Tafadhali kama una msimamo mkali wa dini ishia hapa usiendelee kusoma.
Nilikuwa kijiweni muda mfupi uliopita nacheza mchezo wa Draft. Kaja jamaa mmoja baada ya salamu jamaa mungine akauliza muda ili awahi kuondoka, akajibiwa kwamba ni saa moja na robo.
Sasa shida ikaanza kwa yule mgeni wetu, akatuuliza munawajua Freemasons? Nikajibu nawasikia kwamba ni mtandao wa matajiri wakubwa duniani. Jamaa akanicheka akasema umepotea kaka, hao ni waabudu shetani na wametushika kila kona. Nikambishia nikasema si kweli. Ndipo akaja na somo la saa au mfumo wa kusoma saa.
Akaanza kwa kuuliza sasa ni saa ngapi? nikamjibu saa moja. Akaniuliza hapo kwenye saa yako imeandikwa ngapi? Nikamjibu saba. Akasema emheeee hapahapo ndipo wametushika. Akauliza munajua kwa nini saa moja iandikwe saba? Nikajibu sijui. Akauliza munajua 666 alama ya mpinga kristo? Nikamjibu nasikiaga. Ndo sasa akaanza hesabu zake kama ifuatavyo.
1. Saa moja inaandikwa saba: 7-1= 6
2. Saa mbili inaandikwa nane: 8-2= 6
3. Saa tatu Tisa: 9-3= 6
4. Saa nne kumi: 10-4=6
5. Saa tano 11: 11-5 =6
6. Saa sita 12: 12-6= 6
7. Saa saba 13: 13-7=6
8. Saa nane 14: 14-8=6
9. Saa tisa 15: 15-9= 6
10. Saa kumi 16: 16-10=6
11. Saa kumi na moja 17: 17-11=6
12. Saa kumi na mbili 18: 18-12=6
Hapo akauliza mumenisoma? Wote tukajibu ndio mzeee.
Akasema kwa masaa 12 mengine Freemason wamefanya kama ifuatavyo.
1. Saa moja inaandikwa 19: 19-1=18=6+6+6
2. Saa mbili 20: 20-2=18=6+6+6
3. Saa tatu 21: 21-3=18=6+6+6
4. Saa nne 22: 22-4= 18=6+6+6
5. Saa tano. 23: 23-5= 18=6+6+6
6. Saa sita 24: 24-6= 18= 6+6+6
Hivyo kuanzia saa saba usiku inarudia tena kama hapo juu kabisa kuanzia namba 1-6. Hivyo tukabaki kimyaaa. Akasema ndo maana yeye hatumii mfumo wa 24hrs anatumia 12hrs system.
Sasa niwaulize wanajamvi kuna ukweli wowote hapa? Je nikweli Freemasons walivuruga saa makusudi? Je kuna ubaya kutumia 24hrs system?.
utajutia ulichokiandika
An idle mind is a workshop of the devil.... Huu upuuzi unaweza ukawa umeanzishwa na mtu mmoja anayejiita mkristu, licha ya wajibu wa kujenga ufalme wa Mungu ('ufalme wako ufike') yeye yuko busy kujenga ufalme wa giza..'
Ni kweli wamevuruga wao ....kuna cku jmaa mmoja alielezea clouds tv
lkn kwa kingereza
Vipi! Umepandwa na wazimu..
Hata hao clouds unadhani kuna mwenye akili timamu..?
wasabato......
ufunuo 13:18,"Hapa ndipo penye hekima.Yeye aliye na akili,na aihesabu hesabu ya mnyama huyo,maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake ni mia sita.sitini na sita."hii habari ya 666 imeandikwa kwenye biblia.Kwa hiyo maana ya kauli yako ni kwamba wasabato ndio wanaoijua vizuri biblia,sivyo?au biblia ni kitabu cha wasabato tu?hilo fungu limezungumza jambo moja zito msilolijua,si wote watakaojua mambo haya,bali ni wale wenye "akili" ya kuielewa "hekima" inayozunguka elimu hii.kama huna hiyo "akili" hata ufundishwe vipi "hekima" hii hautaelewa.sasa nadhani ndugu yangu utaitafsiri vizuri kauli yako kwa mapana yake.
Mkuu hapo jamaa kuna uhuni anafanya na hizo namba anazikorogakoroga anapata hiyo 666. Lengo kutuvuruga tu. Nilijaribu kubishananae lakini alinishinda kwasababu yeye anaongea na data zake na alijipanga wakati mimi nilikuwa sina data na sikujiandaa.
Umeona uje utuvuruge na sisi?Yaani hawa Freemason akiyanani nahisi wameshachoka sasa maana kila kitu ni chao!Diamond kufanikiwa kimuziki ni freemason, kifo cha Kanumba Freemason khaaaa!
Freemason ni nini!?tuanzie hapa
Dahh, we mbona mzito kuelewa hivyoo?Umeambiwa kule Jamii Intelligence kuna thread inayozungumzia kila kitu kuhusu Freemason, sa unaniuliza mi mwalimu wako?We vipi?
Kinanachonishangaza kuhusu huu uvumi wa 666 ni kuona watu wanakua na uoga usio na msingi. Miaka yote mtu uliyoishi mfano kama kweli hiyo 666 ina exist imekupunguzia au kukuongezea nini? The fear of the unknown ni kitu mbaya sana.
ufunuo 13:18,"Hapa ndipo penye hekima.Yeye aliye na akili,na aihesabu hesabu ya mnyama huyo,maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake ni mia sita.sitini na sita."hii habari ya 666 imeandikwa kwenye biblia.Kwa hiyo maana ya kauli yako ni kwamba wasabato ndio wanaoijua vizuri biblia,sivyo?au biblia ni kitabu cha wasabato tu?hilo fungu limezungumza jambo moja zito msilolijua,si wote watakaojua mambo haya,bali ni wale wenye "akili" ya kuielewa "hekima" inayozunguka elimu hii.kama huna hiyo "akili" hata ufundishwe vipi "hekima" hii hautaelewa.sasa nadhani ndugu yangu utaitafsiri vizuri kauli yako kwa mapana yake.
akili yako inapimwa na nani?na nini?wapi?kipimo kipi?
AKILI NI NINI?
Tuanzie hapa
Freemason ni nini!?tuanzie hapa
Vipi unafahamu "Great Disappointment".......Unajua ni kina nani waliosababisha....???
Mama Hellena na wenzake kina Miller unawafahamu . ..?