Hardbody
JF-Expert Member
- Jan 25, 2017
- 3,551
- 3,807
Hivi hiki chama ndio anatoka malema cyo?View attachment 1107494
Kiongozi wa Upinzani rasmi Afrika kusini Mmusi Maimane.
Uchaguzi wa Afrika kusini umeisha juma kadhaa zilizopita kwa chama cha ANC kuibuka mshindi ingawa kwa asilimia pungufu tokea uhuru wa watu weusi mwaka 1994. Uchaguzi huu tuliona vyama vya upinzani vikiongeza wabunge huku ANC ikipoteza viti zaidi ya 20. Na kubwa kabisa ni mikakati ambayo vyama vya upinzani Afrika kusini vilifanya ndio ilipelekea mafanikio haya na baadhi ya mafunzo wanaowapa wapinzani wa Tanzania ni kama yafuatayo.
1.Uhalisia wa malengo
Vyama vya upinzani Afrika kusini vinafahamu fika kuwa ANC ni zaidi ya chama dola bali DINI kabisa maana kuna watu wanakiona kama nembo ya ukombozi wa muafrika hivyo huwaambii kitu kuhusu ANC hivyo kuwachomoa huko inahitaji nguvu kubwa sana hivyo wana malengo ya "taratibu" yaani wanachagua Mikoa ambayo wanataka kuikomboa moja baada ya jingine hivyo wanawekeza nguvu maeneo hayo tu ili vyama vyao vizidi kukua kuliko kujikita kitaifa tu ambako inahitaji rasilimali nyingi na nguvu kazi ambayo kwa vyama vidogo ni ngumu kupambana na ANC. Mfano chama kikuu cha upinzani DA kiliweka malengo makuu matatu kuutetea "MKOA'' wa western cape na kushusha kura za ANC MKOA wa Gauteng na mkoa mwingine mmoja.
Hivyo rasilimali zote na nguvu kazi iliwekezwa maeneo hayo matatu hivyo wameweza kuyafikia na ndio maana wamekubali matokeo ila kama wangekuwa na malengo ya kukomboa mikoa yote 9 wangekuta hawapati hata mmoja sababu bado hawana rasilimali watu na pesa kulinganisha na ANC.
2. Uandaji Ilani
Hapa nimeambatanisha ilani ya chama cha DA ambacho kimetengeneza ilani yenye taarifa za undani zaidi jinsi ya kutekeleza ilani. Yaani wanaelezea kwa undani kabisa pesa fulani itapatikana wapi kwa kutumia data zilizopo na makadirio hivyo kuonyesha kweli wanauwezo wa kutekeleza walioahidi sio tu kusema kwenye ilani kuwa tutapunguza matumizi ya serikali bila kueleza shingapi zimetumika na wwe utapunguza kwenye maeneo gani na uweke tarakimu kabisa. Hii itaweza kushawishi mpiga kura kuwa unakielewa unachokiongelea kuliko maneno matupu.
3. Kujikita kwenye mafanikio ya chama sio udhaifu wa serikali.
Nilichojifunza kwa kupitia ilani ya chama kikuu cha upinzani DA ni jinsi walivyoandaa ilani zao kujikita zaidi kwenye mafanikio waliyopata majimbo/halmashauri zilizowachagua kwenye chaguzi zilizopita. Mfano ukiweka ahadi ya Elimu bure basi onesha mfano kwenye majimbo/halmashauri zinayoongozwa na upinzani jinsi ambavyo mmetatua shida ya gharama kwenye Elimu. Hii itawafanya waone mnaweza tekeleza mlichoahidi sababu majimbo mnayoongoza mmefanikiwa sio unaahidi maji wakati hakuna jimbo la upinzani lenye maji ya uhakika.
4.Kujikita kwenye kurejesha majimbo wanayoongoza(Retention).
Shida moja niliiona kwenye uchaguzi wa 2015 Tanzania Bara ni upinzani kuongeza majimbo mengi mapya lakini vilevile kupoteza majimbo mengi waliokuwa wanatawala mfano huko kanda ya ziwa walipoteza zaidi ya majimbo 90% waliokamata ila wakapata zaidi ya majimbo 5 mapya!!! Sasa hii haifai kwa upinzani unaotaka kukuaa. Nguvu kubwa iwekezwe kwenye kuimarisha chama kwenye majimbo ulionayo ili yasirudi chama tawala alafu uanze kazi upya ni bora uwe na majimbo 10 ambayo yatakuchagua milele kuliko kupata majimbo 5 mapya na kupoteza 5 uliyokuwa nayo unazidi kukiua chama maana yakirudi chama tawala huwezi washawishi wengine wakuchague ilihali majimbo uliyoongoza wamekukataa. Hili lifanyike kwa kuwekeza hata pesa za chama kwenye miradi ya Maendeleo kma elimu,afya,maji,ajira hapo majimbo hayawezi rudi chama tawala hata siku moja hivyo kujenga ngoma imara za upinzani kama walivyofanya DA huko western Cape ambako ANC ni chama cha upinzani kwa miongo kadhaa sasa.
Cc: Salary Slip chige kabombe Malcom Lumumba