yeyey kutembelea mashule.
 
maisha bora kwa kila mtanzania+elimu kwa kila mtoto=yeboyebo primary school
 

Hayo unayaona wewe, ninachotaka kukwambia ni kwamba Mtanzania wa kawaida haguswi na chochote na Bw. kikwete au Waziri yoyote yule mkubwa ametokea humu humu ktk maisha yetu haya haya ya kutojali na siku zote kusukumia tatizo na lawama wengine.

Ngoja nikuulize Watoto wa mitaani wamezagaa hovyo Dar, tena muda wa kwenda shule watoto wa miaka hata 5 wanaosha magari na kuombaomba barabarani ni watz wangapi ambao hata hilo linawagusa? wengi wanapita wamefunga na vioo hata kuwaongelesha hawataki, ni wangapi tumejaribu kuwasaidia hawa watoto?

Ni lini mara ya mwisho umeona mtu hata ameposti humu hili tatizo? Na ukitaka kuhahakisha haya ninao yasema fanya thought experement andika posti mbili tofauti moja kuhusu jinsi ya kuwasaidia watoto wa mtaani na nyingine andika CHADEMA yaigalagaza CCM halafu uangalie muitiko utakuwa wapi!

Nachotaka kusema ni kwamba kama sisi hatujaliani na hatujali maisha ya watu wengine usitegemee Kikwete au pinda aje kujali jamii, kwa maana nao wamelelewa nakukuzwa ktk mazingira ya kutojali kama sisi tu, sasa leo hii wamekuwa wakubwa hawawezi kufanya tofauti na sisi tulivyo, kwa maana nyingine viongozi ni kiio cha jamii wanayoiongoza, tabia za viongozi hazina tofauti na tabia za wananchi wanaongozwa Dunia nzima!

 
labda yebo yebo ndio sare ya shule

Hali ya maisha ya watoto wetu ni mbaya sana, jaribu kufikiri matabaka yanayotengenezwa kwa watoto hawa waliovaa yebo yebo na wale wanaosoma english medium schools ambao hata mikoba ya shule ni ya sare, hawa wengine hata viatu hawana na wenye yebo zilizokwisha ndio wenye unafuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…