Furaha: Kusudi la maisha ya mwanadamu

Furaha: Kusudi la maisha ya mwanadamu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,432
Utahangaika kutafuta Mali na utajiri ili vikupatie furaha.
Utatafuta kazi inayolipa vizuri na iliyo na mazingira mazuri na rafiki ili upate furaha.
Utatafuta mwanaume au mwanamke mzuri kwa kadiri ya viwango vyako ili akupatie furaha.
Utatafuta watoto ili wakupatie furaha.
Kila afanyacho mwanadamu anatarajia kimfurahishe. Je ni nani anayefanya jambo LA kumchukiza mwenyewe?
Siku moja kundi la watu 500 walikua wamehudhuria Semina. Mara msemaji mkuu wa semina hiyo akaanza kumpa kila mtu puto (balloon), na kuwaambia kila mmoja aandike jina lake juu la puto alilopewa. Kisha maputo yote yakakusanywa na kuwekwa kwenye chumba kimoja.Kisha watu wote wakaambiwa waingie kwenye chumba hicho na kila mmoja atafute puto lenye jina lake ndani ya dakika 5. Kila mmoja akaanza kuhangaika huku na kule akitafuta puto lake bila mafanikio, na chumba chote kikawa na fujo tupu.Baada ya dakika 5 kwisha, hakuna hata mmoja aliyekua amefanikiwa kupata puto lake. Ndipo msemaji akawaambia basi kila mmoja achukue puto lolote tu na ampe mtu ambaye jina lake limeandikwa kwenye puto hilo. Ndani ya dakika chache kila mmoja akawa ameshapata puto lake.Ndipo msemaji mkuu akasema: "Hii inatokea kwenye maisha yetu kila siku. Kila mtu anahangaika kutafuta furaha yake huku na kule, bila kujua ilipo. Furaha yako ipo kwenye Furaha za watu wengine. Wape furaha watu wanaokuzunguka;nawe utapata Furaha yako. Na hilo ndio lengo kuu la maisha ya Mwanadamu
 
Umetisha sana Bujibuji nimekukubali nampenda yule furaha yake furaha yangu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom