Friikiki Bora Kuliko Zote

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,609
Reaction score
1,735
Je, ni ya:

1. Ronaldinho dhidi ya Uingereza
2. Stoichkov dhidi ya Ujerumani
3. Juninho...
4. Kalusha...
5. Okocha...
6. Bergkamp
7. Hooidjonk...
8. Pirlo
9. Companero...
10. De Piero...

?
 
Je, ni ya:

1. Ronaldinho dhidi ya Uingereza
2. Stoichkov dhidi ya Ujerumani
3. Juninho...
4. Kalusha...
5. Okocha...
6. Bergkamp
7. Hooidjonk...
8. Pirlo
9. Companero...
10. De Piero...

?


Free kick namba moja kwako itabakia kuwa namba 1 kwa watu wanaojuwa Soka.
Cafu alimfuata mtakatifu kisha akamwambia Cardoso Caraninho yaani ipige moja kwa moja...
Basi Mtakatifu akarudi nyuma na kisha akafuata maelekezo aliopatiwa na Evangelisco de Marcos Morares al maarufu kama Cafu.

Hakuna aliedhani, lakini alisikika mtangazaji aliekuwa anatangaza mechi hiyo kwa Lugha ya kilatini akilalamika kwa mayowe hata kabla mtakatifu hajaugusa mpira
''Goraaaaaazo, Goraaaaaazo il Santa Ronaldinho Gaucho pena Gorazooooo Gooooraaaaaaaaaaaaaazo''

Sasa Companero watafsirie washashi Gorazo ni nini...
 
freekick bora ni ya dinho dhidi ya england na mpiga free kick bora ni mtoto wa mzee penambuccano.
 
Mnacheza nyie, freekick kali kuliko zote ilipigwa na Roberto Carlos dhidi ya France kwenye mashindano (siyakumbuki jina) yaliyofanyika nchini France kabla ya 1998 World cup. Iangalieni kwenye Youtube halafu mtaniambia. CNN waliichagua kama "the greatest sporting play of the year" kwa mwaka 1998.
 


mkuu Roberto Carlos alibutua lishuti ila tu aliukata mpira.
yale yalikuwa mashindano ya mataifa manne kabla ya world cup.
Siku hizi hayapo mashindano yale.

Ile free kick ya Santa Gaucho hata wangekuwa makipa wanne wasingeidaka.
 
mkuu Roberto Carlos alibutua lishuti ila tu aliukata mpira.
yale yalikuwa mashindano ya mataifa manne kabla ya world cup.
Siku hizi hayapo mashindano yale.

Ile free kick ya Santa Gaucho hata wangekuwa makipa wanne wasingeidaka.

Ile ni fluke, hata Ronaldinho alikiri kuwa alibahatisha - hizo stori za Cafu na Gorazo ni geresha tu kama ile ya man of the match bila kuingia uwanjani!
 
Ile ni fluke, hata Ronaldinho alikiri kuwa alibahatisha - hizo stori za Cafu na Gorazo ni geresha tu kama ile ya man of the match bila kuingia uwanjani!


Nilikupa home work ya kuwaelezea wasomaji hapa nini maana ya neno Gorazo...
We Companero unaanzisha thread kisha unakuja kuponda majibu ya wachambuzi wa Soka tuliotukuka...
Acha habari zako hizo.

forza Santa Gaucho...
 
.....Ile free kick ya Santa Gaucho hata wangekuwa makipa wanne wasingeidaka.

Nimeipenda hii na kwa kweli sijawahi ona free kick ya aina hiyo katika maisha yangu. In fact hata David Seaman Kipa wa England alikiri kwamba kijana Dino amemtibulia historia yake na alistaafu soka kwa masikitiko makubwa.
 
mkuu Roberto Carlos alibutua lishuti ila tu aliukata mpira.
yale yalikuwa mashindano ya mataifa manne kabla ya world cup.
Siku hizi hayapo mashindano yale.

Ile free kick ya Santa Gaucho hata wangekuwa makipa wanne wasingeidaka.




Una maana gani kwamba alibutua? Ni kwamba alipiga kwa nguvu, tatizo liko wapi? Kwani freekick hazipigwi kwa nguvu? Halafu kuukata mpira si ni moja ya mbinu za kupiga freekick? Ulitaka apige dochi?

Na kwa kuongezea, freekick nyingi huwa zinapigwa kutumia upande wa ndani wa mguu lakini Roberto aliipiga kutumia upande wa nje wa mguu. That's what made it very special!
 
Ya Aurelio kwenye UEFA Liverpool vs R. Madrid (2009) kama sijakosea.
 
Dinho ile free kick kama vile ilikua imepagwa.. unless otherwise, it marked the histry!
 
Je, ni ya:

1. Ronaldinho dhidi ya Uingereza
2. Stoichkov dhidi ya Ujerumani
3. Juninho...
4. Kalusha...
5. Okocha...
6. Bergkamp
7. Hooidjonk...
8. Pirlo
9. Companero...
10. De Piero...

?

shunshuke nakamura/celtic vs man u
 
Muanzisha thread umefanya kosa kubwa sana kutoiweka freekick ya Roberto Carlos dhidi ya France 1997 kwenye kombe la nchi nne. Ukiangalia hata video yenyewe unamuona ball boy anajiandaa kuduck ule mpira(yalikuwa maelezo shuti la R Carlos ball boy huruhusiwi kulidaka acha mpira mpaka utulie wenyewe) na Barthez alijua umetoka ghafla ukaingia.

Miaka 13 baadaye yaani mwaka 2010 ulifanyika utafiti na wanafizikia wakafikia hitimisho kwamba ile haikuwa fluke kwani inaweza kurudiwa ikiwa mpira utapigwa kwa nguvu inayopaswa kwani utafuata trajectory ile ile. Kwa wale waliosoma Physics A level wataelewa zaidi maelezo yafuatayo.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…