Funzo kutoka Kenya: Katiba mpya au Tume huru sio suluhu ya uchaguzi wa Amani!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Nitoe pole kwa familia ya mkuu wa ICT wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa msiba wa kusikitisha na ulioacha majonzi.

Kabla ya kuwa na katiba mpya wapinzani na pengine wengi wa wananchi wa Kenya waliaminishwa kuwa majanga mengi yanayohusu uchaguzi,amani na hali ya ujumla ya uendeshaji wa Taifa hilo hayakwenda vyema kwa kuwa hakuna katiba nzuri inayoweza kusimamia hali ya mambo.

Pia kulikuwa na kilio kikubwa juu ya uhuru wa Tume ya uchaguzi ,kwa wanaokumbuka kuna mtu maarufu hapo Kenya ukiongelea Tume Huru ya Uchaguzi akiitwa Kivuitu..huyu alitangaza matokeo Ikulu na Rais Kibaki akaapishwa hapo hapo na baada ya hapo alikwea pipa kuelekea South Africa.Kipindi hiki Tume iliitwa sio huru na ikapelekea mfumo wa Tume unadilishwe kwa sababu hii na pia kwa sababu ya katiba mpya ya Kenya.

Kwa ufupi kilio hiki au imani potofu "myth" hii sio jambo la kipekee kwa nchi ya Kenya bali ni jambo au imani ya wanasiasa wengi barani Africa.

Kila uchao ni lazima usikie kilio cha Tume kutokuwa huru au katiba kuwa mbovu...

Haijawahi kuwekwa kiwango cha uhuru wa Tume duniani kote...yaani kwa wanasiasa kila wakishindwa lazima utalisikia hili neno.

Tukirejea hapa nchini kumekuwa na kilio cha namna hii kwa miongo kadhaa sasa kiasi cha kumfanya JK angalau kujaribu kuwaletea hilo jinamizi linaloitwa katiba mpya ingawa palitokea mkwamo kwa kuwa suala hilo lilipigiwa kelele na wanasiasa,kuratibiwa na wanasiasa na hatimaye kuharibiwa na wanasiasa.

Kipo kilio cha mara kwa mara cha kudai Tume huru ingawa hakuna ushahidi usio na Shaka juu ya Tume kukosa uhuru.

Nadhani kwa yanayoendelea Kenya ni wazi kuwa hakutawahi kutokee usalama katika uchaguzi hata kama Tume ya uchaguzi itakuwa chini ya malaika na Katiba ikawa kama kitabu cha msahafu au bibilia.

Kwa maoni yangu sioni haja ya kuendelea na mchakato wa katiba mpya uliokwama kwani ni upotevu wa fedha unaolenga kutafuta au kufikia matarajio yasio na mashiko.

Yaani Katiba mpya au Tume huru sio suluhisho la figisufigisu za uchaguzi...hizi zitakuwepo tu.

RIP MJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI KENYA.
 
Tutengeneze katiba nzuri na tume huru ya uchaguzi halafu hayo mengine tutajua mbele ya safari, kwani mnaogopa nini
 
Unapopinga uhuru wa tume huku ukionyesha kuwa hii iliyopo ni huru basi anzisha vuguvugu la kuondoa huo uhuru ulioko kwenye tume! Maana kwako wewe tume huru Ni hatari! Tume huru huko kenya ndiyo iliyomuua huyo nani sijui!! Mwambie mwenyekiti wenu wa chama amteue polepole kuwa mwenyekiti wa tume! Si mwenyekiti wa ccm ndiye mteuzi wa tume? Kwa nini msimshawishi ahamishie Nec pale lumumba?si kuna kile chumba mlikuwa mnakifanya store zamani?hamishieni ofisi za Nec hapo!Nalaabuk
 
Kiuhalisia mimi sidhani kama kunaweza kuwepo na tume huru ya uchaguzi. Hiyo ni kwa sababu sidhani kama watu wanaoiunda hiyo tume wanaweza wasiwe kabisa na upendeleo wa vyama.

Naamini mioyoni mwao lazima tu watakuwa wanapendelea upande flani.

Lakini, licha ya kwamba tume ya uchaguzi ya Tanzania si huru [kwa sababu inaundwa na rais aliyeko madarakani na mpaka sasa wote wamekuwa ni wenyeviti wa CCM], mimi naamini kuwa uwepo si mwarobaini wa matatizo yetu ya chaguzi.

Kwa Tanzania bara, naamini kuwa hata ingekuwepo hiyo tume huru, CCM bado ingekuwa inashinda tu kwa sababu vyama vya upinzani havijielewi na ni dhaifu sana. Pia havina dira wala mwelekeo wowote ule. Mtu hujui hata vinasimamia nini.
 
