From China With Fake Love

From China With Fake Love

streat Anthem

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
395
Reaction score
476
Wahenga walisema ukipenda boga, penda na ua lake. Kiukweli wahenga waliona kitu katika upendo ambacho kilikuwa hakiendi sawa. Na baadhi ilikuwa ni mtu kumpenda mtu kwa sababu ya kitu flani na kile kitu kikiondoka Upendo unakosa maana.

Ama niseme mtu alikua anapenda nusu nusu na kujikuta anachagua vya kupenda, zile sababu zinazoleta sababu ya kupendwa zisipokuwepo Nusu nyingine ya Chuki inachukua nafasi.

China ni nchi ambayo inapatikana katika bara la Asia. Ni nchi ambayo inazidi kuendelea kwa kasi katika kila nyanja za kimaisha. Na iyo ni kutokana na uzalendo wa watu wao kufanya kazi usiku na mchana na Uongozi mzuri toka kwa viongozi wao.

Kipindi cha nyuma Tanzania na China zilikua ni nchi zilizokuwa na urafiki mkubwa sana (labda kutokana na sera ya Ujamaa), China ilijotolea kwa hali na mali kuhakikisha Tanzania inaendelea. Kuanzia sekta ya viwanda kama Ujenzi wa kiwanda cha urafiki, sekta ya usafirishaji kama ujenzi wa reli ya Tazara na sekta nyingine mbalimbali kama elimu, afya na Ulinzi na Usalama.

Naamini kwa asilimia kubwa mahusiano mazuri yalijengwa kwa misingi ya kuheshimiana, kudumisha undugu hata kudhihirisha upendo baina ya nchi hizi mbili.

Naamini hata mikataba iliyofanywa kipindi cha nyuma ilikuwa ni ya kibinaadamu iliyojali masilahi ya pande zote. Bado nazidi kuamini uongozi mzuri wa J.K Nyerere na viongozi wa china walikuwa wanampango wa kufanya hizi nchi mbili kuwa ndugu wa damu bila kujali Rangi wala dini.

Nakuja kushangazwa na hali inayoendelea hivi sasa! China imebadilika kuliko nilivyotarajia. Ule upendo uliokuwepo umegeuka na kuwa wa kimaslahi zaidi. Urafiki umekuwa wa kinafki sana, yani hakuna tena undugu uliojengwa kipindi cha nyuma.

China ndio imekua nchi namba moja kuharibu mazingira ya Tanzania kwa bidhaa zao zisizojali afya zetu na mazingira yetu. Sio simu wala nini, karibia kila kitu ni feki na cha ovyo kabisa. Yani wanafanya nchi yetu kuwa jalala na shimo la takataka zao. Na nina mashaka na mchele wa plastiki utakuwa unatoka China.

China imekua ikiongoza kutengeneza barabara zilizo mbovu kiasi ambacho ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na wao kwa sababu ya miundo mbinu mibovu.

China wamewafanya dada zetu kuwa watu wa ajabu kupita mfano. Kuanzia nywele, makucha, madawa ya kunenepesha makalio na maziwa, Vipodozi vyenye kemikali nyingi na viungo vya bandia (sijui vya kufanyia nini). Mavazi kutoka China ni balaa tupu, sijui huwa wanatengeza kwa ajili ya nini, malighafi ni zetu lakini tunacholetewa ni zaidi ya dharau. Mikataba inayofanywa na Wachina ni ya kilaghai na faida kubwa wanachukua wao.

Kwenye viwanda na sehemu za kazi wanawatesa watanzania na wengine hupigwa kama watoto wadogo. Nilisikia kuwa wale wachina wanaofanya huku kazi wengi wao ni wafungwa, sina uhakika ila Kama ni kweli kwa nini watuletee waalifu ndo waje wajenge barabara zetu, wafanye biashara na kujenga viwanda. Ni wazi kuwa waalifu hao hawatafanya mambo kwa ufanisi.

China inashiriki kwenye wizi wa rasilimali zetu kama wanyama. Pia inashiriki kwenye biashara haramu ya pembe za ndovu na vifaru.

Ningependa kuwakumbusha Wachina wabadilike, wakumbuke enzi za kiongozi wao Mao aliekuwa ana upendo kwa nchi za kiafrika. China waache tabia kama za mataifa ya Magharibi, tabia za kinyonyaji na kukosa utu.
Mkipenda biashara na rasimali zetu, pendeni na afya, utu wetu na mazingira yetu.
 
Si ndio maana tumewaletea toothpick na simu za tecno jamani !
 
Tumia vya nchi nyingine achana na vya China...
Dunia inaenda kwa kasi sana, kila nchi inatafuta namna ya kuendelea
 
mbona vitu vizuri vya kichina vipo sema ni gharama that's y wabongo tunaletewa third class from China ila kama pesa inaruhusu zipo bidhaa za first class
 
Back
Top Bottom