Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 12,845
- 27,270
Theists Hi... 👋
Moja kwa moja kwenye mada. Sasa ni hivi.
Uchaguzi na Hiari ya kweli, ili viwe huru na vyenye uhuru kamili, ni lazima vifanyike bila shuruti, vitisho wala adhabu.
Ili chaguo liwe la kweli na la hiari, ni lazima lifanywe bila shinikizo, shuruti, vitisho au adhabu.
Watu wa dini wanaamini kwamba Mungu alitoa freewill ya mtu kuamua na kuchagua kutenda matendo atakayo kwa uhuru, hiari na maamuzi yake mwenyewe.
Halafu hapohapo wanakwambia endapo mtu ataamua kuchagua kutenda matendo mabaya kwa kutumia freewill ileile iliyowekwa. Basi atakutana na adhabu kali ya moto wa milele, Jehanam la moto🔥
Sasa hebu tujiulize hivi....👇
Kwa nini freewill haiwezi kuwepo bila mabaya kuwepo?
Je freewill inategemea mabaya yafanyike ndio ionekane ipo?
Kwa nini uwepo wa freewill utegemee uwepo mabaya?
Inashindikana vipi, freewill iwepo yenyewe tu, bila kutegemea uwepo wa mabaya?
Kuna haja na sababu ipi ya msingi mabaya yawepo na yafanyike kuonyesha eti kuna freewill?
Huyo Mungu alishindwaje kuumba Dunia yenye freewill pasipo mabaya?
Kama toka mwanzoni, Huyo Mungu alijua kabisa hapendi mabaya, Sasa
alishindwaje kuumba Dunia isiyo na mabaya? Alishindwaje kuumba binadamu wema tu, watakao mtii na kutenda mema siku zote na wakati wote?
Kama tangu mwanzo, Mungu alijua hapendi mabaya yafanyike, Kwa nini aliweka freewill ya mtu kuweza kuchagua kutenda mabaya?
Kama huyo Mungu ni upendo na anapenda watu watende matendo mema tu, Kwa nini aliruhusu mabaya yawepo na yafanyike kwa kigezo cha freewill?
Kama huyo Mungu anajua kabisa kuna freewill ya mtu kuweza kutenda mabaya, Kwa nini aje atoe adhabu wakati anajua kabisa aliweka freewill ya mtu kuchagua kutenda jambo lolote, ikiwemo mabaya kwa hiari?
Baada ya kujiuliza hivyo, Sasa tuangalie hii mifano hapa chini...👇
1-MFANO WA BABA NA MTOTO.
Tu assume, Baba ana mwanae ambaye ni mwanafunzi wa shule. Imefika siku ya jumatatu. Baba anamwambia mwanae hivi "Leo una uhuru na hiari ya kuchagua kwenda shule au kubaki nyumbanu" Lakini endapo nikirudi kutoka kazini nikakuta hujaenda shule, nita kutandika viboko vya hatari.
Huu tayari ni mtego sio uhuru wala
hiari huru.
Kwa scenario hii, Ni kweli mtoto amepewa uhuru, lakini sio uhuru ulio huru na wenye hiari huru. Kwa sababu endapo akichagua kubaki nyumbani asiende shuleni, Baba akirudi atamchapa viboko. Hivyo ili mtoto ajiepushe na adhabu hii, itambidi aende shuleni. Hivyo mtoto hatakuwa na uhuru wenye hiari huru.
2- MFANO WA MAJAMBAZI AU WEZI.
Wezi au majambazi wanavamia nyumbani kwako halafu wanakwambia una uhuru kuchagua, uwape pesa zako bila ya wao kukuua au wakuue kwanza kisha ndipo wachukue pesa zako.
Huu tayari ni mtego wala sio uhuru wenye hiari huru.
Kwa situation hii, ni kweli umepewa uhuru wa kuchagua. Lakini option ya pili uliyopewa itaondoa uhai wako. Kwa hiyo ili ukwepe kifo, itabidi ukubali option ya kwanza utoe pesa zako tu, ziende ubaki salama.
Baada ya kuangalia mifano hii, sasa turudi kwenye hii "freewill" inayodaiwa kuwekwa na Mungu.
Ikiwa matokeo ya mtu kuchagua kutenda mabaya ni hukumu ya milele na moto🔥 wa milele basi "freewill" inayohubiriwa ni sawa na hiari anayokupa jambazi anaposema, “Ni chaguo lako: pesa zako au uhai wako.” Uko huru kubaki na pesa zako, lakini utalipia kwa damu yako.
Kwa maana hiyo, ili mtu akwepe adhabu ya moto wa milele, hata kama freewill ya kutenda mabaya ipo, itambidi atende mema tu, ili akwepe kuingia motoni.
Na hii inakua sio freewill yenye hiari huru bali ni MTEGO wa kupeleka watu wakaungue moto, endapo watatenda mabaya.
Freewill inge make sense kama ingekuwa hivi:
Tenda mema au mabaya vyovyote sawa tu. Mungu anatupenda sote watenda mema na mabaya, bila kujali wala kutoa adhabu kwa yeyote. Kwa sababu kila mmoja yuko huru kutenda vyovyote kwa kutumia freewill iliyowekwa kutenda vyovyote.
Lakini hii ya kusema eti uko huru kutenda vyovyote lakini endapo utachagua kutenda mabaya, utachomwa moto. HII SIO FREEWILL, BALI NI MTEGO WA KUNASA WATU, WAKA UNGUE MOTO.🔥
Uhuru na hiyari kamili havipaswi kuwa na shuruti, shinikizo, vitisho au adhabu.
Vinginevyo huyo Mungu kama alikuwa hataki mabaya yafanyike, angeumba binadamu wema tu, watakao tenda mema siku zote na wakati wote.
Freewill inayo tegemea mabaya hiyo ni freewill ya mchongo. Na ni mtego!
I'm out.
Seran, Mallerina, Lax Al Mukheef secretarybird Poor Brain Lamomy
Iceberg9