Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Anaandika Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe.
Nawashukuru wote mliojitekeza kwa wingi Mahakamani siku ya jana, hata nilipokuwa Polisi Kati juzi Alasiri, nawashukuru wanachama,wapenzi wa Chama chetu cha CHADEMA, ndugu,jamaa na marafiki kwa maombi ya kila mmoja wenu katika hili.
Kwa pamoja tushikamane kupigania haki katika Taifa letu kuhakikisha Katiba, Sheria na taratibu zilizopo zinafuatwa, sio Kiongozi mwenye mamlaka juu ya wengine aamue yeye atakavyo bila kufuata Katiba, Sheria na taratibu zinavyoelekeza.
Hapa sipiganii haki yangu tu bali Watanzania wote ambao wananyasika kwa kutopewa haki zao za msingi, lakini huu ni mwanzo wa kupigania nchi irejee katika utawala bora unaofuata Katiba, Sheria na taratibu za nchi.
Kwa pamoja tupiganie haki kwa nguvu zote kuliko kipindi kingine chochote hapo nyuma.
Asante sana.