Fungu la kumi inayojulikana kama zaka ni asilimia kumi (10%) ya mapata yako. Tuseme wewe ni mwajiriwa, unalipwa mshara mwisho wa mwezi, asilimia 10 ya mshahara wako unautoa kama zaka. Na pia hutakiwi kutoa zaka peke yake, zaka inatakiwa iambatane na sadaka.
Ndugu zangu, kuna baraka sana unapokua muaminifu kurudisha zaka kamili na sadaka (kwa wale wanaofanya hivi naamini watashuhudia). Tujitahidini sana kurudisha zaka na sadaka.
Malaki 3:10-12
[10]Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
[11]Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
[12]Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.