Miye naunga mkono uwepo wa Katiba mpya,tume huru,mamlaka ya Bunge kuidhinisha uteuzi wa Jaji Mkuu,Spika wa Bunge kuwa sio mwanasiasa bali mwajiriwa anaeomba hiyo nafasi na kufanyia vetting na Bunge,Bunge kuuhusika katika upatikanaji wa A.G,DPP,DCI!
Na pia kupunguza madaraka ya rais ya uteuzi kwa kuyagawa madaraka hayo kwa Bunge!

Tupate kwanza Katiba mpya,hayo mengine tutayatatatua mbeleni!
 
Nitoe pole kwa familia ya mkuu wa ICT wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa msiba wa kusikitisha na ulioacha majonzi.

Kabla ya kuwa na katiba mpya wapinzani na pengine wengi wa wananchi wa Kenya waliaminishwa kuwa majanga mengi yanayohusu uchaguzi,amani na hali ya ujumla ya uendeshaji wa Taifa hilo hayakwenda vyema kwa kuwa hakuna katiba nzuri inayoweza kusimamia hali ya mambo.

Pia kulikuwa na kilio kikubwa juu ya uhuru wa Tume ya uchaguzi ,kwa wanaokumbuka kuna mtu maarufu hapo Kenya ukiongelea Tume Huru ya Uchaguzi akiitwa Kivuitu..huyu alitangaza matokeo Ikulu na Rais Kibaki akaapishwa hapo hapo na baada ya hapo alikwea pipa kuelekea South Africa.Kipindi hiki Tume iliitwa sio huru na ikapelekea mfumo wa Tume unadilishwe kwa sababu hii na pia kwa sababu ya katiba mpya ya Kenya.

Kwa ufupi kilio hiki au imani potofu "myth" hii sio jambo la kipekee kwa nchi ya Kenya bali ni jambo au imani ya wanasiasa wengi barani Africa.

Kila uchao ni lazima usikie kilio cha Tume kutokuwa huru au katiba kuwa mbovu...

Haijawahi kuwekwa kiwango cha uhuru wa Tume duniani kote...yaani kwa wanasiasa kila wakishindwa lazima utalisikia hili neno.

Tukirejea hapa nchini kumekuwa na kilio cha namna hii kwa miongo kadhaa sasa kiasi cha kumfanya JK angalau kujaribu kuwaletea hilo jinamizi linaloitwa katiba mpya ingawa palitokea mkwamo kwa kuwa suala hilo lilipigiwa kelele na wanasiasa,kuratibiwa na wanasiasa na hatimaye kuharibiwa na wanasiasa.

Kipo kilio cha mara kwa mara cha kudai Tume huru ingawa hakuna ushahidi usio na Shaka juu ya Tume kukosa uhuru.

Nadhani kwa yanayoendelea Kenya ni wazi kuwa hakutawahi kutokee usalama katika uchaguzi hata kama Tume ya uchaguzi itakuwa chini ya malaika na Katiba ikawa kama kitabu cha msahafu au bibilia.

Kwa maoni yangu sioni haja ya kuendelea na mchakato wa katiba mpya uliokwama kwani ni upotevu wa fedha unaolenga kutafuta au kufikia matarajio yasio na mashiko.

Yaani Katiba mpya au Tume huru sio suluhisho la figisufigisu za uchaguzi...hizi zitakuwepo tu.

RIP MJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI KENYA.
Ulikuwa sahihi kujiita jingalao. Unalitendea haki jina lako. Kuna wakati hata wakubwa wenu huwa wanashangaa jinsi mawazo yenu yalivyo! Nakumbuka Kiongozi mmoja wa juu kabisa aliwahi kunieleza kwamba, kuna wakati huwa haamini kama hawa Vijana pro ccm mitandaoni huwa wanaongea vitu wakiwa serious au wapo katika kutafuta mkate wao!
Alidai kama huwa mpo serious basi moja ya dhambi kubwa iliyofanywa na chama chetu ni kuwafanya Vijana kuwa wapumbavu!
Hii post yako inaongeza ushahidi wa maoni yake!
Nadhani hata Mzee Ben huwa anarefer kwenu kabla hajasema Watanzania ni wapumbavu..
 
Mada ya hovyo kabisa. Tena mada ya mtu 'mpumbavu'. Unaongea upuuzi kwa kuwa unanufaika na mfumo uliopo.

Tangu lini upotofu ukatumika kutengeneza ukamilifu? Tuseme leo hii kwamba adhabu za makosa ya barabarani ziondolewe kabisa kwa kuwa hazijawahi kumaliza ajali?

Anyway, angalau umeonesha kuwa unafahamu kuwa tume iliyopo sio huru.
 
tangu siku ile prof kabudi alivyofafanua kuna nchi hazina sio tu katiba mpya bali hazina katiba kabisa na maisha yao yanakwenda mfano uingereza na SA nilijufunza katiba sio mwarobaini wa matatizo ya mtanzania.
Hoja mufilisi kabisa...

