Freeman Mbowe Vs Sir Alex Ferguson

Mleta Post popote ulipo Mwanza hebu anza kupata Balimi baridiiii nitalipa. Umeandika vyema sana. Wanasiasa wanaotoka CHADEMA kuja CCM ni wanasiasa waliopikwa na Mbowe wakapikika. Ndio maana wakija huko ni uteuzi tu hakuna cha mchujo wala nini. Ukiona kazi imetangazwa wakaaply wengi na wewe ukaipata bila hata ya kufanyiwa interview, basi wewe ni mtu kiboko
 
huyo kamanda si wa kununuliwa
Agiza Jack Daniel nakuja kulipa. Mwambie na kumhakikishia jamaa kuwa wengine njaa hazijawahi kutuondoa katika uanaume wetu.
Tokea 1997 nimeiunga mkono Chadema kwa kusaidia kuijengea uwezo kwa kadri ya uwezo na nafasi nipatayo na sijadai fadhila hata mara moja zaidi ya kufurahishwa na juhudi zao za utetezi kwa wasio na sauti.
Nakumbuka zamani hizo nikiwa mikoa ya kanda ya kati nilipata kumuuliza marehemu Warid Kabouru akiwa Katibu Mkuu wa Chadema na mtu mwenye ushawishi mkubwa kama Mbunge wa kwanza kabisa wa upinzani, kuwa hivi huko tuendako hatuwezi kusalitiana? Akasema mwendo ni mdundo tuu!
Imagine hapo nilikaribisha ujumbe wa viongozi akiwa na wenzake wanywe chai kwangu. Miaka kadhaa baadae nilibaki kusikitika tuu kwa alilolifanya.
Sisi tupo na tutakuwepo, hata Chadema ikifutwa watafuta chama bali itikadi itabaki moyoni tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa.. Ndo maana mara nyingi wanalialia kuwa amedumu sana
 
Kama CCM ilivyompika Lowassa akaja chadema mkamkabidhi na chama kabisa pamoja na ugombea magogoni!
 
Itikadi gani itakayobaki moyoni mwako?!
 
Ukiwa na nafasi ya kufanya jambo usiitumie vibaya maana kuna watu wanatafuta hata sehem ya kuongelea matatizo yao wanakosa.
What a shame! Thread mbovu ya mwaka 2018 ndo hii, unalinganisha vitu ambavyo habadani haviwezi kulinganishika.
Kumjua Sir Ferguson kwenye mpira ndio unakuja kupost ujinga kama huu.?? Shame on you.

Tutumie kalamu na majukwaa kama haya vizuri...huwezi kuandika ujinga kama huu.

Inasikitisha sana tena sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Falsafa za mpira na siasa ni tofauti...
Mpira ni biashara, mpira unajumuisha chakato nyingi sana mpaka kuwa na timu imara. Kumbuka pia kwenye mpira watu wanahodhi madaraka na kumiliki hivi vilabu. Miliki inaweza kuwa ya aina mbili, mosi ya wanachama kama vilabu kadhaa tunavyovijua na pili za watu binafsi kama tunavyojua pia.

Mbowe ana mazuri yake na nina mkubali sana tena sana ila kumfananisha na Sir Ferguson HAPANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea kwa HISIA KALI sana JIWE wa puuzi wake wanaamini wakifuta Chadema wameua upinzani NO upinzani uko mioyoyoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu mpinge kwa Evidence kwamba wanaotoka Chadema wanakumbana na Teuzi Direct

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu mpinge kwa Evidence kwamba wanaotoka Chadema wanakumbana na Teuzi Direct

Sent using Jamii Forums mobile app
Sipingi na sitopinga hali ya kisiasa hapa nchini kwetu maana sijihusishi na siasa na sitokuja kujihusisha kamwe ila nachopinga DIRECT ni mleta mada (kilichoandikwa) kumfananisha Sir Alex Ferguson na Mbowe...huu ni ujinga kiwango cha lami ya barabara ya mwendo kasi.

Unafananishaje meneja wa mpira, ambae anafundisha soka tu...tena sio soka, alikua kwenye kablu ya soka inayomilikiwa na watu binafsi. Je unataka kusema uyu anaefananishwa nae iki chama ni chake binafsi (kuna tetesi zinasema ivyo maana hataki kubanduka kwenye kiti)..???

Kabla hatujatumia kalamu zetu narudia tena na tena tuwe WAANGALIFU MNOOOO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hili ni andiko la kishujaa sana lililojaa ukakamavu mtupu !

Hongera sana Kamanda .
 
Hukumuelewa mleta mada , ambaye ana akili sana na anafahamu soka na siasa ni tofauti bali alichotaka watu wafahamu ni uwezo mkubwa wa Bilionea Mbowe kwenye siasa za Tanzania akifananisha na uwezo wa Ferguson kwenye soka enzi zile.

Labda kama ulikuwa umelenga tu kupiga kelele hapa jf ili kupata airtime
 
Hebu basi wewe tumia kalamu yako kumfanabisha Mbowe na Ferguson tuone!
 
Tapatapa lakini mleta Uzi sasa hivi anakunywa Balimi na samaki mkubwa pale ndama igoma baada ya kuleta bandiko zuri
 
Mbona unataka kupasuka? Unajua maana ya comparison? Umeambiwa kabisa ugwiji wa Ferguson katika soka ndio kama wa Mbowe katika siasa, kwamba ni watu never say die sasa usichoelewa ni nini?
Hakuna aliyesema Alex na Freeman wakiingia kwenye soka pamoja inakuwaje au wakiingia kwenye siasa inakuwaje. Ukitaka kusoma andiko ukiwa tayari na chuki yako huwezi kuelewa zaidi ya kupotoka.
Tuliza akili kisha tafakari kijana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…