From CTO's Desk - Monitor Usage, save your Voucher

Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,204
5,523
Vema, kuna wandugu katika uzi huu hao chini wamelalamikia tatizo la mitandao kukutaarifu baada ya kuwa imekula vocha zako zote.
Huu ni wizi na nimeshaongea na hawa wandugu lakini inaonekana hata wao hawajui vema cha kufanya. Kwa kuwa Mimi ni mwanateknolojia badala ya kulalama nikaanza kusaka suluhisho.
Natumia Linux kwa hiyo solution niliyotafuta kwa ajili ya suluhu ni Linux pia, kuwa wazi zaidi ni Debian. Lakini unaweza kupika vyanzo (compile sources) mwenyewe ktk Linux yeyote.

Ni programu inaitwa "Download Monitor". Nukuu ya ufupisho wa utambulisho wake ni hii:
"Monitors the amount of data downloaded and uploaded over the network over time. Displays this data in easy to read graphs. Allows a usage quota to be set and warns when the quota is exceeded or soon to be exceeded. Useful for people on capped data plans."

MAMBO INAYOKUSAIDIA
- Kukupa idadi ya Matumizi ya data zako zilizopandishwa/kushushwa mtandaoni
-Inakuchorea grafu zinazoonesha matumizi ya saa, siku mwezi n.k.
- Inakuonya pindi unapovuka mwisho wa matumizi uliojipangia

MATUMIZI NA FAIDA ZAKE
Ukiisha kuiweka ktk mashine yako, ianzishe na badili mpango (Edit->Preferences)
Andika mpango wa mtumizi yako. Mfano kama matumizi yako ni 50Mb Jaza
Upload 0GiB----50MiB
Download 0GiB---50MiB
Total Quota 0GiB---50MiB

Hi itakusaidi ukinogewa na Internet ukafika kiwango hich, yaani bundle yako imeisha itakupa onyo. Disconnect Modem yako papo hapo na ununue bundle nyingine.

NAIWEKAJE?
Ingia kiunga hiki: https://launchpad.net/download-monitor

Kama unatumia Linux familia ya Debian (Mint, Ubuntu, Debian kwa uchache) Pakua faili linaloishia na .deb. Ukimaliza piga kidoko-mbili (double click) kwenye faili hilo na ufuate maelekezo. Kwa wale wa familia zingine, pakua faili linaloishia na .tar.gz. Kongoa (extract) mafaili yote katika kabrasha moja na Uyapike mwenyewe. Sitaweka hatua hizo labda kama kuna mtu atazihitaji.

Lakini kwa watumiaji wa ubuntu ni rahisi zaidi maana ipo tayari katika bohari (repository) zao. Kuweka chapa amri hii
sudo apt-get install download-monitor

Furahia!
BH,
CTO - Hosanna Higher TechnologiesKwa maelezo zaidi tembelea mtandao wa programu hii: https://launchpad.net/download-monitor

Kiunga chenye malalamiko: https://www.jamiiforums.com/habari-...anzania-nchi-ya-ajabu-sana-2.html#post5152839
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom