PreGE2025 Freeman Mbowe: Niseme nini? Tukiongea watasema tunawashwawashwa, wasemao ni wenye mamlaka!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
Mbowe.jpg

Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza sababu ya kukaa kimya tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho, Januari 22, 2025, akisema wanaotakiwa kusema kwa sasa ni viongozi waliokabidhiwa mamlaka na chama.

Katika uchaguzi huo, Tundu Lissu alishinda nafasi ya uenyekiti kwa kupata asilimia 51.5 dhidi ya Mbowe (asilimia 48.3), huku John Heche akishinda nafasi ya makamu mwenyekiti dhidi ya Ezekia Wenje.

Soma pia: Ukimya wa Mbowe

Tangu wakati huo, Mbowe aliyetangaza kuwa atajikita kwenye biashara zake, amekuwa kimya, licha ya misukosuko iliyoibuka ikiwamo ya kuibuka kundi la G55 lenye makada wengi waliomuunga mkono, ambao sasa baadhgi yao wametangaza kukihama chama hicho.

Soma pia: Wataka Mbowe ajitokeze

Alipoulizwa sababu ya kuwa kimya, Mbowe alisema: “Niseme nini? Wasemao ni wenye mamlaka.. wasije wakadai "tunawashwawashwa.”

Kauli ya Mbowe imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob maarufu Boniyai, kutangaza kwamba hakihami chama hicho na kuwaonya baadhi ya makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe.
 
Huyu ana kinyongo ndio maana hata mahakamani anashindwa kwenda.

Hakusoma alama za nyakati na kufanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi kama ambavyo hata Mama Abduli hataki kusoma alama za nyakati na kufanya maamuzi ya busara angali mapema.

Sisi wengine ni watu wadogo sana, tunachofanya ni kushauri tu, ila muda ndio kila kitu.
 
Mnamchokonoa sana, mnataka aongee mpate pa kuanzia.

Chadema ina uongozi yeye aongee nini?

Mjumbe wa kamati kuu siyo pake yake kwanini msitake wajumbe wengine waongee, wao hawaoni hao wanaohama?
 
View attachment 3339031
Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza sababu ya kukaa kimya tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho, Januari 22, 2025, akisema wanaotakiwa kusema kwa sasa ni viongozi waliokabidhiwa mamlaka na chama.

Katika uchaguzi huo, Tundu Lissu alishinda nafasi ya uenyekiti kwa kupata asilimia 51.5 dhidi ya Mbowe (asilimia 48.3), huku John Heche akishinda nafasi ya makamu mwenyekiti dhidi ya Ezekia Wenje.

Soma pia: Ukimya wa Mbowe
Tangu wakati huo, Mbowe aliyetangaza kuwa atajikita kwenye biashara zake, amekuwa kimya, licha ya misukosuko iliyoibuka ikiwamo ya kuibuka kundi la G55 lenye makada wengi waliomuunga mkono, ambao sasa baadhgi yao wametangaza kukihama chama hicho.

Soma pia: Wataka Mbowe ajitokeze

Alipoulizwa na JamiiForums leo Mei 19, sababu ya kuwa kimya, Mbowe alijibu kwa njia ya WhastApp: “Niseme nini my brother!? Wasemao ni wenye mamlaka.... wasije wakadai "tunawashwawashwa.”

Kauli ya Mbowe imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Boniface Jacob maarufu Boniyai, kutangaza kwamba hakihami chama hicho na kuwaonya baadhi ya makada wa chama hicho wanaohama wakitumia jina la Mbowe.
Ni kweli wenye madaraka ndo wenye haki ya kuwasha na kuwashwa
 
Ni busara kukaa kimya,japo kimya kingi kina mshindo mkuu,akibadilisha gia angani,
Tutamkuta kwenye ilani ya ubwabwa.
 
Nilitegemea Mbowe angetoa tamko kuhusu G55. : “Niseme nini my brother!? Wasemao ni wenye mamlaka..

Mbowe ni Coin-artist 🤧
 
Kinyongo cha nini ana pesa ,biashara zake ndani ya nchi na nje haishi kwa tonetone kama nyie na lisu wenu
Trump ambaye ni trilionea aliendesha Kampeni zake kwa tone tone. Halafu wakati wa "join the chain" mliosema kuwa anakula zile Hela siyo nyie?

Mara mseme CHADEMA ni chagadema, mara ni saccos yake, Leo mnamsifia kuliko hata watoto zake!
 
Huyu ana kinyongo ndio maana hata mahakamani anashindwa kwenda.

Hakusoma alama za nyakati na kufanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi kama ambavyo hata Mama Abduli hataki kusoma alama za nyakati na kufanya maamuzi ya busara angali mapema.
Yaani kuna kitu mnamdai Mbowe?Kawaachia Chama baada ya Uchaguzi bado mpo obsessed. Ni inferiority complex ya hali ya juu.
 
Back
Top Bottom