Hongera sana mkuu, ni opportunity nzuri sana kwako hiyo mkuu, na nina uhakika kuna vitu utagain kutokana na hiyo interview, bila kujali matokeo yatakavyokua. Ushauri wangu;
1.Soma sana kuhusu the Scholarship scheme itself; ilianza mwaka gani? Ina malengo gani? Mpaka sasa mafanikio yake ni yapi? (Hizi taarifa utazipata from the scholarship's website na/au newsletters au reports).
2.Kumbuka zile essays zako wakati una apply (i hope unazo umezihifadhi somewhere) zipitie na uhakikishe maswali yao kwa interview utakavyojibu yapo CONSISTENT na ulichoandika kwenye essays zako.
3.Soma sana kuhusu kozi na vyuo ambavyo umeombea scholarship... Unazijua modules na contents za kozi yako unayotaka kusoma? Unajua historia ya chuo unachotaka kwenda kusoma? Mambo gani makubwa na/au mazuri chuo chako kimeyafanya kuhusiana na field unayotaka kwenda kusoma (discoveries,research, famous people who studied there,historical facts). Hii iunganishe na "Kwa nini umechagua kozi na chuo ulichochagua"?
4.Kwa nini Marekani?
5.unachotaka kwenda kusoma kitakusaidiaje katika kazi/shughuli zako za sasa? Na pia kitakusaidiaje katika mipango yako ya baadae kwenye taaluma yako? Pia, skills na knowledge utakazozipata zitaisaidiaje taasisi unayofanyia kazi na/au nchi yako?
6. Unachotaka kwenda kusoma kinaendana vipi na mipango ya nchi yako? (Eg policy plans, achievements to certain local and/or international targets)
7.mambo gani umewahi kufanya so far kusaidia maendeleo ya jamii yako? Au kusaidia kutatua changamoto fulani inayoikabili jamii yako?
8.Una uzoefu gani katika masuala ya uongozi? (Hapa jikite zaidi katika kuelezea namna ulivyotumia nafasi zako za kiuongozi kutatua changamoto fulani na matokeo uliyopata)
9.What do you bring to the Scholarship scheme? Hapa ujiandae kujibu ni vitu gani fullbright scholarship watafaidika kwa kukuchagua wewe (eg sharing of unique Tanzanian culture and teaching swahili language to fellow fullbrighters, i will use my extensive presence in social media to promote Fullbright scholarships and encourage my followers to apply, etc, etc).
10. How can the impact that you will bring to your career/your insitution/your country post graduation be measured?
11. La mwisho, japokua kiumuhimu hili ndo ilibidi liwe la kwanza... Be as specific as possible to the minute details unapokua unajibu maswali, and hit the point directly bila kuzunguka sana; Pia usije ukatoa majibu very general au non specific... hapo utafeli. Eg unaulizwa how will this scholarship help ur career? Hapo inabidi ujibu specifically skills na knoweldge gani utakazogain kwenye masomo yako,na zitakusaidiaje kwenye career yako; na sio ujibu kiujumla jumla tu.
Kiufupi ni hayo ambayo nimekumbuka haraka haraka; nikipata points zaidi nitaongezea.
ALL THE BEST.
Bradson