FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,063
- 40,724
Kuwa hai ni bahati kubwa sana, lakini kuwa kiumbe chenye akili kuliko viumbe vyote duniani ni bahati mara 10,000 zaidi! (Hongera!)
Hivyo mpaka hapo wewe ni unique kwa kiwango ambacho ubongo wako hauna uwezo wa kung'amua. Imethibitika kwamba dunia ni sawa na chembe ya vumbi kwenye bahari isiyo na mwisho, lakini vilevile uwezekano wa kukuta chembe nyingine ndani ya bahari hiyo yenye uwezo wa kutunza uhai ni mdogo karibia sawa na sifuri, Dunia ni ya kipekee sana na wewe uko ndani yake, entity ya kipekee kama wewe kuwa ndani ya sayari ya kipekee kama hii ni bahati mara trillioni zaidi! (Hongera!)
Chukua dakika chache kujiuliza swali moja la msingi na la kipekee mno, "Je, ni kwanini nataka kuishi?" Hapa watu tofauti wanaweza wakaja na majibu tofauti, mimi nahisi jibu utakalotoa pengine ni haya au baadhi ya haya:
1.) "Nataka kuendelea kuishi kwa sababu maisha ni matamu na nataka nifaidi maisha haya". Chakula ni kitamu na kila mtu hufanya kila awezalo ndani ya dunia hii ili aweze kupata chakula kilicho bora na kitamu kuliko vyote! Ngono ni tamu na kila mtu hufanya kila awezalo ndani ya dunia hii ili aweze kupata mpenzi alie bora na mtamu kuliko wote! (Hongera!)
2.) "Nataka niendelee kuishi kwa sababu nataka niwe maarufu na mwenye kupendwa na kuabudiwa na mashabiki wangu". Power and respect (nguvu na heshima) ni vitamu sana na kila mtu hufanya kila awezalo ndani ya Dunia hii ili aweze kupata 'nguvu' na 'heshima' iliyo bora na tamu kuliko zote! (Hongera!)
3.) Ongezea ya kwako (Umepewa ubongo). (Hongera!)
Cha ajabu na cha kushangaza, jibu lolote utakalo kuja nalo halitakuwa sahihi..,lakini the reverse will be correct. Tuchukulie jibu lako no.1, Unaweza ukafikiri unataka uishi ili ufaidi chakula, lakini ukweli ni kwamba unafaidi chakula ili uishi, period! tena chakula kinafanywa kiwe kitamu zaidi pale uwezekano wa kukusaidia kuishi unapokuwa mkubwa na pia chakula hicho hufanywa kiwe kichungu zaidi pale uwezekano wake wa kukuondolea uhai wako unapokua mkubwa zaidi.
Unaweza ukafikiri unataka uishi ili ufaidi ngono, lakini ukweli ni kwamba unafaidi ngono ili binadamu waendelee kuishi milele, period! Tena ngono hufanywa kuwa tamu zaidi pale uwezekano wa kusaidia binadamu kuendelea kuishi unapokuwa mkubwa na pia ngono hufanywa kuwa chungu zaidi pale uwezekano wa kusaidia binadamu kuendelea kuishi unapokuwa mdogo.
Dadavua jibu No.2 na mengine yote utakayokuja nayo kwa mtindo huu huu wa 'reverse thinking' na utastaajabika.
Sasa kumbe tunarudi pale pale, hatuishi ili tufaidi bali tunafaidi ili tuishi, sasa je, NI KWANINI TUNATAKA KUISHI?!
DON FRANCIS
============================================
Update: 14/07/2021