Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,067
- 1,425
Ni yupi anayebisha ?
Siambi kujipa sifa, tena ambazo sinazo
Hunifuata sharafa, mahali penye mzozo
Wanijua makhalifa, nawachangia mawazo
Kunao wengi magwiji, tena watajika haswa
Kuna mafundi bobezi, vyuoni wamemaizi
Ila kwa wangu ujuzi, hawawezi piga mbizi
Kidogo labda miluzi, na hapo wamejihizi
Sisemi kuwadharau, ndimi kingi pande hizi
Nitajieni mfano, ili nimuangalie
Alienizidi ngano, nyuzi nizimfumie
Tena mlete watano, kimo mjichagulie
Ndimi fundi wa mahaba, karama Mola kanipa
Yalopita ni elimu, nanena yaliyo sasa
Na kabla ya kuhitimu, majaribu ni msasa
Hivi sasa ni Mwalimu, nina kunga za kisasa
Ndimi fundi mahaba, karama Mola kanipa
Abuuabdillah ✍️