Sisi tumeamua kufata mfumo wa kuwa na Katiba na kwa sasa inaonekana wazi tuna hitaji kubwa la kuwa na Katiba Mpya ambayo ndani yake ita-stipulate uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi..

Unajisikiaje kwa mfano ukisikia sehemu fulani mgombea huyu ndie alieshinda lakini kutokana na kutokuwa na Tume Huru ushindi wake akapokwa??

Sometimes u should make up your mind, kutufananisha sijui na SA na GB is absolutely not only rubbish but irrelevant..!!

Wao tawala zao ndio zilianza hivyo kwa kutokuwa na Katiba (kama ni kweli). Sisi Katiba kwetu ndio kila kitu.
 
Inaonekana hujui chochote kuhusu Uhuru wa tume za uchaguzi...kama ni Uhuru wa tume Kenya wanajitahidi ukilinganisha na Nchi nyingine za East Africa... Waulizeni KANU watakuwa na majibu sahihi.. Nadhani kwetu sisi Waheshimiwa kama Mzee Jecha na Jaji Lubuva wanaelewa nachokisema!
Ghana ni mfano mzuri wa kuwa na tume huru ya uchaguzi.. Tume ikiwa huru, vyama tawala vikaondoa hofu ya kupisha vyama vinavyoshinda uchaguzi kwa Amani, daima maendeleo huja kwa kasi sana kwani agenda huwa ni Taifa kwanza badala ya chama kwanza ili usiondolewe madarakani ..
Ukishindwa kuleta maendeleo ktk miaka 50 na bado unalazimisha uwepo, usitarajie utakuwa na mawazo ya kusaidia Taifa. Daima utawaza ufanye nini kuwaangamiza wapinzani wako..
Kinachotokea sasa hapa kwetu ni kielelezo tosha!
 
Kwani huyo mtaalam wa IT Kenya ameuwawa kwa sababu za katiba mpya? Labda ameshukiwa kufanya rigging kwa ajili ya upande flani.Na kama kweli wamemprove kuwa na mipango ya kutotenda haki,basi kifo ni halali yake kama hakuna namna nyingine za kumzuia.Funzo ni kuwa Haki ina gharama kubwa.
 
Subiri siku Mwenye tume abadilishe gia angani kwa kuweka MTU wake ndo utajua kwanini taasisi ikiwa huru faida yake ni nini; kwa jamii ya waKenya ndo wangekua na tume kama yetu nchi yao ingekua zaidi ya Somalia.

Sema watanzania walio wengi ata kusoma na kuandika kwenyewe hawajui sasa hizo haki zao ndo usiseme; sisi tunaoishi mipaki na waKenya tunawaonea wivu sana kuhusu kujitambua.
 
tangu siku ile prof kabudi alivyofafanua kuna nchi hazina sio tu katiba mpya bali hazina katiba kabisa na maisha yao yanakwenda mfano uingereza na SA nilijufunza katiba sio mwarobaini wa matatizo ya mtanzania.

Hawana katiba iliyoandikwa kama kitabu kimoja ila katiba wanazo kwa namna yake - documents nyingi zilizotawanyika. Labda kwanza uangalie maana ya katiba ndio utaelewa.
 
tangu siku ile prof kabudi alivyofafanua kuna nchi hazina sio tu katiba mpya bali hazina katiba kabisa na maisha yao yanakwenda mfano uingereza na SA nilijufunza katiba sio mwarobaini wa matatizo ya mtanzania.
SA INA KATIBA ONE OF THE BEST IN THE WORLD,KUTUAMBIA HAINA KATIBA HUO NI UONGO MKUBWA,NA ON TOP OF THAT HII NCHI (SA) NI NCHI INAYOONGOZWA KIKATIBA ,sio ya kwetu ambayo inatumia mfumo wa executive madaraka yote yamelala na our no 1,usipotoshe watu plz
 
Tutengeneze katiba nzuri na tume huru ya uchaguzi halafu hayo mengine tutajua mbele ya safari, kwani mnaogopa nini
Hata mpewe katiba ya marekani au India mtalalamika tu nyie.Tunakwenda hivi hivi,mlipewa nafasi mkaichezea kwa kususa.Kwa sasa kipaumbele ni viwanda na miundombinu sio katiba
 
SA INA KATIBA ONE OF THE BEST IN THE WORLD,KUTUAMBIA HAINA KATIBA HUO NI UONGO MKUBWA,NA ON TOP OF THAT HII NCHI (SA) NI NCHI INAYOONGOZWA KIKATIBA ,sio ya kwetu ambayo inatumia mfumo wa executive madaraka yote yamelala na our no 1,usipotoshe watu plz
new zealand
israel
uk
canada

democratic countries bila katiba.
hiyo SA nitakuwa nimechanganya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom