Furaha na bashasha hii ya wafanyakazi katika Mei mosi ya 2017 ni ya dhati!?

ikinyunyi

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,065
940
Nipo natazama ITV mubashara, naona baadhi ya wafanyakazi wanashangilia sana lkn wengne wanaonekana hawana shauku yoyote ila ni kama wamelazimishwa. Naomba mniondoe utata hapa, hivi ni kweli furaha na bashasha hii ninayoiona inatoka kwa dhati mioyoni mwao au hawana la kufanya ila imebidi wafanye kwa matakwa fulani fulani, nakaribisha maoni!
 
Hali yenyewe kwa sasa mbaya, baadhi ya wafanyakazi wana mashaka na kazi zao...wanawaza kuhusu maslahi yao yatazingatiwa na kupewa kipaumbele... Wengine wanatabasamu usoni, lakini moyoni hawako vizuri
 
Nipo natazama ITV mubashara, naona baadhi ya wafanyakazi wanashangilia sana lkn wengne wanaonekana hawana shauku yoyote ila ni kama wamelazimishwa. Naomba mniondoe utata hapa, hivi ni kweli furaha na bashasha hii ninayoiona inatoka kwa dhati mioyoni mwao au hawana la kufanya ila imebidi wafanye kwa matakwa fulani fulani, nakaribisha maoni!
Hao watakuwa hired. I m not sure they are really workers
 
Aiseee kwa hio ulidhani watazira na kugoma kuhudhuria maadhimisho? Kumbuka hapo kuna sekta binafsi pia.

Tabasamu la mtu halionyeshi uhalisia wa moyoni.
 
187b11f21556d20fb3401cfba97dc7b3.jpg

MFANYA KAZI BORA 2017

Nimeangalia TV zetu mwanzo hadi Mwisho mategemeo yangu nilitegemea kumuona mfanyakazi bora wa nchi hii kuwa ni mama alie kijijini

Nashangaa vyama vyote vya wafanyakazi havikuona umuhimu wa mkulima katika nchi hii

Nilitegemea kuona viongozi wa taasisi mbali mbali vikitaja nafasi ya mkulima

Mkulima ni mtumishi asie thaminiwa na wale anao watumikia

Naamin siku ya mfanyakazi ni siku ya kumtukuza mama aliepo kijijini....
 
Hao ni Wakulima na Kipekee wanayo Sikukuu yao ya Wakulima Nane nane Mkuu uko Nchi hii Tena hufanyika katika kila Kanda
 
Bima zao zinalatibiwa na taasisi gani? Kiinua mgongo anawalipa nani?
Je mazao yao nani anawapa fidia yanapo kosa soko ?
Nane nane au tisatisa inawasaidia nini wakulima wa nchi hii?
KILIMO ni Kazi sio sherehe ya mavuno lazima na Kazi ya KILIMO itajwe kwenye mei mosi
 
Back
Top Bottom