Maserati
JF-Expert Member
- Jun 15, 2014
- 11,602
- 20,098
Baada ya kupata ban nikaimiss jf Mara 100 ya ninavyoipenda.
Wadogo kwa wahenga,habari zenu wana Jamvi,wana Jf,wana MMU.
Leo nawaletea kisa kimoja hivi cha kusisimua,nasema cha kusisimua kwa sababu mie kimenisisimua sana ikafika sehemu Nina comment,wadada au Hata pengine wakaka lakini fungu la kukosa tunalitaka sie wenyewe.
Jane ana mpenzi wake Tariq,Jane anampenda sana Tariq. Kwa muda wa miaka mi3 Jane amekuwa akimuonyesha mapenzi mazito sana,kumjali na kumsaidia katika mambo mbalimbali yaliyo mfika. Tariq alimpenda Jane lakini si Sawa na ambavyo Jane alimpenda na kujitoa kwa bwana huyo. Jane ilikuwa anaulizia sana mustakabari wa penzi lao,hasa ukizingatia tofauti za kidini walizo nazo,lakini Tariq akamwambia usijali Mimi baba Ndio muislamu na mama yangu ni mkristo,so naweza kubadilisha dini. Jambo hili likamfanya Jane akafurahi na kuona malengo ya mapenzi yao kwenda mbali zaidi. Jane akaenda kinyume na taratibu za kibantu/kiafrica akamtambulisha Tariq kwao pasipo yeye kutambulishwa kwa mwanaume huyo. Baba Jane hakupendezwa na jambo hilo na hakusita kumuuliza mwanae,mmeenda kwao? Jane akajibu hapana,baba mtu akafoka foka pale lakini Jane hakujali. Mapenzi yalimpa upofu na kumfanya asifikilie jambo lolote lile.
Baada ya miezi miwili toka Jane ampeleke Tariq kwao mambo yakabadilika,kulingana na maelezo ya Jane ni kwamba aliomba akatambulishwe na yeye kwa kina Tariq,Ndipo mwanaume yule akageuka mbogo na kuanzia visa. Siku ya siku Jane akafunga safari mpaka Tanga,kutokana na story alizokuwa akipewa na bwana ake mwanzoni mwa penzi lao zilimfikisha kwa kina Tariq. Hamadi!!!! Tariq ameoa na ana mke tena mjamzito.
Jane akavunjika moyo,akarudi dar na kumuuliza Tariq kile alichokiona,akaambulia kupigwa na kutukanwa na mapenzi yakafia Hapo. Jane akaumia moyoni mwake akaielezea familia yake na kila mmoja alimchukia sana kijana yule. Jane akashindwa kuvumilia akataka kujiua kwa kujitundika, lakini alitokea msamalia mwema Steve akamuokoa. Steve aliumizwa na story ya Jane baada ya kumfikisha kwao toka eneo alilotaka kujitundika. Steve akaapa kuirudisha Furaha ya Jane,akimtazama Jane ni msichana mrembo sana,hakuna sababu ya kumuacha aumie na bila ya kujali historia yake akaanza kujiweka kwake taratibu. Akaanza kumtoa out,na kumpeleka vacation,Mara bagamoyo,Mara Zanzibar,kenya na sehemu mbalimbali za nchi na bara la Africa.
Jane akakubali kuanza mahusiano mapya na Steve. Akarejea katika hali yake ya zamani,Furaha na amani moyoni mwake. Baada ya miezi mitatu Steve akamtoa Jane out kupata chakula cha jioni,huko akamfanyia Jane suprise,akataka amvalishe Pete ya uchumba. Jane akakataa akidai ni mapema mno,na kama yuko tayari asubiri ifikie mwaka mmoja toka wajuane,na afanye tukio hilo mbele ya wazazi wa familia zote mbili. Steve kwa kishingo upande akakubali,lakini hakuridhika kabisa kwa sababu alimpenda sana Jane na hakutamani kuendelea kusubiri.
Baada ya mwaka mmoja kutimia,kama ambavyo Jane alitaka steve akaamua aandae sherehe amvalishe mapenzi wake Pete ya uchumba,lakini alivyomwambia Jane,bidada akaomba tarehe isogezwe mbele,akaanza visingizio hatimaye Steve akachoka na kuwashirikisha wazazi wa Jane. Wazazi wakakaongea nae akajitetea ana wasiwasi na woga,lakini hana hakika kama yupo tayari kwa tukio hilo. Wazazi wake wakashangaa sana lakini mwisho wa siku wakamuacha yeye mwenyewe aamue.
Hatimaye akakubali,mwaka Jana mwezi wa nane ikaandaliwa sherehe. Jane hakuna na amani,muda mwingi ilikuwa busy na simu yake. Steve akapiga goti na kuomba Jane aolewe nae,kimya. Steve akasema tena,kimya. Kila mtu akapigwa na butwaa. Sherehe ilifanyika kwa kina Jane,Steve akajaribu tena,Jane akasema hapana. Na kueleza jinsi gani hampendi na hamfurahii kuwa nae,machozi yakaanza kumtoka steve wa watu. Muda Huo Huo mlango ukagongwa kubishwa hodi,kufungua Tariq huyu hapa kajaa,Jane akatoka pale na kumkimbilia Tariq akamkumbatia na kutokomea.
Tariq alianza kumrubuni upya Jane baada ya kuona amezidi kunawili na kupendeza baada yakuachana nae. Tariq akamwambia aliachana na yule mwanamke,yupo single. So akatae Pete ya steve,yeye atamuoa mwezi unaofuatia,Jane akakolea penzi na hatimaye akakataa Pete ya uchumba. Wakaenda kupanga nyumba kigamboni,mwezi wa 12 Jane akapata ujauzito. Tariq akamuaga Jane anaenda Tanga kuongea na wazazi kumuhusu yeye. Week zikakatika,miezi ikapita Tariq hakurudi.
Mwaka 2017,
Baada ya mkasa ile Steve akaondoka Tz,kutokana na stress na aibu akaenda Ulaya. Huko akakutana na binti wa kitanzania,Lilian. Lilian ni engineer katika kampuni moja Kubwa hapa nchini. Kwa muda wa miezi mi3 wakawa wapenzi,hatimaye Steve akarudi Tanzania akawafahamisha familia yake na mpenzi wake. Siku ya siku JKN air port saa mbili usiku Steve akatua,akakutana na familia yake na mpenzi na mpenzi wake Lily,ambae akamtambulisha kwa wazazi wake na kumvalisha Pete ya uchumba on spot.
Hatimaye Jane akaenda kumuona Steve,Jane mjamzito,Amepalala,amekongoloka,amepoteza mvuto wote kwa kipigo na sasa ni zaidi ya miezi minne hajamuona na Wala hajui Tariq aliko,alikwenda tena tanga akaambiwa Tariq ameondoka na mke wake wapo mwanza. Mbaya zaidi Tanga hajulikani,kwao walishamtenga toka amdhalilishe steve,hawamsaidii na hawana Mawasiliano nae,kwa ufupi hawamtaki.
Steve akamuhurumia akaishia kumwambia pole,akampatia laki moja Ili afanye biashara ajikimu. Jane alilia sana,lakini haikusidia.
Hatimaye wiki iliyopita tumetoka kucheza kwaito Serena hotel,Steve marry Lilian. Sherehe ilifana sana.
Jane ana maisha magumu sana sana,lakini hana wa kumlaumu. Fungu la kukosa alilichagua mwenyewe.