Furaha yangu machinga kupewa TIN number

shangoo

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
324
360
Jana machinga wameitwa na kupewa TIN number wamefurahi sanaa pasipo kujua kazi ya TIN ni nini!
Binafsi nimefurahi sanaa kwasababu wakishajua ukweli wa haya mambo TIN number hawa TRA hawatatusumbua naamini manake wafanyabiashara wamegoma kushirikiana naamini wamachinga WAKIPEVUKA wengine tutapoma manake wana umoja sanaa.

Sijui tunaponaje yan SUNGUSUNGU wa TRA wamejaa Kariakoo hakuna pakuhemea na walivyo hawatoi hata elimu kuhusu fine,sijui hii sheria yao ya wanazitekeleza vipi manake kila kosa wanapiga maximum currency.

Mfano: ukiwa huna EFD mshine
Hukumu kwenye sheria inasema ni kulupa fine sio chini ya currency 100 na sio zaidi ya currency 150 na kila currency moja thamani yake ni 20000
Maana yake :150 * 20000=3000000
Sasa sijui kwann hawatumii currency ndogo kama 100,120,130.

Naichukia hii serikali kandamizi sanaaa wasipobadili hizi taratibu za ulipaji kodi wataisoma namba 2020!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom