Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI.

Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)

Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.

Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.

Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.

Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.

Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.

Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9

Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.

Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow

Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006

Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.

Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
 
Asante JF kwa kutuhabarisha, Hongereni kamati ya PAC mapendekezo yenu. Kama mapendekezo yale yatatekelezwa kwa asilimia mia moja....Tanzania inaweza kurudi kwenye mstari ulionyooka na kujiendesha bila tatizo.
 
Naongelea uwasilishaji, si huo uchunguzi. Na pia tumesikia upande mmoja mpaka tungoje upande wa pili wanasemaje.

Mpaka sasa sijaona kilichowasilishwa ambacho hakijibiki.

Hahahahahaaaaa upo? Nakukumbuka sana ulivyokua Unakataaa na kuutetea huu wizi. Kazi unayo, maana suala sio kujibika suala ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu.
 

Attachments

  • 1417021127620.jpg
    1417021127620.jpg
    49 KB · Views: 234
CCM kwa ujumla wake ni janga kwa taifa letu. Tuanze kuwatoa huku serikali za mitaa! 2015 ni kuwapiga cha mbwa mwizi.

Na MKOMBOZI Bank ni MAGUMASHI. Wanauza hisa ili kutakatisha uwekezaji wa hao wezi na mafisadi akiwemo Kilaini na Nzigirwa. Na itakufa wakifilisiwa...

Unaposema Mkombozi wametakatisha fedha huoni kama na benki kuu nao wanahusika katika utakatishaji huo?
 
Mim nalia na viongozi wa dini "toa ndugu toa ndugu ulichonacho mungu anakuona mpaka moyoni mwako" ,sasa kweli amewaona ,vipi mlitoa fungu la kumi? Kwa hizo fedha za madafu mlizogawana kwenye viloba ,nchi hii itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno makubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Sio kupoteza malengo huu ni mjadala au unataka mjadala ugeuke kuwa circlejerk?.
ripoti haijataja katika hizo pesa kiasi seegani ni za umma na zipi ndo iptl walitakiwa kuchukua.hiyo maana yake cag hakufanya kazi inayotakiwa.ilitakiwa alete hesabu kwa mwenzi capacity charge wamelipa ngapi,ilitakiwa ngapi na overchanging ni ngapi,na iptl walipaswa kulipwa ngapi?


We kilaza umeambiwa mchakato mzima ni tapeli mtupu,documents Za kufoji etc. Pap/iptl haikutakiwa kulipwa chochote Kabla ya uamuzi wa court ya kimataifa iliyoshugulikia mgogoro huo.
 
tanzania imejaa vilaza wasiojua haki zao na ndo maana watu hawana uoga, aibu wala huruma ya kuchota pesa tani yao! sasa 1.6b zote mtu anapeleka wapi jamani! tusichokijua kuhusu mahitaji ya kibinadamu, tuna tumbo moja weka na matumbo ya mke na watoto say 4 matumbo plus you then 5 !, hawa watu watano wanahitaji nyumba moja, na gari moja tu! sasa mtu anaiba mabilioni ananunua magari sita, ekari 1000,nyumba tano anajenga kila mkoa! benki ana 10b za ufisadi , tusichokijua tuna vitu tunavyovitaka ila tusivyovihitaji! ukiwa na magari 6 mengine huyatumii na siku ukifa wanapoenda kukuzika wasindikizaji wanatumia magari yako ya wizi kwenye msafara wa kwenda kukulaza fisadi na wakirudi ndugu wanagawana hayo magari kila mmoja anachukua gari moja na kama una nyumba kumi nazo wanagawana moja moja, ukweli unasimama kuwa hukuhitaji magari 6 bali ulihitaji gari moja na nyumba moja tu!, na hivyo hukuwa na sababu ya kuiba mabilioni kununua vitu usivyohitaji! sifa tu zinatusumbua bongo na ni chanzo kikuu cha wizi wote tunaouona! tunataka kusifiwa kuwa na mali nyingi tusizozihitaji wala kuzitumia!


1.6B pesa kuchu sana mamaa, hukumsikia Chenge aliziita vijisenti? nadhani za RICHMONDI zilishaisha hivyo akahitaji kujiboost kidogo.

Hayo magorofa huko mbezi beach, ma-vogue hapo mtaani unafikiri yananunuliwa na mishahara?

mshahara wa waziri inabidi asiule miaka si chini ya mi 3 ili kulipia vogue moja tu hapo CMC.

Sasa kwa akili yakako unafikiria wananunua kwa kutumia nini?miradi ya kuku? WIZI.
 
aibu mahakama kuu kuweka katazo kuzuia kashfa
ya kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa zaidi ya
mabilioni kwenye akaunti ya Tegeta
Escrow.
 
Habinder Singh seth wewe Ni kiboko umeangusha serikali tena Kama ulivyoangusha Kenya. Wewe Ni level za kimataifa.
 
Nimesoma ripoti yote, pamoja na uzuri wake sijaona mahali kilipojumuishwa kielelezo cha utetezi wa BoT ambacho kiligusia uhusika wa ofisi kuu
Anyway angalao kuna debate kuhusu hizo pesa!
 
Mkombozi bank walikuwa wanajua hizi ni fedha za deal; no question about it. Stanbic bank walikuwa wanajua hizi ni fedha za deal, no question about it. Ila walijua na pengine wameshagawa fedha kwa mtindo huo mara nyingi, kuwa hakuna sheria yoyote itakayofanya kazi. Tatizo la nchi yetu si kutunga sheria nyingi zaidi na kuongeza vyombo vya utekelezajia. Tatizo letu ni kuwa taasisi ambazo zinatakiwa kuzitumia sheria hawazitumii na hivyo inaonekana kama vile hazitoshi. Tatizo liko kwenye enforcement ya sheria. Waziri mkuu kila siku ilikuwa ni kudanganya kuwa hiyo ni hela ya binafsi akijua wazi kuwa si kweli. Na aende tuuuuu!! Useless.
 
Back
Top Bottom