Fundisho la maisha kutoka kwa Mwalimu na vita ya Idd Amin

Chifunanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
290
98
Nadhani wengi wetu tunaufahamu msemo huu wa "Sababu tunayo, Nia tunayo na Uwezo tunao". Ni ile speech ya Mwalimu Nyerere iliyotolewa wakati ule wa vita zidi ya Nduli.

Ila watu wengi hawajafikiria hii sentensi maana yake ni nini. Actually hii sentensi ina mambo matatu ambayo unahitaji ili kufanikiwa katika maisha. Na nadhani Mwalimu alisoma vitabu ya Nietzsche ndio akapata sentensi hiyo, inangawa Nietzsche hakusema jinsi Nyerere alivyosema:

Sababu tunayo (reason) - Ukitaka kufanya kitu chochote, kitu cha kwanza cha kujiuliza ni "Nafanya hivi kwa sababu gani?".....kama huna sababu basi usifanye.

Nia tunayo (will) - Lazima uwe na nia ya kufanya kitu, kama huna nia either hautafanya, au hautafanya vizuri.

Uweza tunao (power) - Saa nyingine unakuwa na sababu nzuri ya kufanya kitu...na unatamani ukifanye (nia), lakini uwezo au nguvu huna...unaishia kulalamika tu.

So, katika kufanya kitu chochote na kufanikiwa, lazima kuwe na Sababu, Nia na Uwezo......na ndio maana tulishinda vita dhidi ya NDULI.

Je, katika hii vita dhidi ya UFISADI, tujiulize leo, Sababu tunayo? Nia tunayo? Uwezo je?
 
Back
Top Bottom